COASTAL UNION KUKIPIGA NA COMBINE POLISI TANZANIA.

August 08, 2013
Na Oscar Assenga,Tanga.
TIMU ya Coastal Union "Wagosi wa Kaya"wanatarajia kucheza mechi ya Kirafiki na timu ya Combine Polisi Tanzania Iddi Pili katika uwanja wa Mkwakwani mjini hapa ikiwa ni maandalizi ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania bara ambao utaanza Agosti 24 mwaka huu.

Akizungumza na Blog hii,Mwenyekiti wa Klabu ya Coastal Union,Hemed Aurora alisema maandalizi ya mechi hiyo yamekamilika kwa asilimia kubwa na kinachosubiriwa ni siku ya mchezo huo.

Aurora alisema timu hiyo itaingia mkoani hapa leo jioni tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao Coastal Union  unautumia kwa umuhimu mkubwa wa kujiimarisha kabla ya kuanza msimu mpya wa Ligi kuu hapa nchini.

Aidha alisema kwenye mchezo huo pia utakuwa ni maalumu kwa ajili ya kuwatambulisha wachezaji wao wageni akiwemo kiboko wa Yanga na Simba kutoka klabu ya URA ya Uganda Yayo Lutimba ambaye alisajiliwa na timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili .

Aidha aliongeza kuwa mechi nyengine itachezwa leo kati ya timu ya Coastal Union B ambao watawakabili Kilimani ya Zanzibar mchezo ambao unatarajiwa kuwa na upinzani mkubwa kwa timu zote.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »