MKUU wa wilaya ya Lushoto, Alhaj Majid Mwanga
(juu Pichani)amewaagiza wevyeviti wa vijiji na maafisa watendaji wa Kata na Vijiji kuhakikisha
wanawachukulia hatua ikiwemo kuwapeleka mahakamani wazazi ambao wameshindwa
kuwapeleka watoto wao shuleni na kuendelea kuwaacha majumbani pamoja na kuwapeleka
mijini wakafanye kazi za ndani na kuuza karanga.
Alisema ni suala la ajabu sana mzazi ambaye
anaona mtoto wake amefaulu na kuchukia badala ya kufurahia huku wengine
wakiwashawishi kufanya vibaya mitihani yao ya mwisho ili watakapomaliza shule
washindwe kuendelea na masomo hali hii lazima tuikemee kwa mikoni miwili kwani
italeta adhari kubwa sana kwa vizazi zijavyo.
Aidha aliwataka watumishi kuacha kufanya kazi
kwa mazoea badala yake wafanya kwa uzalendo kwa kuwahi makazini kwa wakati
pamoja na kuchukizwa kwa matokeo yaliyotokea mwaka uliopita hivyo waongeze
bidii katika uwajibikaji wao ili kuweza kusukuma mbele gurudumu la maendeleo
kwenye maeneo yao.
Aidha aliwataka wanafunzi kusoma kwa bidii na
kuacha kudanganyika na vijana ambao wanaweza kuwarubuni na kuwaaribia masomo
yao pamoja badala yake wasome ili baadae waweze kupata matunda yanayotokana na
elimu na kuwa na maisha mazuri.
Mwisho.
EmoticonEmoticon