Benki ya CDRB yatoa msaada wa mbegu za mahindi kwa waathirika wa mafuriko Rufiji

May 31, 2024

 

Rufiji. Tarehe 29 Mei 2024: Kutokana na mafuriko yaliyotokea katika msimu wa masika mwaka huu, Benki ya CRDB imekabidhi msaada wa mbegu za mahindi zenye thamani ya shilingi milioni 50 kwa wananchi wa Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani.

Benki ya CRDB imekabidhi kilo 7,148.857 za mbegu za kisasa za mahindi zitakazosambazwa kwa wananchi ili wazitumie katika msimu ujao wa kilimo kuhakikisha wanakuwa na chakula cha uhakika.
Akikabidhi msaada huo uliopokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Mheshimiwa Meja Edward Gowele, Bi. Tully Esther Mwambapa ambae ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa Benki ya CRDB na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya CRDB Bank Foundation amesema taarifa za athari zilizosababishwa na mafuriko yaliyotokea zimewasikitisha watu wengi ndio maana imekuwa rahisi kwao kutoa msaada huo  utakaosaidia kurudisha shughuli za kilimo kwa uhakika.

“Majanga yana athari kubwa zinazorudisha nyuma uchumi wa watu na maendeleo ya taifa kwa ujumla. Mara zote, hutokea na kutukuta tukiwa hatujajipanga kukabiliana nayo au hatuna uwezo wa kuyazuia yasitokee. 
Hii ndio sababu iliyoishawishi Benki yetu ya CRDB pamoja na kampuni zake tanzu kushirikiana bega kwa bega na Serikali kukabiliana na majanga pindi tu yanapotokea ili kurejesha hali ya kawaida kwa waathirika,” amesema Tully.

Tully amesema walipopata maombi ya uhitaji wa mbegu hizo kutoka kwa Waziri wa TAMISEMI na Mbunge wa Jimbo la Rufiji, Mheshimiwa Mohammed Mchengerwa kwa ajili ya waathirika wa mafuriko, hawakufikiria mara mbili kwani waliona ni jambo jema litakalowasaidia waathirika kupunguza athari walizopitia na kurejesha hali zao kiuchumi.
Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Meja Edward Gowele ameishukuru Benki ya CRDB akisema kitendo ilichokifanya cha kuwakumbuka na kuwakimbilia waathirika wa mafuriko yaliyotokea ni cha kizalendo na kinachopaswa kuigwa na wengine.

“Moyo wangu na kichwa changu kama ilivyo kwa wana Rufiji wengi leo, vimejaa shukrani nyingi. Tunawashukuru sana Benki ya CRDB kwa kutukimbilia kipindi hiki kigumu. Msaada huu wa mbegu za mahindi mnaotukabidhi leo umekuja kwa wakati muafaka kwani utatusaidia kujikwamua kutoka katika athari za mafuriko kwa kupunguza gharama za kilimo hivyo kutuhakikishia mavuno msimu ujao,” amesema Meja Gowele.
Mkuu huyo wa wilaya amesema mvua nyingi zilizonyesha mwaka huu zimesababisha mafuriko ambayo yameharibu mazao yaliyopandwa shambani na hata baadhi ya biashara hivyo kuwarudisha wananchi wengi kwenye lindi la umasikini.

Kwa msaada uliokabidhiwa, Meja Gowele amewahimiza wananchi wa Rufiji kutumia huduma za Benki ya CRDB kurudisha shughuli zao za uchumi kama ilivyokuwa kabla ya kutokea kwa janga hilo la asili na kujijenga zaidi kimapato.
“Hakuna namna nzuri ya kuiunga mkono Benki ya CRDB zaidi ya kutumia huduma zake,” amesisitiza Meja
Sambamba na msaada huo, Taasisi ya CRDB Bank Foundation imetoa mafunzo ya ujasiriamali na elimu ya fedha kwa wanawake na vijana wilayani humo ili kuwaandaa kwa ajili ya kunufaika na mtaji wezeshi utakaosaidia kuinua uchumi wao.

Tully amesema mafunzo hayo yanaratibiwa na Programu ya Imbeju ambayo mpaka sasa imeshawajengea uwezo zaidi ya wajasiriamali 350,000 pamoja na kuwapa mtaji wezeshi wa jumla ya shilingi bilioni 10 nchini kote.

“Kupitia programu hii ya IMBEJU leo hii tutakwenda kutoa mafunzo kwa wanawake na vijana juu ya namna gani programu hii inaweza kuwasaidia kukuza biashara zao na shughuli zao za kiuchumi ikiwamo biashara na kilimo. 
Wataalamu wetu kutoka CRDB Bank Foundation watatoa mafunzo ya ujasiriamali na kuainisha fursa zinazoambatana na programu hii ikiwemo ile ya matumizi ya nishati safi kwa wanawake wanaojihusisha na biashara ya chakula maarufu kama mama lishe,” amebainisha Tully.

Kuhusu mafunzo kwa wajasiriamali hao, Meja Gowele amesema anaamini maarifa watakayoyapata yatakuwa na manufaa makubwa kwa washiriki, familia zao na jamii nzima kwa ujumla wake.
 Gowele.
“Naomba nichukue fursa hii kuwaeleza kuhusu fursa iliyo mbele yenu ya kunufaika na Programu ya Imbeju ambayo ni mahsusi kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali vijana na wanawake. Rufiji ina kila kitu kinachohitajika kwa mjasiriamali kujikwamua kiuchumi na Benki ya CRDB kupitia taasisi yake ya CRDB Bank Foundation inatoa mafunzo na mitaji wezeshi ili kuwakomboa wananchi kiuchumi.

 Niwaombe, tuzitumie fursa hizi tutakazoelezwa leo hii kuwa umakini ili wenye sifa wapate mitaji hii na wale ambao bado hawajatimiza vigezo, wahakikishe wanavikamilisha ili kwa pamoja tuujenge upya uchumi wa wilaya yetu,” amesema Mkuu wa Wilaya Gowele. 

DMI YAJIVUNIA KUZALISHA WATAALAMU WENYE UWEZO MKUBWA

May 30, 2024

Na Oscar Assenga,Tanga

CHUO cha Bahari cha Jijini Dar es Salaam(DMI) kimeshiriki maonyesho ya Elimu,Ujuzi na Ubunifu Jijini Tanga huku wakijivunia kutoa wataalamu wenye uwezo mkubwa wa kusanifu na kuzikarabati meli kupitia Temesa na hivyo kuondoa uhaba uliokuwepo awali nchini .

Akizungumza leo na waandishi wa habari katika Banda lao lililopo eneo la Shule ya Sekondari Popatlaly kunakofanyika maadhimisho ya elimu,ujuzi na ubunifu Captain Mohamed Kauli alisema wameshirika kwa lengo la kueleza wanachokifanya ikiwemo utoaji wa elimu na mafnzo kuhusu ubaharia ufanisi wa meli,usafirisha majini,utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi na ujenzi wa meli .

Alisema awali chuo hichajibwa o kilikuwa kinazalisha mabaharia wakati kilipoanzishwa lakini ili kukabiliana na ombwe la ukosefu wa ajira kutokana na vijana wengi kumaliza vyuo na kukosa ajira na wahitimu haoo wanafaida kubwa mbili wanapohitimu chuo kupata ajiri nchini kwenye sekta ya usafirishaji majini na nje ya nchi kwenye meli.

“Kwa kweli tumekuwa tukizalisha idadi kubwa ya mabaharia wanaofanya kazi nje na ndani ya nchi, kuna gepu kwenye wataalaamu wenye gani ya uchimbaji wa mafuta na gesi baharini lakini pia gepu la upatikanaji wa meli za mafunzo, awali zimekuwa zikiagizwa kutoka nje kwa gharama kubwa”Alisema

Alisema lakini sasa Serikali imetengeza wataalamu wanaotoka kwenye chuo hicho ambao wanajenga meli,kuzisanifu ,kuzikarabati kwenye eneo hilo serikali kupitia Temesa wanajenga na kukabarati meli hizo hapa hapa nchini.

Awali akizungumza mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho,Masaka Julias alisema kwamba mafunzo ambayo wanayapata kwenye chuo hicho yamewawezesha kubuni vitu mbalimbali hivyo kuwawezesha wanapomaliza kuweza kujiajiri kupitia ujuzi walioupata.

Alisema kwamba kwa sasa kupitia mafunzo hayo unawasaidia kutengeneza vitu mbalimbali vya ubunifu huku akieleza wamebuni wazo la kutengeneza roboti kuhamisha mizigo na ya kufunga vifuniko kwenye chupa za bidhaa mbalimbali.


SERIKALI YATANGAZA NAMNA WALIMU WAPYA WATAKAVYOAJIRIWA

May 30, 2024


Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia  Profesa  Adolf Mkenda akizungumza  wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya hali ya ufaulu na ujifunzaji wa wanafunzi ulioshirikisha wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo maafisa elimu mikoa, Halmashauri,Wakurugenzi na Taasisi uliofanyika Jijini Tanga 
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia  Profesa  Adolf Mkenda akizungumza  wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya hali ya ufaulu na ujifunzaji wa wanafunzi ulioshirikisha wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo maafisa elimu mikoa, Halmashauri,Wakurugenzi na Taasisi uliofanyika Jijini Tanga 
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof Caroline Nombo akiungumza  
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini (NECTA) Dkt Said Mohamed akizungumza 
MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian akizungumza 
Meza kuu wakifuatilia 


Na Oscar Assenga, TANGA

SERIKALI imetangaza mkakati wa uboreshaji wa elimu nchini huku ikieleza walimu ambao wataajiriwa ni wale wataokuwa wamefanya mitihani yao na kufaulu vizuri tofauti na ilivyokuwa awali ambapo wizara ilikuwa ikijaza nafasi zilizokuwa zikihitajika bila kupitia mchakato huo .

Mkakati huo wa serikali umetangazwa na Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia  Profesa  Adolf Mkenda aliyasema hayo leo Jijini Tanga wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya hali ya ufaulu na ujifunzaji wa wanafunzi ulioshirikisha wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo maafisa elimu mikoa, Halmashauri,Wakurugenzi na Taasisi

Alisema kwamba wanaoona jambo hilo sio jema kwao lakini wajiulize kwanini madaktari wanapomaliza Shahada ya kwanza wanalazimika kufanya mitihani ndio wanafanya kazi hivyo suala hilo linapelekwa kwa walimu ili kuweza kupata walimu bora.

Waziri Profesa Mkenda alisema kwamba wanaamini kigezo hicho ndio ambacho kitalivusha Taifa na watahakikisha wanachukua walimu waliobora zaidi na watakaofanya mitihani na kufaulu vizuri.

“Kama tunataka tuboresha elimu lazima twende kwa ujasiri tunapojaribu kuajiri walimu tujiulize tunapigania mwanao apata mwalimu bora sasa tutakapo ajiriw lazima wafanye mtihani na watakaofeli hawatapata nafasi”Alisema

Alisema lakini walimu waliopo watalindwa mpaka watakapostaafu na tutaendelea kuwajengea uwezo kwani Rais anatenga fedha nyingi kwenye elimu halafu tujitenge, haiwezekani lazima tathimini tunayoifanya lazima iendelee na hatua nzuri za baraza hatufurahii kufutia mitihani watahaniwa na waliojaribu kuiba mitihani”Alisema .

Aidha alisema kwa sasa wapo kwenye mchakato wa Sheria mpya ambayo itawabana watu watakaobainika kuiba mitihani watakamatwa kushtakiwa kwa kesi za uhujumu uchumi na kwenye hilo niwashukuru Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) kwa kufanya kazi nzuri wanayoifanya.

“Katika jambo hilo tuzidi kuwa makini tusijikuta tukazubaa tukaanguka Necta msilegeze kamba nendeni kuhakikisha mnalisimamia na takwimu ni muhimu zitatueleza vizuri tunakwendaje na katika hilo tunataka kuimarisha takwimu za elimu Tanzania na kazi hii imeanza na timu ipo kazini”Alisema Waziri Profesa Mkenda

Awali akizungumza Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof Caroline Nombo alilipongeza Baraza la Taifa Mitihani (Necta) kwa taarifa yao ya uwasilishaji wa Taarifa ya Tathimini ya ujifunzaji kwa wanafunzi wa kidato cha pili.

Alisema kwamba taarifa iliyowasilishwa inatoa picha halisi kuhusu na ufundishaji na ujifunzaji kwa shule za Sekondari na msingi nchini na mapendekezoo yaliyotolewa yanaonyesha dira ya nini cha kufanya ili kuhakikisha ufundishaji na ujifunzaji na tathimini katika ngazi ya shule unaimarika.

Alisema Wizara hiyo itaendelea kushirikiana bega kwa bega na wadau wote wa elimu na baraza la mitihani kuhakikisha masuala yote ya ufundishaji na tahimini yanaimarishwa kwa lengo la kukuza umahiri wa wanafunzi katika masomo hayo.

“Vile Wizara kupitia Baraza la mitihani tutaendelea kuhakikisha kuwa tathimini ya ujifunzaji wa wanafunzi wa kidato cha pili awamu ya pili ya mwaka 2025 itafanyika kwa ufanisi mkubwa”Alisema

Naye kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini (NECTA) Dkt Said Mohamed alisema suala la kufanya tathimini ni muhimu ili kuboresha kiwango cha elimu na wamekuwa wakifanya tathmini na mitihani na kueleza tahimini hiyo katika maeneo mbalimbali ni kutaka kujua maendeleo ya wanafunzi wamesoma na wanataka kufika wapi.

Alisema wamesema wameanza kufanya tathimini na masomo manne ambayo yameyafanya wakianzia na somo la kwanza ni Hisabati,Sayansi huku akieleza kwamba katika somo hilo katika mtihani wa darasa la saba mwaka huu utakuwa hauna maswali ya kuchagua

Aidha alisema pia alisema hali ya ufauli nchini ukiangalia takwimu upimaji darasa la nne kwa miaka 10 uliopo ufaulu wa jumla umekuwa juu ya asilimia 80 itapanda kidogo na kushuka,miaka 10 hiyo utaona namna ya watahiniwa imekuwa ikiongezeka .

“Mfano mwaka 2015 darasa la nne laki tisa sasa kwenye usajili wanafikia mpaka 1,800,000 na ufaulu wameendelea kubakia 80 asilimia na namba ya watahiniwa imeongezeka mwaka hadi mwaka”Alisema

Katibu huyo alisema kwa upande wa Daraja la saba ulikuwa ni asilimia 67 mwaka 2015 na umeendelea kupanda na kufikia asilimia 80 mwaka 2023 kimahesabu huo ni ufaulu unaoafanana na bado wameendelea kufika asilimia 80 huku akieleza kwa upande wa Sekondari kidato cha pili ufaulu 2015 mpaka 2023 umekuwa ukiongezeka kutoka asilimia 67 2015 mpaka kufikia asilimia 89 mwaka jana.


ASILIMIA 90 YA WANAFUNZI WAPO KWENYE HATARI KUBWA YA KUGONGWA BARABARANI

May 29, 2024




Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga (DAS) Dalmia Mikaya akikata utepe kushirikia uzinduzi wa mradi wa uwekezaji wa miundombinu ya usalama barabarani kwa shule za Msingi Azimio na Makorora Jijini Tanga ambao unaotekelezwa na Shirika la Amend Tanzania na kufadhiliwa na Ubalozi wa Uswis nchini,kushoto ni Kaimu Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Tanga (RTO) Rajab Mhumbi akifuatiwa na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Amend Tanzania Simon Kalolo na kulia ni Mwakilishi wa Balozi wa Uswis nchini Rashid Mbaramula


Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Dalmia Mikaya (kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Amend Tanzania Simon Kalolo(Kulia) wakifungua kitambaa ikiwa ni uzinduzi wa mradi wa uwekezaji wa miundombinu ya usalama barabarani kwa Shule za Msingi Azimio na na Makorora Jijini Tanga ambao unaotekelezwa na Shirika la Amend Tanzania na kufadhiliwa na Ubalozi wa Uswis nchini
Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga (DAS) Dalmia Mikaya kulia akiwa amemshika mkono mwanafunzi wa shule ya Msingi Azimio akiashiria uzinduzi wa mradi wa uwekezaji wa miundombinu ya usalama barabarani kwa Shule za Msingi Azimio na na Makorora Jijini Tanga ambao unaotekelezwa na Shirika la Amend Tanzania na kufadhiliwa na Ubalozi wa Uswis nchini,kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Amend Tanzania Simon Kalolo
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Amend Tanzania Simon Kalolo kulia akisisitiza jambo kwa Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Dalmia Mikaya na viongozi wengine wa Halmashauri ya Jiji la Tanga uzinduzi wa mradi wa uwekezaji wa miundombinu ya usalama barabarani kwa Shule za Msingi Azimio na na Makorora Jijini Tanga ambao unaotekelezwa na Shirika la Amend Tanzania na kufadhiliwa na Ubalozi wa Uswis nchini
Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Dalmia Mikaya akizungumza mara baada ya  kuzindua mradi wa uwekezaji wa miundombinu ya usalama barabarani kwa Shule za Msingi Azimio na na Makorora Jijini Tanga ambao unaotekelezwa na Shirika la Amend Tanzania na kufadhiliwa na Ubalozi wa Uswis nchini
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Amend Tanzania Simon Kalolo akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa uwekezaji wa miundombinu ya usalama barabarani kwa Shule za Msingi Azimio na na Makorora Jijini Tanga ambao unaotekelezwa na Shirika la Amend Tanzania na kufadhiliwa na Ubalozi wa Uswis nchini
 Mwakilishi wa Balozi wa Uswis nchini Rashid Mbaramula akizungumza wakati wa wa uzinduzi wa mradi wa uwekezaji wa miundombinu ya usalama barabarani kwa Shule za Msingi Azimio na na Makorora Jijini Tanga ambao unaotekelezwa na Shirika la Amend Tanzania na kufadhiliwa na Ubalozi wa Uswis nchini

Naibu Meya wa Jiji la Tanga Rehema Mhina akizungumza wakati wa wa uzinduzi wa mradi wa uwekezaji wa miundombinu ya usalama barabarani kwa Shule za Msingi Azimio na na Makorora Jijini Tanga ambao unaotekelezwa na Shirika la Amend Tanzania na kufadhiliwa na Ubalozi wa Uswis nchini
 Sehemu ya wanafunzi wa shule ya Msingi Makorora Jijini Tanga wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa uzinduzi wa mradi wa uwekezaji wa miundombinu ya usalama barabarani kwa Shule za Msingi Azimio na na Makorora Jijini Tanga ambao unaotekelezwa na Shirika la Amend Tanzania na kufadhiliwa na Ubalozi wa Uswis nchini


Na Oscar Assenga, Tanga

ASILIMIA zaidi ya 90 ya wanafunzi katika shule za Msingi Makorora na Azimio jijini Tanga wapo kwenye hatari kubwa ya kugongwa na pikipiki,magari na vyombo vyengine vya moto.

Hatua hiyo imelilazimu Shirika la Amend Tanzania kutekeleza mradi wa uwekeji wa miundombinu salama ya barabara katika shule hizo ili kuwaepusha na ajali wanazoweza kukumbana nazo.

Akizungumza leo katika uzinduzi wa mradi wa miundombinu salama ya barabaraani katika Shule ya Msingi Makorora na Azimio jijini Tanga, Meneja Mkazi wa Shirika la Amend Tanzania Saimon Kalolo wakati wa uzinduzi wa Miundombinu salama ya barabarani katika shule za Msingi Makorora na Azimio Jijini Tanga .

Alisema wameamua kutekeleza mradi huo kunatokana na wanafunzi hao kutembea kwenda na kurudi shuleni kila siku hivyo kuwaweka katika hatari kubwa ya kugongwa na pikipiki, magari na vyombo vingine vya moto.

“Takribani wanafunzi wasiopungua 8 katika shule hizi mbili wamejeruhiwa katika ajali za barabarani katika muda wa miezi 12 iliyopita zote zikihusisha pikipiki”Alisema

Alisema baada ya kushauriana na wadau wa shule hizo wakiwemo wanafunzi na walimu, wanajamii, viongozi wa dini, viongozi wa serikali za mitaa, Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) na Jeshi la Polisi Amend kupitia msaada kutoka kwa Ubalozi wa Uswisi na washirika wake wa serikali.

Alisema baada ya kushauriana wameweka miundombinu salama kwa lengo la kuzuia ajali za barabarani ikiwemo njia za waenda kwa miguu, matuta, vivuko vya pundamilia, alama za barabarani, na elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi wote.

“Tumezindua miundombinu mipya ya kuokoa maisha ya watembea kwa miguu hasa watoto katika Shule za Msingi Makorora na Azimio”Alisema

Aliongeza kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), watoto wanaotembea kwa miguu ni miongoni mwa makundi yaliyo katika hatari kubwa ya kupata majeraha ya barabarani nchini Tanzania.

“Tofauti na watoto katika nchi zilizoendelea wengi wa watoto wa shule katika maeneo ya mijini mkoani Tanga, na Tanzania kwa ujumla, wanatembea kwenda shule bila kusindikizwa na mtu mzima”Alisema

Alisema pia kwa Bara la Afrika watoto wako katika hatari kubwa ya kupoteza maisha kutokana na ajali za barabarani ikilinganishwa na eneo lingine lolote duniani.

“Kwa bahati nzuri njia za kuzuia ajali hizi zinaeleweka vizuri ikiwa ni pamoja na kuwaepusha watoto na msongamano wa magari na kupunguza mwendo kasi wa magari katika maeneo ambayo watoto wanavuka barabara”Alisema

“Mradi huu unaungwa mkono na Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania na una bajeti ya shilingi za Kitanzania 424,983,396 (takriban Faranga za Uswisi 150,000)”Alisema

Aliongeza mradi huo ulianza Septemba mwaka 2023 ambapo shughuli nyingine za mradi zimejumuisha mafunzo ya waendesha pikipiki (bodaboda) 300 ndani ya Jiji la Tanga, waendesha pikipiki 253 mkoani Dodoma ikiwemo kampeni ya uhamasishaji kuhusu masuala ya usalama wa pikipiki, na kuanzishwa kwa 'Kanuni za Maadili' kwa waendesha pikipiki 200 zaidi watapewa mafunzo jijini Tanga ifikapo Juni 2024.”

BARRICK YASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA HEDHI SALAMA DUNIANI KWA VITENDO

May 28, 2024

 

Meneja Mawasiliano wa Barrick nchini, Georgia Mutagahywa (wa pili kushoto) akikabidhi taulo za kike kwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mwananyamala B,Modeta Mushi, zilizotolewa na kampuni hiyo kwa ajili ya kuwasitiri watoto wa kike.Wengine pichani ni Afisa Mawasiliano wa Barrick, Neema Ndossi na Mkaguzi wa Polisi Kitengo cha Usalama barabarani Amina Said.

Na Mwandishi Wetu.

Katika dhamira yake ya kuhakikisha Watoto wa kike na wanawake wanapata elimu kuhusu umuhimu wa usafi katika kipindi vya hedhi, Barrick Tanzania imeshiriki maadhimisho ya siku hii ambayo⁹ huadhimishwa Mei 28 kila mwaka ambapo wafanyakazi wake walishiriki kugawa taulo za kike kwenye makundi mbalimbali yenye mahitaji ikiwemo kwa wanafunzi wa shule ya msingi zilizopo jirani na maeneo ya migodi yake ya North Mara, Bulyanhulu na ofisi ya Dar es Salaam.Vile vile imeshirikiana na Jeshi la Polisi Kitengo cha usalama barabarani kutoa elimu ya usalama kwa Wanafunzi.

Wanawake wengi na wasichana katika jamii zetu hupata changamoto kubwa katika kipindi cha mzunguko wao wa mwezi wa siku za hedhi, kutokana na kutoweza kumudu kununua pedi za kutumia,ukosefu wa elimu kuhusiana na hali hiyo.imani za mila ambazo zinawafanya wengi kuamini kuwa suala la hedhi halipaswi kuongelewa,ukosefu wa mazingira rafiki ya kujihifadhi mtu anapokuwa kwenye hali hiyo kama vile vyoo na maji safi ya kutumia. Changamoto hizo zote zinasababisha watumie vifaa vya kuwasitiri visivyofaa ambavyo vinaweza kuwasababishia kupata maradhi.
Wanafunzi wakipatiwa mafunza ya usafi katika hedhi na usalama kutoka kwa wafanyakazi wa Barrick na Jeshi la Polisi
---
Barrick inaamini Siku ya Usafi wa Hedhi Salama Duniani ni maalumu kwa ajili ya kuvunja ukimya na kujenga ufahamu kuhusu umuhimu mkubwa wa kutunza usafi wakati wa hedhi. Siku hii inaangazia changamoto mbalimbali ambazo wanawake na wasichana kote duniani wanakabiliana nazo kuhusiana na hedhi, ambazo zinaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa afya zao, elimu yao na hali yao ya maisha kwa ujumla.

Kwa kuunga mkono siku hii muhimu, Barrick inachangia katika kujenga jamii yenye usawa, afya, na ufahamu zaidi, ambapo kila mwanamke na msichana anaweza kujitunza kwa ujasiri na heshima wakati wa hedhi yake.
Wanafunzi wa shule ya msingi Mwananyamala B wakifurahia zawadi za taulo za kike walizopewa kwa ajili ya kuwasitiri.

NMB YATOA FURSA KWA VIJANA WENYE BUNIFU MBALIMBALI HAPA NCHINI

May 28, 2024

 

MENEJA wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Baraka  Ladislaus akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho hayo ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Elimu Profesa Adolf Mkenda ambapo alisema kwamba benki hiyo inatambua umuhimu wa ubunifu katika maendeleo ya nchi.
MENEJA wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Baraka  Ladislaus kulia akifurahia Waziri wa Elimu Profesa Adolf Mkenda kushoto wakati alipotembelea banda lao wakati wa ufunguzi wa maadhimisho hayo 



Na Oscar Assenga, Tanga.

BENKI ya NMB imeshiriki kwenye maadhimisho ya wiki ya elimu, ujuzi na ubunifu yanayoendelea kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlaly huku wakitoa fursa kwa vijana wenye bunifu mbalimbali kwenda kufanya majaribio kwenye benki hiyo.

Hayo yalisemwa leo na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini wakati wa ufunguzi wa maadhimisho hayo ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Elimu Profesa Adolf Mkenda ambapo alisema kwamba benki hiyo inatambua umuhimu wa ubunifu katika maendeleo ya nchi.

Alisema kwamba wao kama benki pamoja na ufadhili wanatoa Jukwaa Maalumu (Platfom) kuwakaribisha vijana kufanya ubunifu, maendeleo ya kibunifu na miradi hiyo wamekuwa wakiifadhili.

“Kwa niaba ya Benki ya NMB niwaambie kwamba tunatambua umuhimu wa ubunifu na ndio maana tumeungana nanyi katika wiki hii kwa kuwa elimu ndio inachochea ubunifu sisi kama Benki pamoja na mfadhili tunatoa jukwaa maalumu kuwakaribishasha vijana kuja kufanya ubunifu kufanya maendeleo ya kibunifu na miradi hiyo tunaifadhili”Alisema

Hata hivyo alisema kwamba na inasaidia kuleta chachu ya kuendelela kuleta mendeleo ya ubunifu Tanzania hivyo wataendelea kuwaunga mkono kuhakikisha maendeleo ya sekta hiyo yanapiga hatua kubwa.

“Mh Waziri niwakaribiha vijana wenye bunifu mbalimbali waje kufanya majaribio yao kwenye benki ya NMB tuna platfomu NMB Sign Box nzuri inatoa nafasi nzuri ya bunifu tupo tayari kushirikiana nao kama Wizara kuhakikisha ubunifu unaleta chachu ya maendeleo ya kiuchumi hapa nchini”Alisema

Awali akizungumza wakati akifungua maadhimisho hayo Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda Serikali imesema ipo katika mchakato wa kujenga shule 100 za mafunzo ya Amali nyanja ya ufundi nchi nzima ili kuwawezesha vijana wa kitanzania kuweza kujiajiri au kuajiriwa kupitia ujuzi watakaopata kupitia vyuo hivyo.

Kwa upande wake Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Pastrobas Katambi amesema dunia ya sasa ina mabadikiko makubwa hasa kwenye masuala ya sayansi na teknolojia ujuzi na ubunifu hivyo ni wakati wa vijana wa kitanzania kwenda sambamba na mabadiliko hayo.

Awali Katibu mkuu wizara ya elimu sayansi na teknolojia Profesa Carolyne Nombo alisema wanafunzi 27 walishinda shindano la ujuzi na ubunifu ngazi ya vyuo ambao watafanyiwa mchakato na kupatikana wanafunzi 3 wa fani tofauti ambao watakwenda kushiriki mashindano ya kikanda na kimataifa mapema mwaka 2025.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo Mhe. Husna Sekiboko amesema bunifu zinazoibuliwa katika maeneo mbalimbali nchini zitengenezwe katika uhalisia ili kuleta tija kwa jamii na kiuchumi.

Mwenyeji wa maadhimisho hayo ambaye ni Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Dkt. Batilda Buriani alisema mkoa wa Tanga umepokea trilioni 2 na milioni 600 kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya elimu ambapo shule mpya 27 zimejengwa pamoja na vyuo vya kati ambavyo vipo katika hatua mbalimbali.