WANAOTOROSHA KOROSHO KWENDA NJE YA NCHI WAONYWA, SIKU ZAO ZINAHESABIKA

March 31, 2024


Na Oscar Assenga, TANGA.


BODI ya Korosho Tanzania Mkoani Tanga imewaonya wakulima wenye tabia za kutorosha Korosho kwenda kuuza nje ya nchi kuacha mara moja kufanya hivyo kwani siku zao zinahesabika kutokana na vyombo vya dola vinawatambua na watapokamatwa watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Moja ya athari za utoroshaji wa Korosho kwenda nje ya nchi ni pamoja na kutokufikia malengo ya uzalishaji ikiwemo nchi mapato ambayo yangeweza kusaidia katika kuchochea maendeleo kwa wananchi wake.

Onyo hilo  na Kaimu Meneja wa Bodi ya Korosho Mkoa wa Tanga Atufigwege Mwakyagi wakati akizungumza na waandishi wa habari namna bodi hiyo ilivyojipanga kukabiliana na vitendo hivyo huku wakiwataka wenye tabia hizo kuacha mara moja

Alisema kwani kufanya hivyo maana yake ni kulihujumu zao hilo pamoja na juhudi za Serikali ni kuhakikisha wakulima wanapata bei nzuri na bora ili kuweza kujikwamua kiuchumi kupitia kilimo hicho chenye tija.

“Ndugu zangu mnaotorosha korosho kufanya hivyo ni kosa na vyombo vya dola hivyo tambueni siku zenu zinahesabika sisi kama bodi hatutakubali kuona watu wanahujumu zao hilo kwani zinatakiwa kumnufaisha mkulima na Rais wetu Dkt Samia Suluhu ameweka nguvu kuhakikisha mkulima anapata bei nzuri na bora”Alisema

Aidha alisema kwamba wale ambao wanafanya hivyo wanataka kufifisha juhudi za Serikali ambazo ni kuona wakulima wa zao hilo wananufaika nalo na hatimaye kuweza kujikwamua kiuchumi na kubadilisha maisha yao hivyo hawatakuwa tayari kuona zinakwamishwa kwa namna yoyote ile.

Kaimu Meneja huyo alisema mauzo ya korosho msimu uliopita yalikuwa ni tani 741 kwenye mnada uliofanyika wilayani Mkinga na kufanikisha kuingiza fedha kiasi cha Sh.Milioni 703 ambazo wakulima wa zao hilo wameweza kunufaika nalo.

Akizungumzia suala la udhibiti ubora wa zao hilo alisema kwamba wa sasa wamekuwa wakitoa mafunzo kwa wakulima ili kuweza kulima kilimo chenye tija ili kudhibiti ubora kuhakikisha unakuwa mzuri kabla ya kwenda sokoni ambapo wamekuwa wakiuza kwenye mfumo rasmi.

UPENDO NDIYO NGUZO YA MAFANIKIO YETU -(MB) KIKWETE

March 29, 2024

 Upendo ndiyo Nguzo ya Mafanikio yetu-Kikwete (MB) Maneno hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete alipokuwa anaongea na Viongozi wa Chama wa Halmashauri ya Chalinze alipowaalika kwenye Futari nyumbani kwake Msoga.


Futari hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama wilayani hapo akiwepo Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo Ndg. Abdul sharif Zahor na wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya kutoka kata zote za Jimbo la Chalinze ililenga kuwakutanisha viongozi wa wilaya ikiwa na malengo ya kuupokea mfungo wa mwezi wa Ramadhani, kuwaombea na kuwarehemu viongozi waliowahi kuongoza Wilaya hiyo na amani ya Wilaya hiyo na Wazee.







PAC YAIMIMINIA PONGEZI VETA KWA UJENZI BORA WA CHUO CHA VETA IKUNGI

March 29, 2024

 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore akitoa maelezo kwa kamati ya bunge ya PAC wakati Kamati hiyo ilipotembelea Ujenzi wa miundombinu wa Chuo ch VETA Ikungi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Carolyne Ndombo akizungumza kwenye kamati ya PAC kwenye mradi wa VETA.


Baadhi ya picha ya wajumbe wa kamati ya PAC walipotembelea ujenzi wa VETA Ikungi

KAMATI  ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeipa pongezi nyingi Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kwa ujenzi bora wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Ikungi. Mradi huo ulitekelezwa na VETA kwa kutumia nguvukazi za ndani (Force Account).

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baada ya kukagua chuo hicho, leo, tarehe 28 Machi 2024, wajumbe wa PAC wameonesha kuridhishwa kwa kiasi kikubwa na ubora wa majengo, miundombinu ya chuo na gharama za ujenzi zilizotumika, huku wakirejea na kuzungumzia tofauti na miradi mingine waliyoitembelea.


“Mmetutia moyo, tumetoka na moyo ulionyooka. Tulikuwa tumesononeka sana baada ya kutembelea miradi mingine iliyojengwa kwa utaratibu huu wa force account,” amesema Makamu Mwenyekiti wa PAC, ambaye pia ni Mbunge wa Vwawa, Mheshimiwa Japhet Hasunga.

Naye Mbunge wa Katavi na mjumbe wa Kamati hiyo, Mheshimiwa Mhandisi Isack Kamwelwe amesema ametumia muda mwingi kukagua majengo na miundombinu mbalimbali na kubaini kuwa kiwango cha ujenzi wa chuo hicho ni cha ubora wa hali ya juu.

“Mheshimiwa Mwenyekiti (wa PAC), nimezunguka maeneo mengi, kwenye karakana, vyoo na madarasa, kazi hii ni nzuri sana. Kwa force account, kazi hii ni excellent (bora kabisa). Hata majengo yamejengwa kwa spacing (kuacha nafasi), jambo ambalo linasaidia hata kupunguza madhara inapotokea majanga kama moto,” amesema.

Wajumbe wa Kamati hiyo ambayo miongoni mwa majukumu yake ni kutathmini thamani ya matumizi ya fedha za Serikali (Value for money), wamesema kuwa wameridhika kuona kuwa suala la thamani ya matumizi ya fedha limezingatiwa kwa kiasi kikubwa, hasa kwa kuangalia kiwango cha fedha kilichotumika na pamoja na chuo kuanza kudahili wanafunzi.

“Wakati naingia hapa, mimi nilistuka na kudhani kuwa wametumia pesa nyingi sana. Maana nikiangalia majengo yalivyojengwa kwa ubora, magrili kwenye milango na madirisha yalivyo mazito, nikadhani pesa nyingi sana itakuwa imetumika. Nilivyokuja kusikia taarifa kuwa imetumika shilingi 3 tu nimestaajabu sana. Ni kiwango kidoigo sana cha pesa ukilinganisha na majengo na miundombinu iliyojengwa. Hapa ndipo unaona value for money,” amesema Mheshimiwa Joseph Kakunda, Mbunge wa Sikonge na Mjumbe wa PAC.

Akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi wa chuo hicho, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore, amesema mradi huo wenye majengo 17 umetekelezwa na VETA kupitia chuo cha VETA Singida na ofisi ya VETA Kanda ya Kati katika hatua tofauti tofauti na kwamba utekelezaji wake umefikia asilimia 99.4.

“Majengo yote yamefikia asilimia 100 ya ujenzi, shughuli iliyobakia ni kuunganisha umeme (tail wire) kwa kila jengo kutoka kwenye nguzo za umeme zilizosambaza umeme katika eneo la chuo pamoja na kazi za nje,” amesema.

Amefafanua kuwa utekelezaji wa mradi huo umegharimu kiasi cha Shilingi 3,004,013,405.56, ambapo fedha za ujenzi ni shilingi 2,653,915,038.00 na utengenezaji wa samani ni shilingi 350,098,367.56.

WATANZAMIA TUMIENI FURSA KUPELEKA BIDHAA UINGEREZA

March 29, 2024

 


-Dkt. Kijaji: Watanzania tumieni fursa kupeleka bidhaa Uingereza.

Serikali imewashauri watanzania kutumia fursa ya mpango wa biashara wa Nchi zinazoendelea kwa kuhakikisha wanapeleka bidhaa katika nchi ya Uingereza ili kukuza Uchumi pamoja na pato la Taifa.

Mpango huo mpya umeanza kutumika mwaka jana 2023 ambapo Serikali ya Uingereza iko tayari kupokea bidhaa mbalimbali zinazozalishwa nchini zikiwemo zenye kulipiwa ushuru na zisizolipiwa.

Waziri wa Viwanda na Biashara,Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amesema hayo leo Dar es Salaam katika semina ya wafanyabiashara kuhusu fursa ya kuuza bidhaa katika soko la Uingereza na Nchi zinazoendelea (UK- DCTS).

Akizungumza Mhe.Dkt. Kijaji amesema mpango huo wa bishara na Nchi zinazoendelea kwa Tanzania umekuja muda muafaka kwa kuwa Nchi imerekebisha na kuboresha mazingira ya biashara ili kufanya kukuza kipato na biashara nchini.

Amesema kwa mwaka 2022 mauzo ya Tanzania kwenda Uingereza yalifikia sh. bil 44 ikilinganishwa na manunuzi ya sh. trilioni 3.08 ya bidhaa kutoka Uingereza.

Amesema kupitia takwimu hizo ongezeko la mauzo kwenda Uingereza ni ndogo sana ikilinganishwa na ununuzi wa bidhaa kutoka Uingereza Kwenda Tanzania kwani kwa miaka miwili imeongezeka sh. bilioni mbili wakati bidhaa zilizonunuliwa ni zenye thamani ya sh. triloni 1.06.

“Inahitaji nguvu ili kuweza kuvuka na kufikia malengo halisi ya kuanzishwa kwa mpango huo,” amesema Waziri Kijaji.

Aidha, ametolea mfano taarifa ya Kituo cha Uwekezaji nchini ( TIC) kuanzia mwaka 1997-2024 jumla ya miradi 980 ya kampuni ya Uingereza yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 5655.38 zilizotoa ajira za wastani wa watu 126,322 katika sekta mbalimbali ziliwekezwa nchini.

“ Tuweze kutumia mpango huo na kuchochea mapato pamoja na fedha za kigeni, lakini pia kupitia mpango huo Taifa litakuwa na manufaa mbalimbali ambayo ni kupungua kwa masharti ya kupeleka bidhaa na kwa wenye viwanda ni muhimu kuwa na malighafi zitakazochochea ushindani wa bidhaa za Tanzania,” amesema.

Ameongeza pia manufaa ya mpango huo ni kupungua kwa gharama za kufanya biashara kurahisisha upatikanaji wa taarifa za masoko kwa Tanzania na hata kushirikiana na kampuni za Uingereza kuwekeza na kuzalisha bidhaa bora Tanzania.

Amehamasisha wafanyabiashara kuona umuhimu wa uadilifu katika kuziona fursa na kwamba wapeleke bidhaa zinazokidhi soko hilo.

“Serikali yetu ya awamu ya sita imechukua hatua nyingi za kujenga mahusiano ya kidipolomasia na Uingereza ambapo Nchi hiyo pia ilianza kutoa fedha kupitia huduma mbalimbali ambazo zimeelekezwa katika Miradi mbalimbali,” amesema.

Mhe. Dkt.Kijaji ameongeza kuwa mpango huo umezingatia pia sekta ya biashara kwa kuongeza mchango wa sekta ya biashara katika ukuaji wa viwanda.

Akitoa ujumbe kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania David Cancar amesema chini ya mpango huo Tanzania ndio yenye bidhaa zinazotakiwa na Uingereza.

Amesema kupitia mpango huo kwa Pamoja kutakuwa na ongezeko kubwa la biashara kati ya Tanzania na Uingereza.

DKT. NCHEMBA AONGOZA MKUTANO WA WB KANDA YA AFRIKA

DKT. NCHEMBA AONGOZA MKUTANO WA WB KANDA YA AFRIKA

March 29, 2024

 

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiongozamkutano wa Benki ya Dunia wa Jukwaa la Tatu la Kanda ya Afrika Kundi la Kwanza kwa nchi za Kipato cha Kati lililolenga kujadili namna mashirika ya fedha ya kimataifa yanavyoweza kuongeza fedha kuzisaidia nchi za kipato cha kati kufikia maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii. Mkutao huo umefanyika kwa njia ya Mtandao, kutokea Jengo la Hazina (Treasury Square), jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiongozamkutano wa Benki ya Dunia wa Jukwaa la Tatu la Kanda ya Afrika Kundi la Kwanza kwa nchi za Kipato cha Kati lililolenga kujadili namna mashirika ya fedha ya kimataifa yanavyoweza kuongeza fedha kuzisaidia nchi za kipato cha kati kufikia maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii. Mkutao huo umefanyika kwa njia ya Mtandao, kutokea Jengo la Hazina (Treasury Square), jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akitoa wito kwa taasisi za fedha za kimataifakuongeza fedha kwaajili ya kuzisaidia nchi za kipato cha kati wakati akifungua mkutano wa Benki ya Dunia wa Jukwaa la Tatu la Kanda ya Afrika Kundi la Kwanza kwa nchi za Kipato cha Kati lililolenga kujadili namna mashirika hayo ya fedha yanavyoweza kuongeza fedha kwa nchi hizo. Mkutano huo umefanyika kwa njia ya Mtandao kutokea Jengo la Hazina (Treasury Square), jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi Amina Khamis Shaaban, wakifuatilia mambo mbalimbali wakati wa  mkutano wa Benki ya Dunia wa Jukwaa la Tatu la Kanda ya Afrika Kundi la Kwanza kwa nchi za Kipato cha Kati, ambapo Mhe. Nchemba aliongoza mkutano huo uliofanyika kwa njia ya mtandao, kutokea Jengo la Hazina (Treasury Square), jijini Dodoma.

Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Victoria Kwaka, akitoa mada wakati wa mkutano wa Benki ya Dunia wa Jukwaa la Tatu la Kanda ya Afrika Kundi la Kwanza kwa nchi za Kipato cha Kati, ambapo Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) aliongoza mkutano huo uliofanyika kwa njia ya mtandao, kutokea Jengo la Hazina (Treasury Square), jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizaraya Fedha, Bi Amina Khamis Shaaban na Afisa Mwandamizi wa Idara ya Fedha za Nje wa Wizara hiyo, Bw. John Kuchaka, wakifuatilia uwasilishwaji wa taarifa wakati wa mkutano wa Benki ya Dunia wa Jukwaa la Tatu la Kanda ya Afrika Kundi la Kwanza kwa nchi za Kipato cha Kati, ambapo Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) alikuwa Mwenyekiti wa mkutano huo uliofanyika kwa njia ya mtandao, kutokea Jengo la Hazina (Treasury Square), jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizaraya Fedha, Bi Amina Khamis Shaaban, akifafanua jambo wakati wa mkutano wa Benki ya Dunia wa Jukwaa la Tatu la Kanda ya Afrika Kundi la Kwanza kwa nchi za Kipato cha Kati, ambapo Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) aliongoza mkutano huo uliofanyika kwa njia ya mtandao, kutokea Jengo la Hazina (Treasury Square), jijini Dodoma.

Na. Peter Haule, WF, Dodoma

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ameongoza mkutano wa Benki ya Dunia wa Jukwaa la Tatu la Kanda ya Afrika Kundi la Kwanza kwa nchi za Kipato cha Kati uliolenga kujadili namna mashirika ya fedha ya kimataifa yanavyoweza kuongeza fedha kwa ajili ya kuzisaidia nchi za kipato cha kati ili ziweze kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika nchi zao itakayochochea ukuaji wa uchumi na maendeleo ya jamii.

Akifungua mkutano huo uliofanyika kwa njia ya mtandao jijini Dodoma, Mwenyekiti wa Mkutano huo, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba alisema kuwa Dunia inakabiliwa na migogoro mingi na changamoto za maendeleo ya kiuchumi ambazo zinasababisha kutofikiwa kikamilifu kwa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).

Alisema kuwa kupungua kwa nafasi ya kifedha katika kushughulikia migogoro hiyo kunadhoofisha uwezo wa Serikali za nchi hizo kufadhili programu za kijamii, kuharakisha ufufuaji wa Uchumi na pia kuongeza madeni katika nchi hizo.

“Mizozo inayoendelea nchini Urusi na Ukraine, Mashariki ya Kati na baadhi ya nchi nyingine za Afrika imechochea kupanda kwa bei ya vyakula na kuwasukuma mamilioni ya watu kwenye uhaba wa chakula”, alisema Dkt. Nchemba.

Aidha Dkt. Nchemba aliishukuru Benki ya Dunia kwa mchango wake wa kuzijengea uwezo taasisi katika kuyafikia maendeleo endelevu lakini pia kufufua uchumi kutokana na changamoto mbalimbali zinazotokea Duniani.

Vilevile alisema kuwa kukabiliana na changamoto zinazoikumba dunia sio kazi rahisi kwa nchi moja, hivyo ameomba kuwa na nguvu ya pamoja katika Kanda na Bara la Afrika katika kutafuta utatuzi wa changamoto hizo.

Dkt. Nchemba ameishukuru Benki ya Dunia kwa kummwamini kuongoza kikao hicho kikubwa lakini pia amewashukuru viongozi mbalimbali waliotoa mada ambazo zimewafunbua macho kwa kuona fursa zilizopo katika kukuza una kuwezesha biashara na pia kuwa na majadiliano mazuri wakati wa mikutano ijayo ya majira ya kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) itakayofanyika mwezi Aprili, 2024 jijini Washington D.C nchini Marekani.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Victoria Kwaka, alisema kuwa katika kipindi cha miaka mitano ilitoa misaada na mikopo nafuu yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni tatu kwa nchi za Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Alisema kuwa mwaka wa fedha uliopita Benki ya Dunia kupitia Mfuko wa IDA ilitoa dola bilioni 2.4 na kwamba kiwango cha misaada na mikopo hiyo imeendelea kuongezeka na miongoni mwa nchi zilizonufaika na mpango huo ni Tanzania, Kenya na Eswatini.

Aidha, Bi. Kwakwa amevitaja vipaumbele vya Benki hiyo kuwa ni pamoja na kuhakikisha nchi zitapata umeme wa uhakika, kuwa na maendeleo ya kidigitali, upatikanaji wa ajira, mapinduzi ya kiuchumi, kujenga uwezo kwa rasilimali watu na masuala ya elimu.

Baadhi ya Viongozi walioshiriki mkutano huo ni pamoja na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Victoria Kwakwa, Makamu wa Rais wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) Kanda ya Afrika, Bw. Sergio Pimenta, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia, Bi. Anshula Kant, Mawaziri wa fedha na Mipango (Magavana) na wajumbe wengine.

TEMESA TANGA YAZIDAI TAASISI ZA SERIKALI MADENI ZAIDI YA BILIONI 1.8 ,YAMO MADENI SUGU

March 29, 2024


Na Oscar Assenga,TANGA.

WAKALA wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA) Mkoani Tanga umesema kwamba unazidai Taasisi za Serikali madeni sugu ya zaidi ya Bilioni 1.8 ambao walikwenda kutengeneza magari yao katika karakana ya wakala huo ambapo mengine ni ya muda mrefu.

Hayo yalisemwa na Meneja wa Temesa Mkoa wa Tanga Mhandisi Jairos Nkoroka wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo alisema wanaziomba taasisi hizo kulipa madeni yao ili kuuwezesha wakala huo kuendelea kutekeleza shughuli zao kwa ufanisi.

Meneja huyo aliziomba taasisi hizo nazo ziweze kulipa madeni yao kutokana na kwamba nao pia wanadaiwa Bilioni 1.4 na wazabuni ambao wamekuwa wakipeleka vifaa kwa ajili ya kutengeneza magari

“Tunawakumbusha watulipe ili tuweze kuendelea kuwapa huduma kwani kutokufanya hivyo kunaweza kusababisha kutokupata huduma kwa wakati “Alisema

Aidha alisema kwamba madeni mengi ni ya nyuma ambayo wameyarithi na mengine wameyapeleka makao makuu yao kwa utaratibu mwengine na ya mwaka huu wanaendelea kuwadai kuhakikisha wanalipa

“Tumeanzia kitengo cha mahusiano kupitia mabalozi kwa kujenga mahusiano na hivyo kuzaidia wanaodaiwa kuanza kulipa madeni yao na tunaamini tutaendelea kupata mafanikio”Alisema

Aidha alisema ili kuweza kukabiliana na wadai hao sugu Temesa umeingia mkataba na wazabuni wakubwa (40) wa vipuri vya magari mkoani Tanga ili kuondoa ucheleweshaji ambao ulikuwepo hapo awali badala ya kuanza taratibu za manunuzi ambazo siku za nyuma zilikuwa zinawachelewesha.

Alisema wameamua kufanya hivyo ili kuweza kuhakikisha wanaondokana na ucheleweshwaji huo na kwa sasa wanachukua muda mfupi baada ya siku mbili.

Alisema mpango huo utasaidia kuwawezesha kupata vifaa ambavyo walikuwa hawana na vile vyengine ambavyo kwa hiyo kwa sasa ivi magari ya serikali yanayokwenda kufanyiwa matengenezo yanachukua muda mfupi sana na hatimaye kuruhusiwa kuendelea na shughuli zao.

“Hivi sasa tumeingia mikataba na wazabuni wakubwa na matengenezo ya magari ya Serikali yanatakiwa kutengenezwa na Temesa na tukishindwa kutengeneza kutokana na kitaaluma au vifaa kuna utaratibu ambao unafahamika na tunatoa vibali kwenda kwenye karakana nyengine na yanatrngezwa chini ya usimamizi wao”Alisema

“Katika ishu ya vifaa vya matengenezo ya magari tunatumia muda mfupi kulikagua gari na kubaini changamoto zake kutokana na uwepo wa vifaa vya kisasa “Alisema Jairos

Mwisho


DKT JAKAYA KIKWETE APONGEZA KASI YA UKUAJI TAASISI ZA FEDHA, AIPONGEZA

March 29, 2024

 Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete ameelezea kuridhishwa kwake na kasi ya ukuaji pamoja na uimara wa taasisi za fedha hapa nchini huku akizisisitiza taasisi hizo kuendelea kujiendesha kwa weledi zaidi ili ziweze kuongeza tija katika kuchochea ongezeko la uwekezaji na ukuaji wa uchumi wa nchi kupitia sekta mbalimbali ikiwemo biashara.


Akizungumza kwenye hafla fupi ya futari iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Dkt Kikwete aliitumia benki ya NBC kama mfano muhimu katika kuthibitisha uimara wa taasisi hizo ambazo pamoja na kuongeza viwango vya mikopo na huduma mbalimbali kwa wateja pia zimeweza kutengeneza faida kubwa na hivyo kuendelea kijiimarisha zaidi.

“Napotoa pongezi na shukrani naamanisha kwa dhati kabisa kwasababu mabadiliko (reforms) mengi ya taasisi ya kifedha yalifanyika mimi nikiwa Waziri wa Fedha kwa wakati ule hivyo najua vema tulipo sasa na tulipotoka. Leo hii nikiona mabenki yanatangaza faida kwa mabilioni ya fedha yananithibitisha wazi kabisa kuwa zile ‘reforms’ tulizozifanya kipindi kile zimefanikiwa,’’ alibainisha Dkt Kikwete huku akiitolea mfano benki ya NBC iliyotengenza faida ya sh bilioni 122 kwa mwaka uliopita.

Akitumia mifano na historia zaidi, Dkt Kikwete alitumia muda mwingi kuelezea namna wateja walivyopitia wakati mgumu kupata huduma za kifedha kwenye taasisi hizo kabla ya serikali kuingilia kati na kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kufunga na kubadili muundo wa uendeshaji na umiliki kwa baadhi ya benki hizo.

‘’Leo hii changamoto zote zimebaki historia. Fedha kwenye Uchumi ndio damu ya Uchumi. Sekta ya fedha ikiteteleka ndio chanzo cha uchumi kuporomoka. Uchumi wa nchi unategemea sekta ya fedha hivyo ikiteteleka kila kitu kinaharibika. Hivyo nawapongeza sana NBC na taasisi nyingine zote kwa kuendelea kutoa huduma zenu kwa weledi huku pia mkiendelea kujiimarisha kimitaji,’’ aliongeza.

Akizungumzia matukio ya benki hiyo ya kuandaa futari kwa ajili ya wateja wake kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini Dkt Kikwete alisema matukio kama haya yanaongeza imani kwa wateja wa benki hiyo kwa kuwa ni moja ya thibitisho kuwa uhusiano wa benki na mteja haushii kwenye biashara pekee bali pia unagusa imani za wateja.

“Matukio ya futari kama haya yanasababisha wateja wenu tunajisikia vizuri kwa kuwa tunaona kwamba tunahudumiwa na benki ambayo pia inajali maslahi yetu kiimani’’ aliongeza.

Awali akizungumzia hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi, alisema ni muendelezo wa utaratibu wa benki hiyo kwa miaka 15 sasa ikilenga kujumuika na wateja wake kama hatua ya kuonyesha mshikamano na umoja katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Alisema benki hiyo inaheshimu sana Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kutokana na ukweli kwamba, ni kipindi ambacho mwanadamu anajiweka karibu na Muumba wake kupitia mfungo na kufanya maombi.

“Huu ni mwezi ambao pia unatukumbusha kufanya kilicho chema mbele za Mungu wetu. Kwa kuwa NBC siku zote tupo karibu imani za wateja wetu tumeamua kuandaa futari hii ili kujumuika na wenzetu kufanikisha hilo.” Alisema Sabi.

Zaidi Sabi aliangazia huduma maalum ya benki hiyo, "La Riba," iliyoandaliwa kwa ajili ya wateja wenye imani ya kiislamu kwa kuzingatia kanuni za dini hiyo katika masuala yanayohusiana na fedha na mtazamo wa dini hiyo kuhusiana na riba.

‘’NBC ndio benki ya kwanza kubwa kuanzisha huduma za kibenki zinazozfuata misingi ya kisheria kupitia La Riba Banking ikiwemo akaunti za akiba na biashara kwa watu binafsi, wajasiriamali na makampuni makubwa. Benki pia inayo akaunti ya muda maalum (fixed deposit) inayofuata misingi ya sharia yaani ‘Mudharaba’. Zaidi kupitia dirisha hilo la La Riba tunatoa huduma ya mikopo kwa wafanyanyabiashara wakubwa na wa kati, wajasiriamali wadogo na wafanyakazi wa sekta ya umma na sekta binafsi,’’ alibainisha Sabi.

Hafla hiyo ya futari ilihudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini wakiongozwa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Walid Alhad Omar, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.



Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete (kushoto) akipokea zawadi maalum kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (Kulia) wakati wa hafla futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wa jijini Dar es Salaam jana. Hafla hiyo ilifanyika jana jijini humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.



Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete (pichani) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo ilifanyika jana jijini humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.



Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (kulia) akimkaribisha Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo ilifanyika jana jijini humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.


Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Walid Alhad Omar (pichani) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo ilifanyika jana jijini humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.



Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (pichani) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo ilifanyika jana jijini humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.



Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla hiyo.



Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete (katikati walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa benki ya NBC pamoja na wateja wa benki hiyo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake jijini humo . Hafla hiyo ilifanyika jana jijini humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.

Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NBC wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake jijini humo. Hafla hiyo ilifanyika jana jijini humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.

MAADHIMISHO SIKU YA VIWANGO AFRIKA; TBS YATOA ZAWADI KWA WASHINDI WA MASHINDANO YA INSHA.

March 29, 2024

 Shirika la Viwango Tanzania ( TBS ) , Leo Machi 28, 2024 limeadhimisha siku ya viwango Afrika na kutoa vyeti na zawadi kwa Washindi 10 Bora wa Mashindano ya Insha ambapo Washindi wa nafasi tano za Mwanzo watashiriki Mashindano ya Insha Afrika.


Akizungumza katika Hafla iyo iliyofanyika makao makuu ya TBS Jijini Dar Es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Hassan Bomboko ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Albert Chalamila , amelipongeza Shirika la Viwango Tanzania kwa kazi na Jitihada kubwa za kuhakikisha Watanzania wanafikiwa na Bidhaa zilizo Bora hasa katika kipindi hiki cha Miaka Mitatu ya Serikali ya awamu ya SITA inayooongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

" Niwapongeze TBS kwa kuadhimisha siku hii muhimu kwa namna ya Kitofauti lakini pia niwapongeze washiriki wote zaidi ya 300 waliojitokeza kushiriki mashindano ya Insha hadi sasa tumewapata 10 bora , nyinyi kama wataalamu wetu wa badae wa masuala ya Viwango mmefanya jambo kubwa sana , Juzi wakati tukiadhimisha miaka mitatu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan TBS ni moja kati ya Mashirika yaliyofanya vizuri niwapongezeni sana " alisema Mhe. Bomboko

Akitoa Historia ya Siku ya Viwango Afrika , Mkurugenzi Mkuu TBS , Dkt. Athuman Ngenya amesema
" Shirika la Viwango Afrika lilianzishwa mwaka 1977 likiwa na jukumu kuu la Kuoanisha viwango Afrika ili kukuza biashara na kupunguza vikwazo vya Kibiashara barani Afrika pamoja na kuimarisha ukuaji wa Viwanda Afrika .