TRA TANGA WAADHIMISHI SIKU YA SHUKRANI KWA KUWAKATIA BIMA YA AFYA WATOTO 25

November 26, 2022
 Kaimu Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo Opra Msuya kulia akisisitiza jambo kwa Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure wakati walipowatembelea wakati wakiadhimisha sherehe za shukrani  ambapo walitembelea wodi ya watoto kwenye Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo kugawa misaada mbalimbali ikiwemo kuhaidi kutoa fedha za matibabu za wagonjwa wawili kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji.


Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure kulia akimkabidhi mmoja msaada ya vitu mbalimbali Kaimu Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo Opra Msuya

Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure akizngumza mara baada ya kukabidhi msaada huo







Na Oscar Assenga,TANGA.

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga imeadhimisha sherehe za shukrani  kwa kuwatembelea wodi ya watoto kwenye Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo kugawa misaada mbalimbali ikiwemo kuhaidi kutoa fedha za matibabu za wagonjwa wawili kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji.

Ugawaji wa msaada huo wenye thamani ya Milioni 3.5 ulitolewa katika wodi ya watoto katika halfa iliongozwa na Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure akiwa ameambatana na maafisa mbalimbali wa mamlaka hiyo na watumishi.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo kwa uongozi wa Hospitali hiyo Meneja Specioza alisema kwamba wao katika kuadhimisha wiki ya shukrani kwa mteja waliona watoe shukrani kwa walipa kodi wao kwa kuwapatia msaada huo.

Alisema kwamba walishakutana na wafanyabiashara wao na kwamba katika kipindi hiki wamekuwa na utaratibu wa kuwambuka jamii inayowazunguka hivyo wameona kutembelea hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo kutembelea wodi ya watoto.

Meneja huyo alisema kwamba wametoa shukrani kwa jamii kutokana na kwamba wamaani jamii ikiwa imara na afya bora na kodi itaongezeka maana wanapokuwa na afya ndipo wana pata nguvu za kufanya biashara na kulipa kodi stahiki.

“Tumeona tuje tuwaone watoto tujue matatizo yao na tunalengo la kuwakatia bima ya afya watoto 25 kwa sababu kuna watoto wengi wanahitaji bima lakini wakati tunaendelea na watoto wao tumetembelea pia wodi ya watu wazima tukakutana na wagonjwa wawili.

Alieleza kwamba wagonjwa hao walikuwa wanahitaji msaada wa kufanyiwa upasuaji ambao ni Frank na Mzee Hamisi na hivyo watatoa fedha kuwasaidia waweze kuwafanyiwa upasuaji ikiwa ni kusheherekea sherehe ya kuwashukuru walipa kodi na jamii kwa ujumla.

Awali akizungumza wakati akipokea msaada huo. Kaimu Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo Opra Msuya aliwashukuru Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga kwa kuwapatia msaada huo wagonjwa hasa kwa ajili ya wenzao wenye uhitaji mungu awabariki wanawaomba wasiiishie hapo waendelee kujitolea.

Hata hivyo kwa upande wake mmoja wa wagonjwa ambaye alipatiwa msaada wa kufanyiwa upasuaji Frank Beda anayetokoea wilayani Muheza aliyegongwa na aliyehusika na tukio hilo alikimbia aliwashukuru TRA kwa kuwapatia msaada huo na kwamba mwenyezi mungu awabariki sana katika maisha yao

Mwisho.

TRA TANGA YAKUSUDIA KUKUSANYA ZAIDI YA BILIONI 232 MWAKA WA FEDHA 2022/2023

November 24, 2022

Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure akizungumza na waandishi wa habari baadaa ya kuzungumza na walipa kodi katika hafla fupi ya kuwapongeza kwa ulipaji wa kodi kwa mwaka wa fedha 2021/2022 waliovuka lengo ambapo waliibuka kidedea katika mikoa yote Tanzania. 

Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure akizungumza na waandishi wa habari baadaa ya kuzungumza na walipa kodi katika hafla fupi ya kuwapongeza kwa ulipaji wa kodi kwa mwaka wa fedha 2021/2022 waliovuka lengo ambapo waliibuka kidedea katika mikoa yote Tanzania. 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kanda ya Kaskazini Selestini Kiria  akizungumza 

Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure akikata keki 
Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure kushoto akimsikiliza mfanyabiashara Wilbard Mallya
Sehemu ya wafanyabiashara wakiwa kwenye halfa hiyo

Na Oscar Assenga,TANGA.


MAMLAKA ya Mapato Tanzania Mkoani Tanga (TRA) leo wamekutana na kuzungumza na walipa kodi Mkoani Tanga katika halfa iliyokwenda sambamba na kuwapongeza kwa ulipaji kodi wao wa mwaka wa Fedha 2021/2022 ambao uliiwezesha kuvuka lengo na kuibuka kidedea katika mikoa yota nchini.

Halfa hiyo ilikwenda sambamba na kuwatembelea wateja wakubwa mkoani Tanga ikiwemo wafanyabiashara katika eneo la barabara ya 14 Jijini Tanga na Kiwanda cha PPTL ambako walizungumza nao.

Akizungumza wakati wa halfa hiyo Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure alisema kwamba mamlaka hiyo kwa mwaka wa fedha 2022/2023 inakusudia kukusanya kodi kiasi cha shilingi Billioni 232.69 ikiwa ni malengo ya serikali sawa na ongezeko la asilimia 37 ya mwaka wa fedha uliopita.

Alisema kutokana na uwepo wa Kutokana na ongezeko hilo alitumia fursa hiyo kuwataka wafanyabiashara mkoa humo kuendelea kushirikiana kikamilifu na mamlaka ya mapato katika kuhakikisha wanalipa kodi kwa wakati na kwa hiari ili kuweza kufikia malengo yaliyowekwa ya kuendelea kung’ara katika ukusanyaji wa kodi hapa nchini

Meneja huyo alisema mamlaka hiyo kuibuka kidedea ni kutokana na walipa kodi wa mkoa wa Tanga kulipa kodi na hivyo kuwawezesha kufanya vizuri katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 .

Alisema kwa mkoa wa Tanga walikuwa wamepangiwa lengo la kukusanya billion 169.68 lakini wao wameweza kukusanya billioni 207.52 ikiwa ni sawa na asilimia 121.6% hivyo waliwashukuru kwa kuwawezesha kufikia lengo hilo.

Meneja huyo alisema pia katika mwaka wa fedha 2022/2023 lengo lao la ukusanyaji limeongezeka na kufikia bilion 63 ambayo ni sawa la ongezeko la asilimia 37% ya lengo la mwaka huu ni bilion 232.69 kwa hiyo wana kazi kubwa ya kufanya.

Alisema kwa sababu mwaka uliopita waliweza hatua ambayo imepelekea mwaka huu wameongezewa lakini katika hayo yote hatukuweza pekee yetu bali ni ushirikiano wenu wadau na hivyo kuweza kulipa kodi kwa hiari

Hata hivyo Meneja huyo aliwataka wafanyabiashara katika mkoa huo kuhakikisha wanaendelea kulipa kodi pamoja na kutekeleza maagizo ya serikali ya kulipa kodi kupitia mfumo wa kielektroniki.

“Lakini pia niwatake kutoa taarifa kwa mamlaka ya mapato pale panapotokea changamoto yoyote ikiwemo ya kusitisha biashara au kuhama”alisema

Awali akizungumza Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kanda ya Kaskazini Selestini Kiria aliipongeza mamalaka hiyo kwa mafanikio waliyoyapata kwa mwaka wa fedha uliopita.

Sambamba na hilo pia amewaomba kuendelea kuboresha huduma zao ili kuzidi kuwavutia wateja kuweza kulipa kodi kwa wakati.

Akizungumza wakati alipotembelewa kwenye duka lake Mfanyabiashara Wilbard Mallya aliipongeza mamlaka hiyo kwa huku akiiomba Serikali kuwaangalia wafanyabiashara kwenye suala la kodi pamoja na kurahisisha utoaji wa huduma.




CHUO CHA BANDARI CHAJIVUNIA KUTOA WATAALAMU BORA NCHINI

November 21, 2022

Afisa Msajili katika Chuo cha Bandari Pendo Mtinangi akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Tanga katika viwanja vya Bandari kunakoendelea Mashindano ya Shimuta kuhusu umuhimu wa chuo hicho

Afisa Msajili katika Chuo cha Bandari Pendo Mtinangi akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Tanga katika viwanja vya Bandari kunakoendelea Mashindano ya Shimuta kuhusu umuhimu wa chuo hicho

Afisa Uhusiano wa Chuo cha Bandari Edda Mmari akizungumza na waandishi wa habari leo


Afisa Utawala Mwandamizi katika chuo hicho Halima Kagobe akizungumza

Mratibu wa mafunzo ya muda mfupi John Leonard akizungumza




Chuo cha Bandari kimejivuna kutoa wataalamu bora wengi ambao wamekuwa ni chachu ya mafanikio katika sekta ya uchukuzi na nyingine hapa nchini.

Hatua hiyo inatokana na takwimu kuonyesha kuwa fursa ya ajira kwa wahitimu wake ni zaidi ya asilimia 90 huajiriwa katika maeneo mbalimbali ya sekta ya uchukuzi Nchini .

Hayo yalibainishwa Leo naAfisa Utawala Mwandamizi katika chuo hicho Halima Kagobe wakati wakizungumza na waandishi wa Habari Jijini Tanga katika viwanja vya Bandari kunakoendelea Mashindano ya Shimuta

Ambapo alisema kuwa Kutokana na umahiri wa uwepo miundombuni bora ya kujifunza umefanya chuo hicho kuweza kutoa wanafunzi ambao wanahitajika katika soko la ajira.

Alisema kuwa kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia ambayo chuo hicho kinakwenda sambamba Kwa kuweka mitambo ya kisasa pamoja masomo ambayo ya yanaendana na hitajio la soko la ajira.

"Chuo chetu kinajukumu la kuandaa wataalamu ambao wataweza kutumika na TPA pamoja na sekta nzima ya uchukuzi kutokana na mafunzo ambayo wanayatoa Kwa Wanafunzi wao"Alisema Kagobe

Awali akizungumza Mratibu wa mafunzo ya muda mfupi John Leonard alisema kuwa kozi za uendeshaji wa mitambo Kwa kipindi cha miaka ya hivi karibu imepata mwitikio mkubwa na vijana wa jinsia ya kike.

Alisema kuwa mafunzo yanayotolewa katika chuo hicho sio tuu yameweza kunufaisha wananchi wa hapa nchini pekee hadi nje ya nchi hususani zilizoko katika ukanda wa Afrika ya Mashariki.

Alisema wanatoa kozi za utalaamu katika maeneo ya Bandari na usimamizi wa shughuli za forodha wanayo makundi mawili ya kozi za muda mfupi ambazo wanayatoa kwenye chuo cha Bandari .

Mratibu huyo alisema kwamba upande wa kozi ya vyombo vya kuendesha mashine mbalimbali zinazotumika Bandari ikiwmo uendeshaji wa vyombo vya winch na vyengine ambavyo zimefungwa kwenye Bandari kubwa hapa nchini ikiwemo za Dar na Mtwara.

Naye kwa upande wake Afisa Uhusiano wa Chuo cha Bandari Edda Mmari alisema wameshiriki kwenye mashindano ya Shimuta yanayoendelea Jijini Tanga ili kutangaza chuo hicho ambacho kimekuwa kikitoa wataalamu mbalimbali katika sekta ya uchukuzi hapa nchini

Alisema pia Michezo hiyo inaunganisha taasisi mbalimbali na wao ni sehemu yao na wanatoa huduma kwa wananchi hivyo wamekuja kutangaza chuo cha Bandari ambacho kinatoa kozi za muda mrefu na mfupi hivho waliona ni muhimu kushiriki ili kuwaelezea umuhimu wake na uwepo wake hivyo wanawakaribisha watu wote kufika kujiunga na chuo hicho na wao wapo tayari kuwahudumia .


Mwisho




TPDC YALAZIMISHWA SARE NA BMH MICHUANO YA SHIMUTA TANGA

November 19, 2022

 

KOCHA wa timu ya TPDC Bizoo Bituka akitia maelekezo kwa wachezaji wake
Kikosi cha timu ya TPDC kilichocheza dhidi ya BMH leo kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Tanga School.

Na Oscar Assenga,TANGA.

TIMU ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) imelazimishwa sare tasa ya kutokufungana na timu ya Benjamini Mkapa Hospitali (BMH) ikiwa ni muendelezo wa Michuano ya Shimuta inayoendelea kutimua vumbi Jijini tanga.

Mchezo huo uliochezwa kwenye Dimba la Shule ya Sekondari Tanga Ufundi ulikuwa wa aina yake kutokana na kila timu kutaka kuondoka na alama tatu na hivyo kuzidisha upinzani .

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo Kocha wa timu ya TPDC Bizoo Bituka amesema malengo yake makubwa ilikuwa ni kupata pointi tatu muhimu lakini hata pointi moja aliyoipata wanashukuru. Alisema pamoja na uwepo wa ushindani katika michuano hiyo lakini wao wamejipanga na kujiimarisha kuhakikisha wanapata alama tatu kila mchezo ili kuweza kutimiza malengo yao ya kunyakua ubingwa wa mchezo huo.

Sehemu ya kikosi ambacho kiliwakilisha timu ya TPDC katika mchezo wa leo ni Nahodha Dalushi Shija, Oscar Mwakasege, Peter Ngalu, Mwikabe Muhono.



Mwisho

TRA, KCMC ZATOSHANA NGUVU MICHUANO YA SHIMUTA TANGA

November 16, 2022


Mshambuliaji wa timu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kulia akiwani mpira dhidi ya timu ya KCMC wakati wa michuano ya Shimuta inayoendelea kutimua vumbi kwenye viwanja vya Mizani Jijini Tanga
Mshambuliaji wa timu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kulia akiwani mpira dhidi ya timu ya KCMC wakati wa michuano ya Shimuta inayoendelea kutimua vumbi kwenye viwanja vya Mizani Jijini Tanga
Mshambuliaji wa timu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kulia akiwani mpira dhidi ya timu ya KCMC wakati wa michuano ya Shimuta inayoendelea kutimua vumbi kwenye viwanja vya Mizani Jijini Tanga








NA Oscar Assenga, TANGA

TIMU za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mabingwa Watetezi kwa upande wa mpira wa Miguu na Hospitali ya Rufaa KCMC ya Kilimanjaro zimetoshana nguvu baada ya kufungana bao 1-1, katika michuano ya Shimuta inayoendelea Jijini Tanga.

Mchezo huo ambao ulifanyika kwenye viwanja vya Mizani Jijini Tanga ulikuwa na upinzani mkubwa kwa kila timu kutaka kupata matokeo mazuri jambo ambalo lilizidisha ugumu wa mchezo huo

Timu ya KCMC ndio walikuwa wa kwanza kupata bao la kupitia Yusuph Madili aliyepiga faulu ya kona iliyotinga moja kwa moja na hivyo kuamsha shangwe na hari kwa mashabiki wao.

Mpaka timu hizo zinakwenda mapumziko KCMC walikuwa mbele kwa bao 1-0 ambapo kipindi cha pili kilianza kwa kasi kutokana na kila timu kufanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji wake na kuingiza nguvu mpya.

Walionekana kujipanga na kujiimarisha katika kipindi hicho timu ya TRA ilianzisha mashambulizi mfululizo lango mwa wapinzani wao huku wakicheza pasi fupi fupi na ndefu .

Kutokana na aina hiyo ya mchezo ambao walikuwa wakicheza iliwapelekea kuweza kupata bao la kusawadhisha kupitia kwa Datram Benzema ambaye alitumia uzembe wa mabeki kupachika wavuni bao hilo na hivyo kuamsha shangwe uwanja mzima.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo Katibu wa timu ya TRA Kamna Shomari alisema kwamba wanamshukuru mwenyezi Mungu kwa kuwawezesha kupata Sare na wana mechi nyengine.

Alisema kwamba hivyo wana matumaini watarekebisha mapungufu na kufanya vizuri Michezo ijayo na kwamba wamepania kuhakikisha wanapata matokeo mazuri kwenye mechi yao


TPDC YAZIGARAGAZA BENJAMINI MKAPA HOSPITALI, TPHPA MICHUANO YA SHIMUTA TANGA.

November 16, 2022

 

Kikosi cha timu ya  Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wanaume 

Kikosi cha timu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wanawake 

Na Oscar Assenga, TANGA

TIMU ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) ya kuvuta kamba kwa upande wa wanaume leo wameibuka kidedea kwenye mchezo wa kuvuta kamba baada ya kuwavuta timu ya Benjamini Mkapa Hospitali kwa seti 2-0.

Mchezo huo ambao ulikuwa wa aina yake ulifanyika kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Popatlaly Jijini Tanga ambapo wachezaji wa timu ya kuvuta kamba ya TPDC walionekana kuwa makini jambo ambalo liliwawezesha kuibuka na ushindi huo

Baada ya timu hiyo ya wanaume kumaliza kuvuta kamba iliingia upande wa wanawake ambapo timu ya Shirika hilo nayo iliweza kuibuka kidedea baada ya kuwavuta wanawake wenzao wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viwatilifu (TPHPA) kwa seti 2-0.

Timu ya TPDC ya kuvuta kamba iliwakilishwa vema na wachezaji wake mahiri ambapo kwa upande wa wanaume iliongozwa na Nahodha Joram Ndalahwa,Nnocent Mvamba,Adam Sajilo na Joseph Majebele.

Kwa upande wa timu ya wanawake iliwakilishwa vema na Rehema Saidi,Robi Chambiri,Catherine Madinda na nahodha wao Joyce Kiheka .

BENKI YA CRDB YAENDESHA SEMINA KWA WATEJA WAKE WA MKOA WA TANGA

November 15, 2022

 

 
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omary Mgumba akizungumza wakati akitoa hotuba yake katika ufunguzi rasmi wa Semina ya siku moja kwa Wateja wa Benki ya CRDB wa mkoa wa Tanga, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga, Novemba 14, 2022.  
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa Semina ya siku moja kwa Wateja wa Benki ya CRDB wa mkoa wa Tanga, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga, Novemba 14, 2022. 
Afisa Mkuu wa Biasra wa Benki ya CRDB, Boma Raballa akizungumza wakati akitoa mada ya biashara  na uwekezaji katika Semina ya siku moja kwa Wateja wa Benki ya CRDB wa mkoa wa Tanga, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga, Novemba 14, 2022. 
 Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini, Chiku Issa akizungumza katika Semina ya siku moja kwa Wateja wa Benki ya CRDB wa mkoa wa Tanga, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga, Novemba 14, 2022. 
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa akizungumza katika Semina ya siku moja kwa Wateja wa Benki ya CRDB wa mkoa wa Tanga, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga, Novemba 14, 2022.
 
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Hashim Mgandilwa akizungumza katika Semina ya siku moja kwa Wateja wa Benki ya CRDB wa mkoa wa Tanga, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga, Novemba 14, 2022.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omary Mgumba (kulia) asalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, wakati alipowasili kwa lengo la ufunguzi rasmi wa Semina kwa Wateja wa Benki ya CRDB wa mkoa wa Tanga, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga, Novemba 14, 2022. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa na wa pili kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Tanga, January Kirambata.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omary Mgumba (katikati) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakiwasalimia baadhi ya viongozi waandamizi wa Benki ya CRDB, wakati alipowasili kwa lengo la ufunguzi rasmi wa Semina kwa Wateja wa Benki ya CRDB wa mkoa wa Tanga, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga, Novemba 14, 2022.









Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omary Mgumba akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, muda mfupi baada ya ufunguzi rasmi wa Semina kwa Wateja wa Benki ya CRDB wa mkoa wa Tanga, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga, Novemba 14, 2022.