RUWASA WAKABIDHIWA CHETI CHA ITHIBATI ISO 9001:2015

September 12, 2026
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) imekabidhi cheti cha ubora wa huduma kwa wakala wa maji na usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) ikiwa ni Ishara ya utoaji huduma bora ya maji nchini.

Akikabidhi cheti hicho Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS Mhandisi Abadallha Killeo amesema kuwa utoaji wa cheti cha ubora ni hatua kwani cheti hicho kinatolewa baada ya ukaguzi, upimaji pamoja na kuhakikisha vigezo vya ubora vinafikiwa Mhandisi KIlep alitumia nafasi hiyo kutoa Wito kwa Mnejimenti ya RUWASA kutobweteka kwa hatua hiyo kwani upimaji na ukaguzi wa ubora ni suala endelevu.

Cheti hicho cha Ubora kimekabidhiwa mbele ya Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso katika siku ya ufungaji wa Kikao kazi cha siku tatu kwa watendaji na Menejimenti ya Ruwasa jijini Dodoma.

Waziri wa Maji Mhe.Aweso alitumia nafasi hiyo kuwapongeza RUWASA kwa kufanikiwa kupata cheti cha ithibati namba ISO 9001:2015. ‘’Kupata cheti ni jambo moja , uwajibikaji ni suala la Pili, naomba mhakikishe mnaendelea kusimamia ubora wa huduma kwa wananchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi alimhakikishia Mhe.Waziri kuwa RUWASA itaendelea kusimamia utoaji huduma bora kwa wananchi ambao ndio walengwa katika utendaji wa kila siku wa RUWASA.

Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA inahudumia Mikoa 25 nchini katika Wilaya 128 ambapo mpaka kufikia Desemba 2025 huduma ya upatikanaji wa maji Vijijini ilifikia asilimia 85.2 kutoka asilimia 64 iliyokuwepo wakati RUWASA inaanzishwa mwaka 2019.

Kwa mwaka wa fedha 20226/2027 Ruwasa imepanga kutumia shilingi Bilioni 188 ambapo kiasi cha shilingi Bilioni 41 imelenga kuanzisha miradi mipya katika vijiji 400 kote nchini.

Kikao hicho cha siku tatu kiliongozwa na kauli mbiu inayosema ‘’kutoka ujenzi wa Miradi hadi Utoaji Huduma ya Maji ya Uhakika kwa wananchi Vijijini

Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »