MAKATIBU WAKUU WAKUTANA KUPITIA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MUDA WA KATI WA PROGRAMU YA AFDP

September 15, 2026



Na; Mwandishi Wetu- Dar es Salaam

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na wenye Ulemavu Dkt. Jim Yonazi ameongoza Kikao cha Makatibu Wakuu kutoka katika  Wizara  zinazotekeleza Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP), Wakuu wa Taasisi pamoja na Wakurugenzi wa Sekta, pamoja na wataalam kutoka katika sekta hizo  na Ujumbe Kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) katika ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Mtaa wa Magogoni Jijini Dar es Salaam tarehe 15 Septemba 2026.

Kikao hicho kimefanyika baada ya ziara maalumu ya wataalamu kutoka IFAD na AFDP kukamilisha ziara ya kutembelea maeneo yanayotekeleza Programu ya kuendeleza Kilimo na Uvuvi ya kupima matokeo utekelezaji wa program ya muda wa kati (MTR)

Pamoja na mambo mengine IFAD wamepongeza Serikali kwa Kusimamia vyema Shughuli za Programu kwa kuleta matokeo chanya kwa wananchi..Aidha  kikao hicho kimepokea wasilisho la dondoo lnayoainisha hoja za makubaliano yaliyopendekezwa kuhusiana na mwenendo wa utekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP).



Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »