
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, akiongea na uongozi wa Tabora baada ya kuwasili mkoani humo Septemba 12, 2026 kwa ziara ya siku tatu.
………….
Septemba 13, 2026, Dkt Kikwete anaanza ziara ya kukagua utekelezaji wa Mradi wa Jamii Salama katika Wilaya ya Sikonge, mkoani Tabora.
Kabla ya kukagua zahanati mpya na nyumba mbili za watumishi, Dkt Kikwete atatembelea kliniki tembezi katika Kitongoji cha Ipembe, Kata ya Kiloli, Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, ili kujionea huduma zinazotolewa kwa wananchi wa maeneo ya pembezoni.

Mradi huo unatekelezwa na Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete (JMKF), kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais–TAMISEMI, Wizara ya Afya na mamlaka za Mkoa wa Tabora. Ushirikiano huo umefanikisha ujenzi wa zahanati mbili za kisasa na nyumba nne za watumishi katika wilaya za Sikonge na Uyui.
Dkt Kikwete, Muasisi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya JMKF, atakagua namna uwekezaji huo utakavyorahisisha upatikanaji wa huduma za afya kwa zaidi ya wakazi 36,000 wa vijiji hivyo na maeneo jirani.
.jpeg)
Kesho, Septemba 14, atatembelea kliniki tembezi, zahanati mpya na nyumba mbili za watumishi katika Kijiji cha Gengesita, Kata ya Kizengi, Wilaya ya Uyui.
Mradi umefadhiliwa na S. C. Johnson & Son, Inc. ya Marekani, inayounga mkono afya, ustawi wa familia na mapambano dhidi ya malaria duniani, hasa katika jamii zenye changamoto za kufikiwa kirahisi.

EmoticonEmoticon