MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake UWT Taifa Mary Chatanda akizungumza na waandishi wa habari mjini Tanga kuhusu kumpongeza Rais Dkt Samia Suluhu kwa kuimarisha Demokrasia nchini
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake UWT Taifa Mary Chatanda akizungumza na waandishi wa habari mjini Tanga ambao hawapo pichani kuhusu kumpongeza Rais Dkt Samia Suluhu kwa kuimarisha Demokrasia nchini
MWENYEKITI
wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake UWT Taifa Mary Chatanda akizungumza na
waandishi wa habari mjini Tanga kuhusu kumpongeza Rais Dkt Samia Suluhu
kwa kuimarisha Demokrasia nchini
Na Oscar Assenga,TANGA
MWENYEKITI
wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake UWT Taifa Mary Chatanda amesema UWT
imekoshwa na uamuzi wa kihistoria wa Rais Dkt Samia Suluhu kuondoa
zuio la mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa nchini maamuzi ambayo
yameleta faraja kwa vyama hivyo na hivyo kufungua ukurasa mpya wa demokrasia nchini
Chatanda
aliyasema hayo leo kwenye ofisi za CCM Mkoa wa Tanga wakati akizungumza
na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali kuhusu kuondoa zuio la
mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa nchini ambapo
Alisema
kwamba UWT imekoshwa na hatua ya kihistoria kuondoa zuio la mkutano ya
hadhara vyama vya siasa ikiwemo kukwamua mchakato wa kupata Katiba mpya
ambapo alisema kwamba wao wanaunga mkono uamuzi wa Kukwamua mchakato wa
marekebisho ya Katiba ya Tanzania na hivyo tunahimiza amani na
utulivu wakati wote wa kusubiri Serikali kukamilisha taratibu zote za
kuanza mchakato huu kama alivyoeleza Mhe Rais Samia Suluhu Hassan katika
hotuba yake jana tarehe 3 Januari 2023.
Alisema
pamoja na kufanya marekebisho ya sheria mbalimbali ili kupanua wigo wa
demokrasia nchini ambapo alisema maamuzi ya Rais Dkt Samia yameleta
faraja kwa vyama mbalimbali vya siasa nchini na kuwezesha kufikia hatu
kubwa ya kidemokrasia nchini.
Aidha
alisema Rais Dkt Samia ameendelea kuonyesha udhabiti wa kauli zake kwa
matendo ambapo hata alipohutubia Taifa mara baada ya kuapishwa Maci
19,2022 alisema wakati huo sio wa kutazama mbele kwa mashaka bali ni kwa
kutazama kwa matumaini mwisho wa kumnukuu.
Mwenyekiti
Chatanda alisema maamuzi aliyoyafikia Rais Dkt Samia kupitia mchakato
wa maridhiano kuanzia kuundwa Kikosi cha kazi pia mazungumzo kati ya
Vyama vya Siasa na Vyama vya CCM na Chadema yameleta matumaini mapya
katika kujenga demokrasia ya kuaminiana baina ya vyama vyote vya siasa
nchini ambayo ni chachu katika ujenzi wa Taifa lenye umoja Amani a
Utulivu.
“Lakini
niwaambie kwanza falsafaya Rais Samia Suluhu ni kujenga upya nchi yenye
umoja katika ujenzi wa Taifa inayoongozwa falsafa ya 4R maridhiano
ustahimilivu,mabadiliko na kujenga upya nchi hadi sasa falsafa hiyo
imefanikiwa kwa asilimia 100” Alisema Chatanda
Hata
hivyo alisema sio tu kwa kuleta mafanikio makubwa ya kisekta
aliyotekeleza Rais kwa muda mfupi wa chini ya miaka miwili madarakani
licha kuipokea nchini ikiwa na hali tete ya kutokana majanga ya Corona
,vita ya Ukraine na kufiwa na mtangulizi wake mwaka 2021
“Kwa
kweli sisi UWT tunasema Rais Dkt Samia amefanya jambo kubwa sana hivyo
tunampongeza na hizo zinazotokana na matokeo ya mkutano baina ya Rais
Samia na vyama vya siasa kwenye usajili wa kudumisha nchini,uwt
wanampjgeza Rais Samia kwa kufanya maamuzi yalitileta furaha isiyo na
kifani kwa wananchi wa Tanzania na wapenda Amani dunia kote kwa kutoa
majawabu ya vikwazo vya demokrasia nchini wao na majanga ya korona,vita
ya Ukraine na kufiwa na mtangulizi wake Mwaka 2021" Alisema Chatanda
Aliongeza
kwamba bali falsafsa hìzo zinahimiza siasa za kustaarabu zenye kuweka
watu pamoja,kujenga hoja za ushawishi kupitia majadiliano mazungumzo
kuhusisha vyama vya siasa katika kuendesha nchi hivyo kutokana na hilo
UWT wanampongeza Rais huku wakieleza kwamba hakika wanawake wanaweza.
Hata
hivyo alisema kwamba Jumuiya hiyo ya UWT inawahimiza viongozi wanawake
wa vyama mbalimbali kuandaa mikutano mingi ya hadhara ili kuweza kupokea
changamoto mbalimbali zinazowagusa wanawake wa Tanzania wanakabiliwa na
changamoto zinazofanana bila kujali itikadi zao na pia katika mikutano
wanapendeleza hatua mahususi za kuchukua kwa Serikali ili kumkomboa
mwanamke kiuchumi,kijamii na kisiasa.
Mwenyekiti
Chatanda alisema kwamba pia wamefurahishwa na uamuzi wa Serikali ya
awamu ya sita ya kuridhia mapendekezo ya kikosi kazi cha kufanya
marekebisho ya sheria kadhaa ndani ya nchi kwa nia ya kuimarisha
demokrasia zaidi ambayo yatahusisha wananchi.
Alisema
wanaamini marekebisho hayo pia yatazingatia masuala ya usawa wa
kijinsia katika kuongeza uwakilishi wa wanawake kwenye siasa na uongozi
kuanzia kwenye vyama vya siasa kama ambayo wameshuhudia namna Rais Samia
Suluhu alivyojitahidi kuongeza ushiriki wa wanawake kwenye uongozi
ndani ya Serikali yake na chama cha Mapinduzi
Mwenyekiti
Chatanda aliwahimiza viongozi wake wa Jumuiya ya UWT kuanzia ngazi za
Tawi ,Kata/Wadi ,Jimbo, wilaya , Mkoa mpaka Taifa pamoja na
Madiwani,wawakilishi na Wabunge Wanawake kufanya mikutano ya hadhara kwa
kufuata taratibu zote ,mikutano hiyo ilenge kuelezea utekelezaji wa
Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 , kusikiliza kero za
wananchi na kujibu hoja mbalimbali zitakazopotoshwa kwa lugha ya
kistaarabu na kwa kutumia takwimu sahihi , sisi Viongozi wa UWT Taifa
tutaonyesha mfano kwa kutumia fursa hii iliyotolewa na Mhe Dk Samia
Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .
Hata
hivyo pia alitumia nafasi hiyo kuitaka Jumuiya ya UWT kuendelea
kuwaomba Watanzania kuendelea kumuamini Mheshimiwa Rais Dkt. Samia
Suluhu Hassan na kumuunga mkono kwani ana dhamira njema ya kujenga Taifa
linaloongea lugha moja , na ambalo kila mmoja anashiriki katika ujenzi
wa Taifa lake .
MWISHO
EmoticonEmoticon