Baaadhi ya watu mbalimbali wakitembelea banda la Tanzania, nchini Saudi Arabia, katika maonyesho ya utalii ya '(Travel and Tourism Pioneers Forum - 2017).
Maonyesho ya utalii nchini Saudi Arabia yaipaisha Tanzania
Na Mwandishi Maalum, Saudi Arabia
Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia mwishoni mwa juma hili ulishiriki katika maonyesho ya Safari na Utalii yajulikanayo kama '(Travel and Tourism Pioneers Forum - 2017).
Maonyesho ya TPF 2017 ambayo hufanyika kila mwaka kwa uandalizi Al Awsat Expo chini ya uhisani wa Mwana Mfalme HRH Prince Dr. Seif al Islam bin Saud bin Abdulaziz, yamefanyika kwa mafanikio huku ubalozi wa Tanzania ukifanikiwa kwa kiasi kikubwa kutangaza utalii wa Tanzania.
Akizungumza katika maonyesho hayo, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza, alisema kwamba maonesho hayo yalikuwa maalumu kwa wafanya maamuzi na viongozi wa asasi za utalii (decision makers and leaders and tourisma leaders) nchini Saudi Arabia.
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza, mwenye suti nyeusi akizungumza jambo na wageni waliotembelea katika banda la Tanzania kwenye maonyesho hayo.
Alisema kwamba kuwa banda la Tanzania lilifanikiwa kuonesha vivutio vya utalii vya Tanzania ikiwemo mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama, hifadhi za taifa, maeneo ya kihistoria ya Zanzibar, kilwa na Bagamoyo.
Mazungumzo yakiendelea yakiongozwa na Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia
Watu wakipata maneno juu ya utalii wa Tanzania nchini Saudi Arabia
Karibuni Tanzania.
“Tunashukuru kwa kiasi kikubwa kushiriki katika maonyesho haya sambamba na Tanzania kutangaza vivutio vya utalii wan chi yetu, tukiamini kuwa ni fursa adhimu kwa nchi yetu.
“Tunaendelea na juhudi za kutangaza nchi yetu ya Tanzania sambamba na kuwaonyesha watu wa Saudi Arabia juu ya umuhimu wa kutembelea nchini kwetu ili kujionea fursa mbalimbali za kiuchumi na utalii,” Alisema.
Kwa mujibu wa Balozi Mgaza, miadi na majadiliano kuhusu kukuza utalii (promotion of tourism) yalifanyika baina ya washiriki wa Tanzania na mawakala wa utalii (tour operators) na wa usafiri (travel agents).
EmoticonEmoticon