MHE. BALOZI OMAR AZUNGUMZA NA UONGOZI WA TWIGA CEMENT

January 20, 2026

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akizungumza jambo wakati wa kikao chake na uongozi wa Kampuni ya Saruji ya Twiga, ambacho kilijadili masuala mbalimbali yanayohusu uendelezaji wa uwekezaji wa Kiwanda cha Saruji cha Twiga, kilichofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine aliuhakikishia uongozi huo kuwa Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini ili kuimarisha sekta ya viwanda.



Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akiongoza kikao kikao chake na uongozi wa Kampuni ya Saruji ya Twiga kikihudhuriwa pia na viongozi wengine wa Wizara ya Fedha na Mamlaka ya Mapato, ambacho kilijadili masuala mbalimbali yanayohusu uendelezaji wa uwekezaji wa Kiwanda cha Saruji cha Twiga, kilichofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine aliuhakikishia uongozi huo kuwa Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini ili kuimarisha sekta ya viwanda.

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Twiga Cement, Bw. Alfonso Velez, akizungumza jambo wakati wa kikao chake na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (hayupo pichani), ambapo walijadiliana masuala mbalimbali yanayohusu uendelezaji wa uwekezaji wa Kiwanda cha Saruji cha Twiga, kilichofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (katikati), Meneja Mkuu Kampuni ya Twiga cement Bw. Alfonso Velez (wa nne kulia), Kaimu Kamishna wa Idara ya Uchambuzi wa Sera, Dkt. Remidius Ruhinduka (kulia), Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uchambuzi wa Sera, Bw. William Mhoja (kushoto), Kamishna Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mcha Hassan Mcha (wa tatu kulia), Kamishna Msaidizi Idara ya Sheria-TRA, Bw. Gabriel Kimweri (wa pili kulia), Mjumbe wa Bodi wa Twiga cement, Bw. Raymond Mbilinyi (wa nne kushoto) na Mkurugenzi wa Fedha wa Twiga Cement, Bw. Simon Renauld (wa pili kushoto) na Meneja Biashara Mwandamizi wa Kampuni hiyo, Mhandisi Danford Semwenda (wa tatu kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kikao chao kilichojadiliana masuala mbalimbali yanayohusu uendelezaji wa uwekezaji wa kiwanda cha Saruji cha Twiga, kilichofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)

Na. Saidina Msangi na Joseph Mahumi, WF, Dodoma

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Twiga Cement ukiongozwa na Meneja Mkuu wake, Bw. Alfonso Velez, Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma, ambapo pande hizo zimejadili masuala mbalimbali yanayohusu uendelezaji wa uwekezaji wa Kiwanda cha Saruji cha Twiga.

Mhe. Balozi Omar, aliuhakikishia uongozi huo kuwa Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini ili kuimarisha sekta ya viwanda.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo Bw. Alfonso Velez, alisema kuwa lengo la kampuni ni kuendelea kukuza uwekezaji nchini ili kukidhi mahitaji ya soko pamoja na kutoa ajira kwa wananchi.

Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Kaimu Kamishna wa Idara ya Uchambuzi wa Sera Dkt. Remidius Ruhinduka, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uchambuzi wa Sera, Bw. William Mhoja, Kamishna Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mcha Hassan Mcha, Kamishna Msaidizi Idara ya Sheria -TRA, Bw. Gabriel Kimweri, Mjumbe wa Bodi wa Twiga cement, Bw. Raymond Mbilinyi na Mkurugenzi wa Fedha wa Twiga Cement, Bw. Simon Renauld, Meneja Biashara Mwandamizi wa Kampuni hiyo, Mhandisi Danford Semwenda na maafisa waandamizi Wizara ya Fedha.

MWISHO

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »