USISHANGAE MATAA MJINI,TEMBEA UONE MCHANGA UNAOHAMA ( SHIFTING SANDS) NGORONGORO

January 15, 2026




Waswahili husema tembea uone na Mwenda bure si mkaa bure huenda ataokota.


Ukitaka kujaribu kuuokota mchanga unaohama njoo jirani na bonde la Olduvai ndani ya hifadhi ya Ngorongoro ushangae.


Jirani na bonde hili la Olduvai kuna mchanga unaohama  ambao huwavutia mealfu ya watalii kuja kujionea maajabu hayo.


Mchanga huu upo katika umbo la nusu mwezi na upo  karibu na Bonde la Olduvai ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro. 

Mchanga huu wenye rangi nyeusi umetokana na madini ya chuma na majivu yaliyotokana na mlipuko wa Volcano kutoka Mlima Oldoinyo Lengai.


Mchanga huu ambao husogea kwa kasi ya takribani mita 15–29 kwa mwaka tuta lake lina urefu wa mita 5 na upana wa mita 100.


Hayo ndiyo maajabu ya Hifadhi ya Ngorongoro ukitaka kujua zaidi kuhusu mchanga huu tembea uone kwani fahari ya macho ni kuona  na fahari ya macho haifilisi duka.


 _Tumerithishwa, Tuwarithishe_

Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »