
Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Laurent Luswetula (Mb) akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), katika siku ya ufunguzi rasmi wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha ikiwa ni maadhimisho ya tano, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi” yanayoendelea katika Viwanja vya Usagara, Jijini Tanga, ambayo yamezikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hitadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka mkoa wa Tanga na mikoa ya karibu.

Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Laurent Luswetula (Mb) akipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Dadi Kolimba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa alipowasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa jijini Tanga kabla ya ufunguzi rasmi wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha ikiwa ni maadhimisho ya tano, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi” yanayoendelea katika Viwanja vya Usagara, Jijini Tanga, ambayo yamezikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hitadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka mkoa wa Tanga na mikoa ya karibu.

Baadhi ya picha za Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Laurent Luswetula (Mb) pamoja na Timu ya Uratibu ya Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha kutoka Wizara ya Fedha wakijadili katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Jiji la Tanga kabla ya ufunguzi rasmi wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha ikiwa ni maadhimisho ya tano, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi” yanayoendelea katika Viwanja vya Usagara, Jijini Tanga, ambayo yamezikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hitadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka mkoa wa Tanga na mikoa ya karibu.


Baadhi ya picha za Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Laurent Luswetula (Mb) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Dadi katika Viwanja vya Usagara, Jijini Tanga, ikiwa ni siku ya ufunguzi rasmi wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha ikiwa ni maadhimisho ya tano, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi” yanayoendelea katika Viwanja vya Usagara, Jijini Tanga, ambayo yamezikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hitadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka mkoa wa Tanga na mikoa ya karibu.

Baadhi ya wananchi na wadau mbalimbali wa sekta ya fedha wakifuatilia kwa makini siku ya ufunguzi rasmi wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha ikiwa ni maadhimisho ya tano, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi” yanayoendelea katika Viwanja vya Usagara, Jijini Tanga, ambayo yamezikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hitadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka mkoa wa Tanga na mikoa ya karibu.

Baadhi ya picha Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Laurent Luswetula (Mb) (Katikati), Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Dadi Kolimba (wa pili kushoto), Kaimu Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Dionisia Mjema (wa pili kulia) pamoja na viongozi kutoka Wizara ya Fedha na Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hitadhi ya Jamii ikiwa ni siku ya ufunguzi rasmi wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha ikiwa ni maadhimisho ya tano, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi” yanayoendelea katika Viwanja vya Usagara, Jijini Tanga,
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Tanga)
…………….
Na. Chedaiwe Msuya na Eva Ngowi, WF, Tanga
Katika dunia inayobadilika kwa kasi ya kiuchumi na kiteknolojia, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kuimarisha sekta ya fedha na kusogeza huduma za kifedha karibu zaidi na wananchi ili kuchochea ustawi wa jamii na maendeleo ya Taifa. Hatua hiyo imejitokeza Januari 21, 2026 wakati wa ufunguzi rasmi wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yaliyofanyika katika Viwanja vya Usagara, Jijini Tanga.
Akizungumza katika ufunguzi wa maadhimisho hayo kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula (Mb), alisema Serikali imeweka mazingira wezeshi kupitia sera, sheria na mipango mbalimbali ikiwemo Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha, Programu ya Elimu ya Fedha kwa Umma na Mpango wa Huduma Jumuishi za Fedha, hatua zilizochangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa sekta ya fedha nchini.
Alisema hadi Septemba 2025, Tanzania ilikuwa na benki za biashara 35, benki za maendeleo mbili, benki za huduma ndogo za fedha tatu pamoja na taasisi zaidi ya 2,800 za huduma ndogo za fedha, huku mawakala wa benki wakifikia zaidi ya 145,000. Aidha, rasilimali za benki zimefikia shilingi trilioni 71.8, amana trilioni 50.2 na mikopo kwa sekta binafsi trilioni 42, hali inayoonesha kuimarika kwa uchumi na uwekezaji.
Mhe. Luswetula pia alibainisha kuwa sekta ya bima na masoko ya mitaji imeendelea kukua, huku Tanzania ikiondolewa katika orodha ya nchi hatarishi kifedha ya Umoja wa Ulaya na kwenye orodha ya uangalizi ya FATF, hatua itakayorahisisha miamala ya kifedha na kuvutia uwekezaji zaidi kuanzia Januari 29, 2026.
Akiongea kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Kaimu Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha Bi. Dionisia Mjema alisema Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa ni fursa muhimu ya kuwajengea wananchi uelewa wa masuala ya fedha, kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha na kukuza uchumi wa Taifa.
Alieleza kuwa maadhimisho hayo ni utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha (2020/21–2029/30) na Programu ya Kutoa Elimu kwa Umma, inayolenga kutoa maarifa kwa wananchi juu ya usimamizi wa fedha binafsi, uwekaji akiba, mikopo, uwekezaji, bima, kodi na masuala mengine muhimu ya kifedha.
Bi. Mjema alisema kuwa malengo makuu ni kuongeza uelewa wa wananchi, kusaidia wajasiriamali wadogo na wa kati, kuimarisha utamaduni wa kuweka akiba na kulipa madeni kwa wakati, na kuongeza mchango wa sekta ya fedha katika ukuaji wa Uchumi na kusisitiza kuwa elimu itakayotolewa ni bure kwa wananchi wote.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Dadi Kolimba, akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mhe Balozi, Dkt Batilda Burian, alisema Mkoa wa Tanga umepokea zaidi ya shilingi trilioni 3.1 kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika awamu ya kwanza ya Rais Samia, kwa ajili ya maboresho ya Bandari ya Tanga yaliyoongeza shehena, mapato na ajira.
Aidha, pato la mkoa limeongezeka hadi shilingi trilioni 9.5 mwaka 2024 na kuufanya mkoa wa Tanga kushika nafasi ya sita kitaifa katika vita dhidi ya umaskini.
Mhe. Kolimba alieleza kuwa sekta ya fedha ni nguzo muhimu ya uchumi wa mkoa huo, akibainisha kuwa Tanga ina benki kubwa 10 na taasisi 355 za huduma ndogo za fedha, huku mikopo ya zaidi ya shilingi bilioni 6.8 ikitolewa kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Alitaja uelewa mdogo wa masuala ya fedha kwa baadhi ya wananchi kuwa changamoto, akieleza matumaini kuwa maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yataongeza elimu na matumizi sahihi ya huduma za kifedha.
EmoticonEmoticon