Chama Cha Maafisa Mawasiliqno wa Serikali Tanzania (TAGCO) kimeendelea kutoa mafunzo mbalimbali ikiwemo matumizi ya teknolojia ya Akili unde (Artificial Intelligence – AI) kwa Maafisa Mawasiliano wa serikali kwa lengo la kuhakikisha wanafanya kazi kuendana na mabadiliko ya teknolojia.
Mafunzo hayo yanayoendeleq kufanyika Mkoa wa Morogoro yamejikita kuongeza ubunifu katika kazi na kuzifanya kuwa bora zaidi umaoendana na wakati.
Akizungumza katika mafunzo hayo, Mshauri Mwelekezi wa Mawasiliano ya Kimkakati Bi. Annastazia Rugaba, ameipongeza TAGCO kwa kuandaa mafunzo hayo, akisema kuwa ni hatua muhimu itakayowawezesha kuongeza weledi na ubunifu katika kazi zao za kiutendaji.
“Napenda nipongeze Chama Cha Maafisa Habari wa Serikali Tanzania (TAGCO) kwa kufanya mafunzo haya, ambayo naamini yataleta mabadiliko makubwa katika tasnia ya Mawasiliano kwa Umma. Kwanza, katika upande wa teknolojia nategemea tutapata mabadiliko chanya, kwa sababu fani hii ya Mawasiliano kwa Umma inategemea sana teknolojia. Hivyo ni lazima wajifunze ili waendane na mabadiliko ya teknolojia na kuweza kuweka utamaduni wa taasisi wa kujenga mawasiliano mazuri ndani na nje ya taasisi,” amesema Annastazia Rugaba
Kwa upande wake, Afisa Mawasiliano Mwandamizi kutoka Kampuni ya Uendelezaji Joto Ardhi Tanzania (TGDC) na mwanachama wa TAGCO, Boaz Mazigo, amesema amefurahishwa kuwa sehemu ya mafunzo hayo yanayowawezesha kutumia teknolojia ya akili mnemba katika kazi zao za kiofisi, akisema ni teknolojia inayosaidia kurahisisha na kuharakisha utendaji kazi.
“Ninayo furaha kubwa ya kuwa katika kikao hiki cha namna ya kutumia teknolojia ya akili mnemba, kwa sababu ni kitu ambacho kimekuja kutuletea mwanga mkubwa wa namna ambavyo kazi zetu zinapaswa kufanyika kwa ufanisi. Niwaombe viongozi wa taasisi nyingine waendelee kuwashika mkono Maafisa Habari ndani ya taasisi zao ili mafunzo kama haya yanapotangazwa nao waweze kushiriki,” Boaz Mazigo amesema
Naye Mkuu wa Kitengo cha Habari, kutoka Wizara ya Habari na Mawasiliano Zanzibar, Takdir Suweid, ametoa wito kwa waajiri katika sekta ya umma na binafsi kuwaruhusu wafanyakazi wao kushiriki mafunzo hayo ili kupata mabadiliko ya kiutendaji yatakayosaidia kuboresha utendaji wa kazi zao.




EmoticonEmoticon