MBUNGE MAKBEL ASISITIZA AMANI HUKU AKIWATAKA WANANCHI KUTOVIPA NAFASI VIASHIRIA VYA UVUNJIFU WAKE

November 24, 2025




Na Oscar Assenga, TANGA

MBUNGE wa Jimbo la Tanga(CCM) Kassim Amar Mbarak (Makbel)  amewataka wananchi wa mkoa huo kuhakikisha hawavipi nafasi viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani kutokana na kwamba wanahitaji amani kwa ajili ya maendeleo ya mkoa na nchi kwa ujumla.

Makubeli aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa halfa ya tathimini ya Programu ya kuchangia Ujenzi wa Hospitali itakayofuata maadili ya Kiislamu inayosimamiwa na Taasisi ya Islamic Development Foundation (TIDF)iliyofanyika eneo la Duga Jijini Tanga.


Alisema mpango wa ujenzi wa Hospitali itakayokuwa ikitoa huduma kwa kufuata maadili ya Kiislamu kwa wagonjwa ambao wanakwenda kupata huduma mbalimbali ni nzuri na hivyo watahakikisha wanawaunga mkono ili waweze kutimiza ndoto yao aliyoanzisha.


Aidha alisema kwamba amani ni jambo muhimu huku akisisitiza watanzania kuendelea kuliombea Taifa na watu wa Tanga wawe wa kwanza kuhakikisha amani ya nchi inaendelea kuwepo kutokana na kwamba ndio nguzo muhimu ya maendeleo.


“Tusivikubali viashiri vyovyote vya uvunjifu wa amani tunahitaji amani kwa ajili ya maendeleo ya mkoa na nchi kwa ujumla lakini viongozi wa dini tuendelee kuhamasisha suala la amani “Alisema


Alisema kwamba licha ya kuwepo kwa ujenzi huo lakini watakuwa wamebuni kitu cha kipekee kwenye soko na jamii kutokana na kufuata misingi na maadili ya kiislamu na ikibainika kwamba ukienda hospitali mwanaume unapata matibabu na daktari mwanaume italeta ushindani wa kibiashara.


Aidha alisema kwamba Hospitali itakayojengwa itapelekea athari chanya kwa jamii kutokana na kwamba nyengine zinakazojengwa itabidi zifuata misingi ya huduma za kijamii wanazozitoa itabidi wabadilike kutokana na kwamba bila kufanya hivyo watashindwa kuendana nao.



Alisema hivyo itabidi wabadilike na wakishindwa kufanya hivyo watakosa soko na biashara kupotea huku akieleza kwamba utafiti unaonyesha kwamba binadamu anafurahisihwa zaidi na maadili kuliko huduma.


“Unaweza kuwa na miundombinu mizuri lakini watendaji wana lugha chafu na maadili mabovu ukashindwa kupata watu wanaokuja kupata huduma katika eneo lako hivyo ikisimama hospitali moja na Hospitali zote za Tanga mjini zitabadilika kuendana na mazingira”Alisema


Hata hivyo alisema kwamba mfano huo unaendana na na mifumo ya fedha kwa kiislamu ilianza ikiwa migeni sana na iliaanza kupitia benki moja Tanzania ikatengeneza huduma kwa mfumo wa dini watu wakaa na wakawa na sheria ya fedha kwa mifumo ya kiislamu na huduma ipo na huduma za kibenki zinaendelea .


Alisema waitazame Tanga Islamic Hospitali kuchochoea cha kwenda kubadilisha maadili katika utoaji wa huduma kwenye sekta ya Afya Tanga na Tanzania kwa ujumla kwa maana hilo linawezekana na watu watavutiwa na hivyo na kupelekea watu wote kuiga mfano wa kutoa huduma kwa mifumo hiyo.



“Sio tunaenda kujenga tu kuna ujumbe tunakwenda kupelekea kwenye jamii ukiacha hilo mradi huu sio mdogo ni mkubwa alikuja Mufti Dkt Abubakari Zuberi akazindua kongamano kubwa Tanga hawana namna inabidi waunmge mkono juhudi za mufti ni kuhakikisha baada ya shule kuhakikisha kila mkoa uwe na hospitali au kituo cha Afya kikubwa hizo ni ndooto zake kuhakikisha jamii ya waislamu wanamiliki miradi mbalimbali ikiwemo ya Afya”Alisema


Akizungumza wakati akieleza tathimi ya mradi wa ujenzi wa Hospitali hiyo,Mratibu wa Taasisi ya Tanga Islamic Development Foundation (TIDF) Hamad Kidege alisema kwamba taasisi hiyo ilianzishwa rasmi Agosti 9 mwaka 2009 ikiwa ni mjumuiko wa misikiti ya Tanga Jijini ipatayo 16 ambao walikutana katika kikao na kuanza na wazo na ndoto jambo ambalo leo lipo kwenye utekelezaji wake.


Alisema kwamba katika mradi huo taasisi hiyo imekuwa ikisimamia mpango wa ujenzi wa Hospitali itakayofuata maadili ya Kiislamu kupitia mipango mbalimbali ikiwemo kapu la ijumaa,Muslim Swadakatul Jaariya Fund,Bahasha na Msikiti huku akieleza kapu la Ijumaa kwa mwaka 2025 kwa muda wa miezi 10 wamepokea sadaka ya Milioni 17,008,361.


Aidha alisema kwamba katika mchango kupitia Masjid Al-Ihsaan kwa kipindi cha miezi 10 wamepokea kiasi cha Milioni 2,706,079 huku kupitia Masjid Mujahidina wamepokea sadaka ya miezi mitatu 103,500.

















Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »