KIKUNDI CHA AMANI NCHINI WAFANYA MKUTANO MAALUMU ULIOLENGA KUHAMASISHA UZALENDO NA KUELEZEA MAFANIKIO YA SERIKALI

March 01, 2026



Na Oscar Assenga,Tanga

KIKUNDI cha Amani nchini kimefanya mkutano maalumu leo katika Jiji la Tanga  uliolenga kuhamasisha uzalendo, kuelezea mafanikio ya Serikali na kupongeza utekelezaji wa ahadi za siku 100 za Rais tangu alipochaguliwa 2025.

Akizungumza wakati wa mkutano huo Maalumu Mwenyekiti wa Kikundi hicho nchini Hassan Kubebelwa alitoa wito kwa watanzania hususani vijana wametakiwa kuwa wazalendo kwa nchi na kuacha kukubali kushawishiwa na watu wanaoshinda kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii kueleza mabaya pekee na kuficha mazuri mengi yanayofanywa na Serikali

Katika kulitilia mkazo jambo hilo aliiomba Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Jeshi la Polisi, kuongeza kasi ya kuwafuatilia na kuwachukulia hatua kali watu wanaojiita wanaharakati wa mitandaoni wanaotumia majukwaa hayo kupotosha ukweli na kuichafua Serikali

"Lengo la kuja Tanga ni kuwahamasisha wanakikundi wenzetu wasimame kidete kuelezea maendeleo ya miundombinu mkoani hapa na nchi nzima. Tuache kusikiliza upotoshaji wa mitandaoni; Serikali imaleta fedha za mikopo ya asilimia 10 kwenye halmashauri, watu wakope na kujiendeleza badala ya kulalamika," alisisitiza Kubebelwa.

Awali akisoma riskala ya kikundi hicho, Mjumbe wa Kikundi hicho, Rehema Manyama alieleza katika kipindi cha siku 100, Rais ameonyesha dira kwa kufanikisha utoaji wa Bima ya Afya kwa wote, kuzalisha ajira kwa vijana ikiwemo kutoa mikopo.

Aidha alitoa ushauri wake kwa ngazi za mikoa ziendelee kutoa elimu ya uzalendo na kuimarisha elimu ya amali ili vijana wajiajiri na kuingiza kipato

 

Naye Mjumbe Zuberi Gogo, alibainisha kuwa ingawa hitilafu ndogo ndogo haziwezi kukosekana, changamoto kubwa inatokana na baadhi ya watendaji wanaopindisha taratibu na kuigombanisha Serikali na wananchi. Alitoa wito kwa wananchi kuelewa taratibu za kiserikali ili wasipotezwe na upotoshaji.

Akizungumzia suala la mikopo, Mjumbe Zainabu Salim Ugata, alifafanua kuwa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri haina upendeleo, bali inatolewa kwa vikundi vilivyofuata taratibu zote zilizowekwa. Alisema kikundi hicho kitaendelea kuzunguka mikoa yote nchini kutoa elimu kwa umma ili kuongeza uelewa wa mambo ya Serikali.





Washiriki wa mkutano huo waliazimia kuwa ni wajibu wa kila mzalendo kuilinda taswira ya nchi na kuhakikisha kuwa fursa za kiuchumi zinazotolewa na Rais zinawafikia walengwa bila vikwazo.



Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »