Na Mwandishi Wetu, Tanga
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Muheza mkoani Tanga kimesema hakihusiki na vitendo vinavyodaiwa kufanywa na aliyekuwa Katibu wa chama hicho wilayani humo, Joseph Mwakidasi, huku kikiwataka wanachama kuendelea kudumisha mshikamano na kuepuka makundi yanayoweza kukigawa chama.
Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Katibu wa CHADEMA Jimbo la Muheza, Michael Mhina, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matukio yaliyojitokeza ndani ya chama katika siku za hivi karibuni.
Mhina alisema Julai 8 mwaka huu viongozi wa chama waliona kupitia vyombo vya habari taarifa za Mwakidasi akimtuhumu Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, John Heche, kutumia vibaya fedha zinazochangwa na wanachama kupitia kampeni ya "Tone Tone".
Alisema kutokana na uzito wa tuhuma hizo, Kamati Tendaji ya Wilaya ilikutana kwa dharura Julai 9 na kumuita Mwakidasi ili afafanue chanzo cha madai yake, lakini hakufika wala wanachama wa CHADEMA. Alisema waliingia ofisini baada ya kuchukua funguo kutoka kwa m hayo, Julai 21 tuliamua kutoa taarifa kwa vyombo vya dola ili vifanye uchunguzi kuhusu kilichotokea. Sisi kama CHADEMA Muheza hatuhusiki kwenye kikao hicho wala kutoa maelezo.
Mhina alidai kuwa Julai 20, Mwakidasi aliwasili katika ofisi za CHADEMA Wilaya ya Muheza akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi kutoka wilaya nyingine pamoja na watu ambao, kwa mujibu wa chama hicho, si viongozi wala wanachama wa CHADEMA. Alisema waliingia ofisini baada ya kuchukua funguo kutoka kwa mweka hazina wa chama.
Kwa mujibu wa Mhina, watu hao walifanya kikao ndani ya ofisi hizo na baadaye kurekodi na kusambaza taarifa mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii, jambo alilodai lilisababisha taharuki miongoni mwa wanachama na wananchi wa Muheza.

"Baada ya matukio hayo, Julai 21 tuliamua kutoa taarifa kwa vyombo vya dola ili vifanye uchunguzi kuhusu kilichotokea. Sisi kama CHADEMA Muheza hatuhusiki na yaliyofanywa na watu hao," alisema Mhina.
Alisema viongozi wa chama wilayani humo wanaendelea kumuunga mkono Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, John Heche, pamoja na Mwenyekiti wa chama, Tundu Lissu.
Pia aliomba vyombo vya dola kuchunguza madai ya kuwahamasisha wananchi kuhudhuria mkutano kwa ahadi ya kulipwa fedha, akisisitiza kuwa CHADEMA haina utaratibu wa kuwalipa wanachama kushirikiio yote yaliyotokea katika ofisi za chama, akidai hatua zilizochukuliwa na Mwakidasi na wenzake zilichangia taharuki miongoni mwa wanachama na wananchi wa shughuli za chama.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Muheza, Ally Mahanyu, alisema chama kinapinga vitendo vinavyodaiwa kufanywa na Mwakidasi kwa madai kuwa vilikiuka taratibu za chama.
Mahanyu alisema viongozi walimuita Mwakidasi mara kadhaa kwenye vikao vya Kamati Tendaji ili kutoa maelezo, lakini hakuitikia wito huo.
Aidha, alivitaka vyombo vya dola kuchunguza matukio yote yaliyotokea katika ofisi za chama, akidai hatua zilizochukuliwa na Mwakidasi na wenzake zilichangia taharuki miongoni mwa wanachama na wananchi wa Muheza.
Aliwataka wanachama wa CHADEMA kuendelea kuwa watulivu, kuwaamini viongozi wao na kushiriki shughuli za ujenzi wa chama kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la CHADEMA Wilaya ya Muheza, Isa Mwaikani, alisema baraza hilo pia lilimuita Mwakidasi kutoa maelezo kuhusu tuhuma alizozielekeza kwa Heche, lakini hakuitikia wito huo.
Mwaikani alisema viongozi wa chama walishangazwa na tuhuma hizo kwa kuwa, kwa mujibu wa muundo wa uongozi wa chama, Makamu Mwenyekiti hahusiki na usimamizi wa fedha.
"Hatuelewi amepata wapi ujasiri wa kumtuhumu kiongozi wa juu wa chama bila kuwasilisha ushahidi kwenye vikao halali vya chama," alisema.
Aliongeza kuwa wanachama wengi wa CHADEMA Muheza wameendelea kubaki ndani ya chama na hali ya kisiasa wilayani humo ni tulivu.

Akijibu tuhuma hizo, aliyekuwa Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Muheza, Joseph Mwakidasi, alisema madai yanayotolewa dhidi yake hayana ukweli na kwamba anaendelea kutetea nafasi yake ndani ya chama.
Alisema hana mpango wa kuhamia chama kingine cha siasa na anasubiri maamuzi ya vikao vya chama kuhusu nafasi yake.
Kuhusu tuhuma alizomwelekeza John Heche, Mwakidasi alisema suala hilo linatokana na mijadala iliyofanyika katika kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA kilichofanyika Dodoma, akidai baadhi ya taarifa zilizokuwa siri zilivuja kutoka ndani ya chama.
Mwisho.

EmoticonEmoticon