MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Ayubu Sebabili amesisitiza umuhimu wa ukusanyaji wa mapato huku akiwataka madiwani wa Halmashauri hiyo kuwasaidia katika eneo hilo kutokana na kwamba hayakusanywi mbinguni wala hewani bali ni katika maeneo yao yanayoishi.
Sebabili aliyasema hayo leo wakati akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri hilo ambalo awali lilitanguliwa na Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri na Makamu wake ikiwemo kamati mbalimbali.
Alisema katika suala la ukusanyaji wa mapato wanahitaji kutoa ushirikiano kwa sababu maendeleo ya wilaya yataendana pia na kazi ya ukusanyaji wa mapato kama watakasanya kidogo hata asilimia 10 ya vijana,wanawake na walemavu watapata kidogo.
Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba iwapo wakiendelea kupata kidogo fedha inayotoka haitatosheleza hivyo wanahitaji kufanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha mapato yanaongezeka.
“Kwenye hili la mapato tunahitaji uadilifu wa nyie madiwani mnaweza kutufikisha pazuri lakini kama mtashirikiana na watu ambao wamepewa dhamana ya kukusanya mapato halafu wakawa sio waadilifu maanake mnakwenda kuiharibu Halmashauri”alisema DC huyo
“Lakii kwenye mapato lazima tuwe na ubunifu pamoja na uwepo wa watalaamu lakini nyie ndio mnafanya maamuzi hivyo tunahitaji kuibua vyanzo vipya vya mapato ambavyo ni sahhi kwa mujibu wa sheria havina maudhi kwa wananchi na ubunifu wetu ni wa muhimu sana”Alisema
Akizungumza matumizi ya tekonolojia katika ukusanyaji mapato ,aliwataka madiwani waende wakasimamie suala hilo kama ni posi kufanya kazi zifanye inavyostahili kama ni control number zitolwe inavyostahili wote pamoja wewe kitu kimoja kuhakikisha jambo letu linakwenda vizuri tofauti na hapo wanakwenda kuiharibu halmashauri.
Akizungumzia suala utatuzi wa migogoro katika maeneo yao aliwaambie kwamba iwapo watashiriki vizuri katika utatuzi wa migogoro wana uhakika kwa asilimia kubwa wananchi wataweza kuwaelewa kwa sababu haiwezekani mgogoro una miaka karibu 20 kijiji wanamsubiri mkuu wa wilaya kwenda kuupatia ufumbuzi.
“Hivyo lazima migogoro yote mnaipatia ufumbuzi kwa ushirikiano ngazi za chini fanyeni mikutano ya hadhara ya utatuzi kule kwenye kamati za maendeleo hakikishe kunakuwa agenda ya utatuzi wa migogoro muijue ambayo ni kero tukiweza kutatua migogoro chini hata suala la usalama linakuwa ni zuri”Alisema
Alieleza kwamba migogoro mingi ni ya ardhi hivyo wanaomba utaratibu wa kisheria utumike kutatua migogoro hiyo kwa kuyaelewa matatizo yaliyopo na hatua ambazo wamezichukua kuleta suluhu.
Hata hivyo aliwataka kujiepusha na vitendo vya rushwa kwa sababu Serikali haitomtetea kiongozi wa umma ambaye anahusika kwenye vitendo hivyo.
Hata hivyo akielezea usimamizi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo alisema katika eneo hilo kwa uzoefu wanafeli sana kutokana na baadhi yao kujihusisha na miradi ukishaamua kuwa mtumishi wa umma ndani ya halmashauri nidhamu ni kitu muhimu .
Awali akiungmza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza Dkt Jumaa Mhina alimpongeza Rais Dkt Samia Suluhu kwa ushindi mkubwa alioupata kwenye uchaguzi mkuu wa 2025 wanaendelea kumuunga mkono na kupokea maelekezo mbalimbali katika utekelezaji wa shughuli za kuwaletea maendeleo watanzania.
Naye kwa upande Mwenyekiti wa Halmashauri ya Muheza Salim Sechambo alisema kwamba moja ya vipaumbele vyake ni kuhakikisha wanasimamia kikamilifu suala la mapato katika halmashauri hiyo .
Alisema kwamba wana vyanzo vingi vya mapato kikubwa ni kushirikiana kwa kina na kuinyesha utulivu na kusimamia vyanzo vilivyopo na kubuni vyengine kwa maslahi mapana ya Muheza.
Aliongeza pia wanakwenda kusimamia vema miradi na ambayo wanaanza nayo ni kusimamia kwa nguvu zao zote na kuhakikisha kila fedha inayoingia kwenye Halmshauri hiyo ili dhamira ya Rais Dkt Samia Suluhu na Mbunge wao Hamisi Mwijuma “Mwana FA” inatimia
Mwenyekiti huyo wa Halmashauri alisema kwamba wanahitaji umoja na mshikamano hivyo wasitoe nafasi ya mpasuko bali waonyeshe umoja ili waweze kuijenga Halmashauri hiyo.
Mwisho.
EmoticonEmoticon