Na Oscar Assenga,TANGA
MGOMBEA Urais kupitia Chama cha NLD Doyo Hassani Doyo amesema kwamba akipata ridhaa ya kuwa Rais Ubunge itakuwa ni nafasi ya wito na ndani ya miaka mitano hivyo mtu akipelekewa fomu ya ubunge atatimua mbio kwa sababu hakutakuwa na maslahi.
Doyo aliyasema hayo leo wakati alipozindua Kampeni za chama hicho Taifa zilizofanyika eneo la Komesho Jijini Tanga ambapo alisema kwa sababu atakwenda kushusha maslahi ya wabunge ili kusiwe na fujo kwenye vyama vya siasa kwa kushusha kiwango cha mshahara wao kwa mwezi
Alisema kwamba kwa sasa mbunge analipwa milioni 12 kila mwezi wakati daktari bingwa analipwa Milioni 1.8 hivyo iwapo akipata ridhaa ya kuwa Rais atashusha viwango hivyo kwa wabunge ili walipwe madaktari bingwa kutokana na kazi kubwa wanayoifanya kuwahudumia watanzania
“Niwaambie hapa kwamba nikiwa Rais Ubunge itakuwa nafasi ya wito na ndani ya miaka mitano mtu akipelekewa fomu ya ubunge atatimua mbio kwa sababu hakuna pesa na nitakwenda kushusha maslahi ya wabunge ili kusiwe fujo kwenye vyama vya siasa mbunge analipwa milioni 12 uzalendo uko wapo wakati daktari bingwa analipwa milioni 1.8 lakini mwana sasia analipwa milioni 12 kwa mwezi nikiwa rais mbunge atalipwa mlioni 1.5 na Daktari Bingwa atalipwa milioni 12”Alisema Doyo
“Hatutaki mchezo ni nchi hii viongozi wa Serikali wamekuwa wakitunga kanuni kwa ajili ya faida ya maisha yao wakati mama mjamzito anatozwa fedha kwa ajili ya kujifungua laki moja mbunge analipwa milioni 12 kwa mwezi na sitingi allowance lakini mtanzania maskini anakwenda kulipishwa laki moja mama yake akijifungua mdogo wake"Alisema
Hata hivyo alisema kwamba hilo haliwezekani ndio maana aliwaeleza kwamba akiingia madarakani ndani ya siku 100 za kwanza atapiga marufuku wakina mama wakienda kujifungua kutozwa gharama zozote ndio maana amekuja Tanga kuomba kura ili awe Rais wa nchi ili aondoe kero zinazowakabili.
Ajira kwa vijana
Alisema kwamba Serikali ya NLD itahakikisha inaboresha ajira kwa vijana ikiwemo kuimarisha uzalishaji wa mazao mbalimbali ikiwemo ya chakula na kuhakiksha wazee wanapata matibabu bora.
EmoticonEmoticon