MCC RAJAB APIGA KURA PANGANI,AIPONGEZA INEC KWA KUWEKA UTARATIBU MZURI WA UPIGAJI KURA VITUONI

October 29, 2025



Na Oscar Assenga,PANGANI.

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa (MCC) Rajabu Abdurhamani ameipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi(INEC) kwa kuweka utaratibu mzuri wa watanzania kupigia kura kwenye vituo mbalimbali hapa nchini.

Pongezi hizo alizitoa leo mara baada ya kupiga kura katika kituo cha Pangani Mashariki ambapo aliungana na wananchi wa eneo hilo kupiga kura kwa ajili ya kuwachagua viongozi mbalimbali akiwemo Rais,Wabunge na Madiwani.

Alisema kwamba ameanzia Pangani lakini anategemea baadae kwenye maeneo mengine na amejionea namna hali ilivyo katika vituo vya kupigia kura kutokana na mpango mzuri uliowekwa na tume na hivyo kuwawezesha wananchi kutimiza haki yao na msingi bila kuwepo kwa changamoto yoyote ile.

“Kwa kweli katika hili niwapongeze sana Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kwa kuweka utaratibu mzuri nimeuliza hapa nimeambiwa watu wanapiga kura na utaratibu uliowekwa ni mzuuri na hivyo kuwawezesha wananchi kutimiza haki yay a msingi bila vikwazo vyoyote”Alisema

“Lakini kabla ya uchaguzi huu tulipita kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kwa kipindi cha miezi miwili hivyo leo nimeona nitimize wajibu wangu wa kupiga kura na hivyo kuhamasisha wananchi kama viongozi tunapiga kuwa na wao kutoka kwa wingi kupiga kura”Alisema

Hata hivyo alisema kwamba wananchi ni vema kuendelea kujitokeza kwa wingi kutokana na hali ya amani,mshikamano umetawala na kila mmmoja anapata haki yay a kupiga kura katika maeneo waliopo.






Share this

Related Posts

Previous
Next Post »