Showing posts with label siasa. Show all posts
Showing posts with label siasa. Show all posts

NIKIWA RAIS UBUNGE ITAKUWA NAFASI YA WITO- DOYO

September 04, 2025 Add Comment


Na Oscar Assenga,TANGA


MGOMBEA Urais kupitia Chama cha NLD Doyo Hassani Doyo amesema kwamba akipata ridhaa ya kuwa Rais Ubunge itakuwa ni nafasi ya wito na ndani ya miaka mitano hivyo mtu akipelekewa fomu ya ubunge atatimua mbio kwa sababu hakutakuwa na maslahi.

Doyo aliyasema hayo leo wakati alipozindua Kampeni za chama hicho Taifa zilizofanyika eneo la Komesho Jijini Tanga ambapo alisema kwa sababu atakwenda kushusha maslahi ya wabunge ili kusiwe na fujo kwenye vyama vya siasa kwa kushusha kiwango cha mshahara wao kwa mwezi

Alisema kwamba kwa sasa mbunge analipwa milioni 12 kila mwezi wakati daktari bingwa analipwa Milioni 1.8 hivyo iwapo akipata ridhaa ya kuwa Rais atashusha viwango hivyo kwa wabunge ili walipwe madaktari bingwa kutokana na kazi kubwa wanayoifanya kuwahudumia watanzania

“Niwaambie hapa kwamba nikiwa Rais Ubunge itakuwa nafasi ya wito na ndani ya miaka mitano mtu akipelekewa fomu ya ubunge atatimua mbio kwa sababu hakuna pesa na nitakwenda kushusha maslahi ya wabunge ili kusiwe fujo kwenye vyama vya siasa mbunge analipwa milioni 12 uzalendo uko wapo wakati daktari bingwa analipwa milioni 1.8 lakini mwana sasia analipwa milioni 12 kwa mwezi nikiwa rais mbunge atalipwa mlioni 1.5 na  Daktari Bingwa atalipwa milioni 12”Alisema Doyo
 

“Hatutaki mchezo ni nchi hii viongozi wa Serikali wamekuwa wakitunga kanuni kwa ajili ya faida ya maisha yao wakati mama mjamzito anatozwa fedha kwa ajili ya kujifungua laki moja mbunge analipwa milioni 12 kwa mwezi na sitingi allowance lakini mtanzania maskini anakwenda kulipishwa laki moja mama yake akijifungua mdogo wake"Alisema

Hata hivyo alisema kwamba hilo haliwezekani ndio maana aliwaeleza kwamba akiingia madarakani ndani ya siku 100 za kwanza atapiga marufuku wakina mama wakienda kujifungua kutozwa gharama zozote ndio maana amekuja Tanga kuomba kura ili awe Rais wa nchi ili aondoe kero zinazowakabili.


Ajira kwa vijana



Alisema kwamba Serikali ya NLD itahakikisha inaboresha ajira kwa vijana ikiwemo kuimarisha uzalishaji wa mazao mbalimbali ikiwemo ya chakula na kuhakiksha wazee wanapata matibabu bora.


MGOMBEA MWENZA WA URAIS WA CCM BALOZI NCHIMBI AKIWAHUTUBIA WAKAZI MJI MDOGO WA ISAKA WILAYA YA KAHAMA

September 04, 2025 Add Comment


 Mgombea Mwenza wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi  akiwahutubia Wakazi wa mji mdogo wa Isaka wilayani Kahama, jimbo la Msalala,kwenye mkutano mdogo wa hadhara leo Alhamis Septemba 4,2025,mkoani Shinyanga.

Pamoja na mambo mengine Dkt Nchimbi pia aliwanadi wagombea Ubunge,akiwemo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Msalala Mabula Johnson Magangila pamoja na Madiwani.




Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi anaendelea na mikutano yake ya Kampeni Mkoani Shinyanga ya kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030,ambayo inalenga kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa Maendeleo katika miaka mitano ijayo huku akitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM,Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani wa Chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025.

MAVUNDE AWEKA WAZI MIKAKATI YA KUIPAISHA MTUMBA KIUCHUMI

MAVUNDE AWEKA WAZI MIKAKATI YA KUIPAISHA MTUMBA KIUCHUMI

September 04, 2025 Add Comment

 

Na Alex Sonna,Dodoma

Katika jitihada za kuboresha maisha ya wananchi na kuleta maendeleo ya kweli, Mhe. Anthony Mavunde ameahidi kuibadilisha sura ya Jimbo la Mtumba endapo atachaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo hilo.

Akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa kampeni Dodoma Mavunde alisema kuwa anahitaji ridhaa ya wananchi wa Jimbo hilo ili aweze kuwatumikia kwa ufanisi zaidi kwa sababu yeye ni mtumishi wa watu, na anaelewa kwa undani kero na changamoto zinazowakabili.

Amesema moja ya malengo yake makuu ni kuhakikisha Mtumba inageuka kuwa mji wa kisasa unaong'aa, hasa kwa kuzingatia kuwa Serikali inatekeleza mradi wa ujenzi wa mji mpya wa Serikali kwa gharama ya shilingi bilioni 600.

Ameongeza kuwa Kupitia mpango huu, Mavunde anataka kuona Mtumba inakuwa kitovu cha maendeleo na huduma bora kwa wakazi wake.

Katika sekta ya elimu, Mavunde amekuwa mstari wa mbele. Tayari amejenga shule mbalimbali zikiwemo Shule ya Msingi Chiwondo, Mkoyo na Mahomanyika Sekondari.

Ameahidi kwamba endapo atapata nafasi ya kuwa mbunge, atahakikisha kila eneo lenye upungufu wa shule linapatiwa shule ili watoto wote wapate haki ya msingi ya elimu. Kwa sasa ujenzi wa Shule ya Chawha unaendelea, hatua inayodhihirisha dhamira yake ya kuboresha elimu.

Mavunde pia amegusia changamoto ya michango ya mitihani ya Jumamosi, akisema kuwa atahakikisha michango hiyo inaondolewa ili kupunguza mzigo kwa wazazi.

Aidha, amesema kuwa atahakikisha barabara ya Hombolo – Mayamaya pamoja na barabara nyingine za ndani katika mitaa mbalimbali ambazo ni korofi, zinatengenezwa. Ameahidi kununua greda maalum litakalotumika kuimarisha barabara hizo mara kwa mara.

Katika sekta ya maji, Mavunde amesema kuwa uwezo wa kuzalisha maji jijini Dodoma umefikia lita milioni 47 kwa siku na kueleza kuwa lengo lake ni kuhakikisha kata zote ikiwemo Hombolo, Ihumwa, na Mahomanyika zinapata huduma ya maji safi na salama.

Ameahidi kuwa huduma hiyo itatolewa bure kwa baadhi ya maeneo yenye uhitaji mkubwa kama njia ya kupunguza gharama kwa wananchi.

Baadhi ya wananchi wa Jimbo la Mtumba wamezungumza na Mzalendo Blog kuwa Mavunde anaonekana kuwa na maono makubwa kwa Jimbo lake, akilenga kuboresha miundombinu, huduma za kijamii na uchumi wa wananchi.

DKT.NCHIMBI AWAOMBA WANANCHI SHINYANGA KUMPIGIA KURA ZA KISHINDO ZA URAIS DKT.SAMIA ,WABUNGE NA MADIWANI

September 03, 2025 Add Comment


MGOMBEA Mwenza wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amewahutubia maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Shinyanga ambapo ametumia nafasi hiyo kuwaomba kumpigia kura za kishindo mgombea Urais wa CCM Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, wabunge na madiwani.


Dk.Nchimbi  ametoa ombi hilo leo Septemba 3,2025 alipokuwa akiwahutubia maelfu ya wananchi kwenye mkutano mkubwa wa hadhara ambapo katika mkutano huo amewanadi  Wabunge wa Mkoa huo akiwemo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi.


Wengine ni  Mgombea Ubunge Jimbo la Kishapu, Lucy Mayenga , Jimbo la Solwa Ahmed na Itwangi na Azza Hillal pamoja na madiwani.

Dkt. Nchimbi ameendelea kunadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030,ambayo kimsingi imelenga kwenda kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa Maendeleo katika miaka mitano ijayo.

Aidha amekuwa akitumia  nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM,Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani wa Chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025



TUME YATOA MWALIKO KWA WAANDISHI WA HABARI WENYE NIA YA KURIPOTI MATUKIO WAKATI WA UCHAGUZI

September 03, 2025 Add Comment