Rais Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Chakula Barani Afrika akiwa na Profesa Mary Abukutsa-Onyango kutoka Kenya (kulia) na Mercy Diebiru-Ojo kutoka Nigeria ambao ni washindi wa Tuzo ya Chakula Barani Afrika kwa mwaka 2025 (Africa Food Prize 2025) kwenye hafla iliyofanyika mjini Dakar, Senegal, pembezoni mwa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AFSF) linaloendelea kuanzia tarehe 1 hadi 5 Septemba 2025.
Rais Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Chakula Barani Afrika akiwa na Mwenyekiti wa AGRA NA Waziri Mkuu Mstaafu wa Ethiopia, Mhe Hailemariam Dessalegn na Profesa Mary Abukutsa-Onyango kutoka Kenya na Mercy Diebiru-Ojo kutoka Nigeria ambao ni washindi wa Tuzo ya Chakula Barani Afrika kwa mwaka 2025 (Africa Food Prize 2025) kwenye hafla iliyofanyika mjini Dakar, Senegal, pembezoni mwa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AFSF) linaloendelea kuanzia tarehe 1 hadi 5 Septemba 2025.

Wanasayansi wanawake wawili – Profesa
Mary Abukutsa-Onyango kutoka Kenya na Mercy Diebiru-Ojo kutoka Nigeria –
wametangazwa washindi wa Tuzo ya Chakula Barani Afrika kwa mwaka 2025 (Africa
Food Prize 2025).
Tuzo hiyo, yenye thamani ya Dola za
Marekani 100,000, ilikabidhiwa na Rais Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Chakula Barani
Afrika.
Hafla ya kukabidhi tuzo ilifanyika
mjini Dakar, Senegal, pembezoni mwa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AFSF)
linaloendelea kuanzia tarehe 1 hadi 5 Septemba 2025.
Katika hotuba yake, Dkt. Kikwete
aliwapongeza washindi kwa mchango wao wa kipekee katika tafiti zinazolenga kuongeza
tija ya uzalishaji na kuboresha maisha ya wakulima wadogo barani Afrika.
“Tuzo hii inadhihirisha nafasi kubwa ya
wanasayansi wa Afrika katika kutafuta suluhu za changamoto za kilimo. Ingawa
mwaka huu imeenda kwa washindi wawili, tunatambua kazi kubwa inayoendelea
kufanywa na watu binafsi na taasisi nyingi ili kuhakikisha bara letu linakuwa
na mifumo imara na endelevu ya chakula,” alisema Dkt. Kikwete.
Profesa Abukutsa-Onyango amejikita
katika tafiti za mboga mboga za asili za Kiafrika kama mchicha, sukuma wiki,
mgagani, mchunga, figiri na kisamvu, akihamasisha uzalishaji na ulaji wake kwa
madhumuni ya kuimarisha lishe.
Kwa upande wake, Mercy Diebiru-Ojo
anasifika kwa kubuni na kuendeleza teknolojia ya kisasa ya uzalishaji na
upandikizaji wa mbegu za mihogo kwa kutumia mbinu ya semi-autotrophic
hydroponic technology, ambayo imeongeza mavuno na tija katika kilimo hicho
muhimu barani Afrika.
Tuzo ya Chakula Barani Afrika
ilianzishwa mwaka 2005 chini ya mwamvuli wa mpango wa Mageuzi ya Kijani Afrika
(AGRA). Inatolewa kila mwaka kwa watu binafsi au taasisi zinazotoa mchango wa
kipekee katika kuimarisha mifumo ya chakula na maendeleo ya sekta ya kilimo.
Kwa mwaka huu 2025, jumla ya maombi 601
kutoka ndani na nje ya Afrika yaliwasilishwa kuwania heshima hii kubwa.
EmoticonEmoticon