Mhandisi wa Tanga Uwasa Salum Ngumbi wakati wa ziara ya wateja na mabalozi wa maji kutembelea miradi inayotekelezwa na mamlaka hiyo ili kujifunza na kupata elimu juu ya matumizi sahihi ya maji.
Devotha Mayalla akizungumza wakati wa ziara ya wateja na mabalozi wa maji kutembelea miradi inayotekelezwa na mamlaka hiyo ili kujifunza na kupata elimu juu ya matumizi sahihi ya maji.
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi Mazingira (Tanga Uwasa) umeweka bayana mikakati waliokuwa nayo kwa sasa wa kufufua visima vyote vya maji zilivyokuwa vinatumika ili kupunguza kero ambazo zinaweza kuzuilika.
Mkakati huo uliwekwa hadharani na Mhandisi wa Tanga Uwasa Salum Ngumbi wakati wa ziara ya wateja na mabalozi wa maji kutembelea miradi
inayotekelezwa na mamlaka hiyo ili kujifunza na kupata elimu juu ya
matumizi sahihi ya maji.
Alisema visima hivyo vipo katika maeneo ya uwanja wa ndege,na Mwakileo ikiwa ni mbadala wa maji kwa wananchi,ikitokea kupungua kwa maji ili waweze kuvitumia kwa ajili ya kuwafikia wananchi pasipo kuwepo na kizuizi chochote.
Alisema pamoja na kufufua visima hivyo lazima watahakikisha wanaendelea kutoa huduma bora kwa wananchi ambao wamekuwa wakiwahudumia kila siku ili kuondosha vikwazo ambavyo wanaweza kukutana navyo.
"Mpango tulionao kwa sasa ni kuhakikisha kuwa wateja wetu wanapata maji kukidhi mahitaji muhimu kwa wananchi,pia tuna mpango wa kuanza miradi ya maendeleo katika mamlaka ya maji ikiwemo mradi wa ujenzi wa kutanua bwawa la mabayani na tunatarajia uanze septemba mwaka huu".
Upatikanaji wa maji kwa siku katika maeneo yote ni lita 30,000,ambapo kwa sasa mtambo uliopo ni kwa ajili ya kutanua uzalishaji kufikia lita 45,000 ambayo itasaidia kukidhi haja kwa wananchi wote.
“Kwa sasa upo
mradi uliogharimu zaidi ya sh.Bilioni 10 ambapo fedha hizo ni kwa ajili
ya kuboresha huduma ya maji katika jamii kwani tunafanya hivi
kuhakikisha yaliyojitokeza kwa wananchi kukumbana na changamoto ya
huduma hii hayajitokezi tena na hali iliweza kuwaathiri wakazi katika
maeneo mbalimbali Jijini Tanga kutokana na mvua kutokunyesha kwa kipindi
kirefu na kusababisha Bwawa la Maji kupungua”Alisema
"Tuna
mitambo minne ambayo miwili ndio inatumika Kwa Sasa ns inasaidia
kupandisha Maji mpaka kuwafikia wananchi na mingine miliwi ipo kwa
ajili ya akiba kama ikitokea mmoja kati ya hii ikiharibika"
Mhandisi salum aliwashauri pia wakazi wa Tanga kupanda miti
itakayosaidia kutunza mazingira muda wote na kusababisha kunyesha mvua
za mara Kwa mara Ili kuwepo na upatikanaji wa Maji
“Suala la
miti kuwa michache katika maeneo yetu tunayoishi ni Changamoto niwaombe
wananchi kupanda miti Ili kusaidia mazingira yetu muimarika na Hata mvua
ziweze kunyesha Ili tupate maji muda wote”Alisema
Akielezea
changamoto ya ukosefu wa Maji tokea mwezi Novemba Mwaka jana ambapo
alieleza mpaka kufikia mwezi Machi mwaka huu hali hiyo imeweza kuimarika
hivyo amewaomba wakazi wote kutumia Maji kwa umakini na ikiwemo kujenga
utamaduni ya kuyahifadhi kwa ajili ya kuwasaidia katika maatumizi yao.
"Kuanzia
machi Mwaka huu hali ya upatikanaji wa Maji imeanza kuwa shwari
ingawaje haijafikia asilimia 100 , maeneo mengi yanapata maji na
vilevile Tanga Uwasa tumejipanga kutatua changamoto iliyokuwepo"Alisema
Mhandisi Salum
Naye kwa upande wake Mtaalamu wa Maabara kutokea
kwenye mtambo wa kutibu Maji wa Mowe Amos Rwehangana alisema kwa sasa
hali ya kutoka kwa Maji ipo vizuri katika maeneo mbalimbali yakiwa
masafi na hayawezi kuleta athari yoyote katika jamii na hiyo inatokana
na juhudi walizonazo .
EmoticonEmoticon