Na Mathias Canal, Dar es salaam
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano
da Silva, leo Jumanne Septemba 5, 2017 amefanya mazungumzo na waziri wa kilimo
Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya kikazi
nchini Tanzania.
Katika
ziara hiyo Bw. Graziano da Silva atafanya mazungumzo na viongozi waandamizi wa
Serikali, wadau na anatarajiwa kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,
Dkt. Ali Mohamed Shein sambamba na Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi
wa Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed.
Ziara hii
ya Mkurugenzi Mkuu inajili wakati FAO ikiadhimisha miaka 40 toka kuanza
shughuli zake hapa Tanzania Hafla ambayo itahudhuriwa na Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi. Samia Suluhu Hassan.
Katika
mazungumzo na Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mkurugenzi Mkuu wa FAO anabadilishana
mawazo na Serikali ya Muungano wa Tanzania kwenye masuala makuu yanayohusiana
na uhakika wa chakula na maendeleo ya kilimo, ikijumuisha juhudi za FAO kitaifa
na kikanda.
Pia
yamejadiliwa mambo mengine yanayohusiana na ushirikiano kati ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na FAO, pia masuala ya umuhimu kati ya pande hizo mbili.
Mbali ya
Maafisa wa Serikali, Mkurugenzi Mkuu atakutana na wadau wengine wa FAO hapa
nchini wakiwa ni pamoja na asasi za kiraia, taasisi za elimu, na taasisi za
utafiti.
Baadae
Mkurugenzi Mkuu ataenda Zanzibar ambapo, miongoni mwa mambo mengine,
anategemewa kuweka jiwe la msingi katika jengo la Mradi wa Kuzalisha vifaranga
vya samaki unaofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Korea kupitia Shirika lake
la Maendeleo ya Kimataifa KOICA.
Pia Bw.
Graziano da Silva atapata fursa ya kutembelea mradi wa kilimo cha mwani na pia
kuona maonesho ya bidhaa mbali mbali zilizotengenezwa na wanawake
wanaojihusisha na kilimo cha mwani.
Waziri wa
Kilimo Mifugo na Uvuvi Dkt Charles Tzeba alisema kuwa ujio wa Bw. Graziano da
Silva nchini unaakisi ushirikiano bora uliopo kati ya Tanzania na Shirika la
Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO) ambapo hivi karibuni ILO
walisaidia katika kuandaa mpango wa kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabia
nchi kwa kutoa fedha ya kutengeneza programu ya kutoa maarifa kwa wananchi ya
namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika kilimo.
Dkt Tzeba
alisema kuwa tayari jarida limeshatengenezwa la namna ambavyo wananchi hususani
wakulima katika kilimo chao wataweza kukabiliana na hali ya ukame au mafuriko
kutokana na mvua zilizozidi kiwango.
Sambamba
na hayo Mhe Tzeba alisema pia FAO wametoa simu 50 na Kompyuta 15 kwa wizara ya
Kilimo Mifugo na Uvuvi kwa ajili ya wataalamu wake kuwa na urahisi wa kukusanya
taarifa na kuzifikisha kwa jamii.
Tanzania
ilijiunga na FAO mwaka 1962, na mwaka 1977 FAO ilifungua ofisi zake hapa Tanzania. Katika
miaka 40 ya uwepo wake, FAO imeisadia Serikali ya Tanzania katika kupanga na
kutekeleza sera, mikakati na mipango ya kilimo hapa nchini.
Kazi ya
FAO imejikita katika kuboresha usalama wa chakula na lishe pamoja na maisha ya
wakulima wadogo na hivyo kuwa chachu ya kukua kwa uchumi kupitia sekta ya
kilimo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano
da Silva (Kulia), akimpongeza Waziri wa kilimo
Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba mara baada ya kuelezea taarifa mbalimbali zihusuzo wizara hiyo. leo Jumanne Septemba 5, 2017.
Waziri wa kilimo
Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano
da Silva, kuzungumzia ujio wake nchini na ushirikiano baina ya FAO na serikali ya Tanzania. leo Jumanne Septemba 5, 2017.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano
da Silva, akizungumzia na wataalamu mbalimbali katika Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi juu ya ujio wake nchini na ushirikiano baina ya FAO na serikali ya Tanzania. Kulia kwake ni Waziri wa kilimo
Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba. leo Jumanne Septemba 5, 2017.
Wataalamu mbalimbali katika Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano
da Silva.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José
Graziano
da Silva (Kushoto) akiteta jambo na mwenyeji wake Waziri wa kilimo
Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba mara baada ya kutembelea ofisini kwake. leo Jumanne Septemba 5, 2017.
Waziri wa kilimo
Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba akipokea simu 50 kutoka kwa Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José
Graziano
da Silvakwa ajili ya wataalamu wa kilimo kuzitumia kukusanya taarifa mbalimbali na kuziwasilisha kwa jamii. leo Jumanne Septemba 5, 2017.
Waziri wa kilimo
Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba akionyesha moja ya siku kati ya 15 alizokabidhiwa na Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José
Graziano
da Silva kwa ajili ya wataalamu wa kilimo kuzitumia kukusanya taarifa mbalimbali na kuziwasilisha kwa jamii. leo Jumanne Septemba 5, 2017.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José
Graziano
da Silva akiteta jambo na Waziri wa kilimo
Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba mara baada ya kupokea zawadi. leo Jumanne Septemba 5, 2017.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José
Graziano
da Silva akipokea zawadi ya vinyago kutoka kwa Waziri wa kilimo
Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba mara baada ya mazungumzo ya kikazi kumalizika. leo Jumanne Septemba 5, 2017.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José
Graziano
da Silva akiwaaga watendaji wa wizra ya kilimo Mifugo na Uvuvi mara baada ya kumalizika kwa mkutano akiwa na mwenyeji wake Waziri wa kilimo
Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba. leo Jumanne Septemba 5, 2017.
Picha ya pamoja kati ya Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José
Graziano
da Silva (Aliyeketi kwenye kiti kulia), Waziri wa kilimo
Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba, Katibu Mkuu wizara ya kilimo Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Dkt Maria mashingo na wataalamu wengine kutoka FAO na Wizara ya kilimo.
EmoticonEmoticon