Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (aliyesimama) akiwasilisha Itifaki
Nyongeza ya Tano hadi ya Tisa ya Umoja wa Posta Duniani (UPU) mbele ya
wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu (hawapo pichani) ili iweze
kuridhiwa na Kamati hiyo. Aliyevaa tai ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo
Eng. Edwin Ngonyani. Wasilisho hilo limefanyika mjini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya
Bunge ya Miundombinu Mhe. Moshi S. Kakoso (wa kwanza kulia) akiendesha
kikao cha Kamati hiyo mjini Dodoma wakati Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (hayupo pichani) akiwasilisha Itifaki
Nyongeza ya Tano hadi ya Tisa ya Umoja wa Posta Duniani ili iweze
kuridhiwa. Kushoto ni Katibu wa Kamati hiyo Bi. Hosiana John.
Katibu Mkuu wa Mawasiliano, Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Eng. Maria Sasabo (aliyesimama)
akitoa ufafanuzi kuhusu Itifaki Nyongeza ya Tano hadi ya Tisa ya Umoja
wa Posta Duniani mbele ya Kamati ya Bunge ya Miundombinu mjini Dodoma.
EmoticonEmoticon