CHAMA cha mchezo wa Baiskeli
Mkoa wa Tanga (Chabata) kimeanza mikakati ya kuandaa timu ya mkoa kwa ajili ya
kushiriki mashindano ya mchezo huo taifa ambayo mwaka huu yatafanyika mwezi wa
saba mkoani Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama hicho
mkoa wa Tanga, Dege Masoli aliliambia gazeti hili kuwa timu ya mkoa
itachaguliwa kutokana na mashindano ya mchezo huo ngazi ya mkoa ambayo yataanza
mwezi mei ambapo pia katika watayatumia kwa ajili ya kuwachuja wachezaji ambao
wataunda timu ya mkoa.
Masoli alisema licha ya kuwa
na mikakati hiyo lakini pia chama chao kinakabiliwa na changamoto mbalimbali
ikiwemo uhaba wa fedha hali ambayo inapelekea timu ya mchezo huo kushindwa
kuanza maandalizi mapema.
“Tatizo la uhaba wa fedha katika chama chetu
limekuwa suala kubwa sana hivyo tunawaamba wadau mbalimbali kuweza kujitokeza
kwa ajili ya kutusapoti ili tuweze kushiriki vema mashindano ngazi ya Taifa
“Alisema Masoli.
Aliongeza kuwa wanawaomba
wadau kutoka maeneo mbalimbali,wakiwemo viongozi wa serikali,makampuni, na
taasisi binafsi kuangalia namna gani wanaweza kuisaidia timu hiyo iweza kufikia
malengo yake.
Mwenyekiti huyo alisema wachezaji
5 ndio ambao watachaguliwa ili kwenda kuuwakilisha mkoa katika mashindano ya
Taifa ambapo kwa sasa timu ya mkoa wa Tanga ilianza mazoezi .
Mwisho.
EmoticonEmoticon