Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, TANESCO, Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga amesema umeme ni nishati nafuu zaidi kupikia na kuwahimiza Wanzania kutumia fursa ya uwepo wa umeme katika kila Kijiji na kutumia nishati hii kupikia ambapo watapunguza gharama pamoja na kutunza mazingira.
Mha. Gissima ameyasema hayo Machi 4, 2025 katika Kongamano la Wanawake la Kuhamasisha Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia ya Umeme lililofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City ambapo Mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko ambae aliambatana na Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga.
“Kwa sasa umeme umefika kwenye kila Kijiji hivyo ni vizuri kwa Watanzania kufahamu ya kuwa wanayo fursa ya kupika kwa kutumia nishati safi ya umeme. Tunaendelea kuwahimiza na kuwafahamisha ya kuwa umeme ni nishati safi zaidi na nafuu zaidi ya kupikia”, amesisitiza Mha. Gissima.
EmoticonEmoticon