Mtaalam wa maswala ya maji Kanda ya Afrika Mashariki wa UNESCO's ROEA, Alexandros Makarigakis (kulia) akibadilishana mawazo na Katibu wa Maji Kutoka Wizara ya Maji, Usafi wa Mazingira na Umwagiliaji nchini Kenya, Mhandisi Samweli Alima (kulia) wakati wa uzinduzi wa mradi wa "Unlocking the Ground Water Potential of the Kilimanjaro Water Tower" (Uchakataji wa taarifa za maji ya ardhini chini ya Mlima Kilimanjaro) unaofanyika katika Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.Picha ya Pamoja ya washiriki wa uzinduzi wa mradi wa "Unlocking the Ground Water Potential of the Kilimanjaro Water Tower" (Uchakataji wa taarifa za maji ya ardhini chini ya Mlima Kilimanjaro) unaofanyika katika Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.
Mtaalam wa maswala ya maji wa Kanda ya Afrika Mashariki wa UNESCO's ROEA, Alexandros Makarigakis akitoka salamu za UNESCO wakati wa uzinduzi wa mradi wa "Unlocking the Ground Water Potential of the Kilimanjaro Water Tower" (Uchakataji wa taarifa za maji ya ardhini chini ya Mlima Kilimanjaro) unaofanyika katika Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.
Baadhi ya washiriki Kutoka Tanzania na Kenya walioshiriki uzinduzi wa mradi wa "Unlocking the Ground Water Potential of the Kilimanjaro water tower" (Uchakataji wa taarifa za maji ya ardhini chini ya Mlima Kilimanjaro) unaofanyika katika Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.
Baadhi ya washiriki Kutoka Tanzania na Kenya walioshiriki uzinduzi wa mradi wa "Unlocking the Ground Water Potential of the Kilimanjaro water tower" (Uchakataji wa taarifa za maji ya ardhini chini ya Mlima Kilimanjaro) unaofanyika katika Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.
Na Mwandishi wetu, Arusha.
MATAIFA ya Tanzania na Kenya yanatarajiwa kunuifaka na programu ya pamoja ya utafiti wa maji ya chini ya ardhi ya Mlima Kilimanjaro inayowezeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Shirika la Chakula la Kilimo (FAO).
Programu hiyo ya miaka mitano inayofadhiliwa na Shirika la Uhifadhi wa Mazingira Duniani GEF inagharimu dola za Marekani milioni 8.
Mtaalamu wa maswala ya maji Kanda ya Afrika Mashariki wa UNESCO's ROEA, Alexandros Makarigakis anasema ongezeko la idadi ya watu na mahitaji yao ya maji kwa shughuli mbalimbali zimesababisha wao kufikiria kufanya utafiti wa maji ya ardhini
"Tunaona idadi ya watu inaongezeka na hatupaswi kuangalia mahitaji yao ya sasa tu bali yajayo na mradi huu utasaidia kufahamu vizuri chanzo na kuiongoza jamii namna gani ya kukitunza na kukilinda chanzo hicho" ameeleza Alexandros.
Akizungumza mara baada ya uzinduzi wa mradi wa "Unlocking the groundwater potential of the Kilimanjaro water tower" (Uchakataji wa taarifa za maji ya ardhini chini ya Mlima Kilimanjaro) Mhandisi Maximilian Sereka kutoka Wizara ya Maji Kitengo cha Maji shirikishi ambaye amemwakilisha Mkurugenzi wa Rasilimali Maji Tanzania anasema mradi waliouzindua utasaidia kufanya utafiti na kubaini kina cha maji chini ya ardhi ya mlima Kilimanjaro.
"Mradi huu utasaidia kubadilishana taarifa za utafiti kwa nchi ya Tanzania na Kenya ambazo zitasaidia kufahamu ubora na wingi wa maji huku shabaha ikiwa ni kuboresha maisha ya jamii inayozunguka mlima Kilimanjaro" amesema Mhandisi Sereka.
Katibu wa Maji katika Wizara ya Maji, Usafi wa Mazingira na Umwagiliaji wa nchini Kenya katika mkutano huo wa siku tatu, Mhandisi Samweli Alima amesema nchi yake haijawekeza vya kutosha kwenye maji ya chini ya Ardhi bali ni maeneo machache kama Nakuru, hivyo mradi huo utaenda kuufanya mji wa Mombasa utegemee maji ya ardhini.
"Miji inayozunguka mlima Kilimanjaro na kupitiwa na mikondo ya maji ni Kajiado na Taita nchini Kenya huku Tanzania ikienda hadi mikoa ya jirani na Kilimanjaro kama Manyara hivyo ni vyanzo vinavyovuka mipaka vyenye wakazi zaidi ya milioni mbili" amefafanua mhandisi Alima
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bonde la Pangani, Bw. Segule Segule anasema mradi huu utasaidia kupata taarifa wasizozijua za mwambamaji unaokatiza nchi ya Tanzania na Kenya
Kwa mujibu wa Maelezo kutoka UNESCO, utafiti wa mradi unatarajiwa kufanyika kwa miezi 12.
Mradi wenyewe unatarajiwa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano chini ya ufadhili wa Shirika la Mazingira Duniani (GEF).
Utafiti utafanyika ili kubaini kiwango cha maji kilichopo, yako eneo gani na chanzo chake huku shughuli zinazotarajiwa kufanywa kwa jamii zinazozunguka mlima huo kwa Kenya na Tanzania ni uhifadhi na kuboresha uoto wa asili wa maeneo hayo.
-- Other name :Gadiola Emanuel Digital JourNaList || Athletics Content Creator || Media Manager Athletics Tanzania || Photographer || ICT || PRO || Blogger |Based in Arusha, Tanzania. Mob :+255 784 643 633 E-mail: gadiola25@gmail.com WEB: https://www.wazalendo25.blogspot.com
EmoticonEmoticon