Showing posts with label ziara. Show all posts
Showing posts with label ziara. Show all posts

KATIBU MTENDAJI UNCDF ASIFU MCHANGO WA UWEKEZAJI KUPITIA HATIFUNGANI YA TANGA UWASA KWA JAMII

June 26, 2026 Add Comment


Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA) imepokea ugeni wa viongozi wa kanda na wawakilishi kutoka Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) ukiongozwa na Katibu Mtendaji wa Mfuko huo Bw. Pradeep Kurukulasuriya uliolenga kutembelea na kujionea maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa kuboresha hali ya upatikanaji huduma ya maji Tanga awamu ya tatu kupitia ufadhili wa Hatifungani ya Kijani ambapo UNCDF ni miongoni mwa wadau muhimu walioshiriki katika hatua za awali za kufanikisha mradi huo.

Katika ziara hiyo, Katibu Mtendaji na wageni walipokea taarifa ya mradi na mwenendo wa magawio kwa wawekezaji pamoja na kutembelea eneo la mradi na kujionea kasi ya utekelezaji wa shuguli mbalimbali zinazolenga kuongeza na kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji ya uhakika kwa wakazi wa maeneo ya kihuduma ya Tanga UWASA unaotarajiwa kukamilika mapema mwezi Agosti, 2026.

Katibu Mtendaji pamoja na wageni walipata pia fursa ya kufanya kikao na sehemu ya wanufaika wa mradi wa Hatifungani katika Hospiali ya Jiji iliyopo kata ya Masiwani ambapo awali walikuwa wakipata changamoto katika kutoa huduma kutokana na adha ya upatikanaji wa huduma ya maji ya uhakika na kupitia mradi wa Hatifungani wameboreshewa miundombinu hivyo kuimarisha upatikanaji wa uhakika wa huduma ya majisafi.

Akizungumza mara baada ya ziara hiyo, Katibu Mtendaji wa UNCDF Bw. Pradeep Kurukulasuriya  ameipongeza Tanga UWASA kwa uthubutu huo na kwa maendeleo mazuri ya utekelezaji wa mradi lengwa sambamba na kuonesha nia ya kuongeza wigo wa kuendelea kushirikiana.


" Tunajivunia kuwa sehemu ya mchango katika kufanikisha Hatifungani ya Kijani ya Tanga na matarajio yetu ni kwamba mradi huu utaboresha maisha ya jamii na kupitia hili Tanga UWASA imedhihirisha kuwa inawezekana kuhamasisha uwekezaji ndani ya nchi kwani takriban asilimia 65 ya uwekezaji ulitoka kwa wawekezaji wa Kitanzania, na kwa kupitia mpango huu, tumedhihirisha kuwa mitaji ya ndani inaweza kuhamasishwa ili kufadhili miradi muhimu ya maendeleo na kwa sasa tunasoma mfano huu kwa karibu, tunatafuta kuelewa ni nini kilifanya kazi vizuri, changamoto zipi zilizojitokeza, na ni somo gani tunaweza kujifunza ili tuweze kuiga mafanikio ya Hatifungani ya Tanga si tu ndani ya Tanzania bali katika nchi nyingine pia", alisema Bw. Kurukulasuriya.

Awali kabla ya ziara hiyo, Katibu Mtendaji wa UNCDF na wageni wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Tanga UWASA, Eng. Salum Ngumbi walifika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga kutoa salamu na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe. Dadi Kolimba aliyetoa salamu za Mkoa kwa niaba ya Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Buriani Mkuu wa Mkoa wa Tanga






RAIS SAMIA AWASILI KILIMANJARO AKIELEKEA MKOANI ARUSHA KWA ZIARA YA KIKAZI

March 01, 2026 Add Comment


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA. Amos Makalla na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa ajili ya Ziara ya kikazi mkoani Arusha, tarehe 01 Machi, 2026.



DKT.HASHIL AMSHUKURU RAIS DKT.SAMIA SULUHU KWA UWEZESHAJI WA SERA NA MIONGOZO ILIYOPELEKEA UFUFUAJI VIWANDA NCHINI

October 13, 2025 Add Comment




Na Oscar Assenga, TANGA

WIZARA ya Viwanda na Biashara imemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kwa kuwawezesha Kisera na miongozo ambayo inapelekea ufufuaji wa viwanda nchini hususani katika Mkoa wa Tanga.

Kauli hiyo ilitolewa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt Hashil Abdallah wakati wa ziara yake ya kutembelea viwanda mbalimbali mkoani Tanga inayolenga ufuatiliaji ufufuaji viwanda mkoa wa Tanga ambapo alitembelea kiwanda cha Chuma, Sabuni na Mbao.

Hatua ya ziara ya kiongozi huyo inatajwa kwamba italeta mageuzi makubwa katika ufufuaji viwanda katika mkoa huo ambao miaka ya nyuma kulikuwa na viwanda vingi vilikuwa vinafanya kazi lakini hapo katika viwanda vingi havifanyi kazi.

Alisema ziara hiyo pia ni kuhakikisha Tanga inakuwa ya viwanda ili kujibu mambo mbalimbali ikiwemo changamoto za ajira kwa mkoa wa Tanga kama unavyojua zaidi ya mara mbili Mhe Rais Dkt Samia Suluhu amesisitiza waangalie changamoto za wenye viwanda na wazalishaji ndani ya nchi nzima.

Aidha alisema lakini pia wapeleke jicho lao kwenye mkoa wa Tanga kwa hiyo ni ziara maalumu ya Kiserikali wakiwa wameambana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Rashid Mchata na maofisa wa Serikali wakiangalia utekelezaji wa yale ambayo walikaa na wenye viwanda na kuona walichokuwa wamewahaidi.

“Tunafurahi kiwanda cha kwanza ambacho tumetembelea leo wapo kenye majaribio ya uzalishaji na wamehaidi ndani hya mwezi mmoja uzalishaji wa majaribio utakuwa umekamilika na hivyo kuanza uzalishaji rasmi”Alisema

“Lakini tumetembelea viwanda viwili kimoja cha kuchakata chuma wameshaagiza mashine zipo njiani mwezi ujao watafunga mashine na mwezi wa Desemba watakuwa kwenye majaribio na Januari wataanza uzalishaji”Alisema



Katibu mkuu huyo alisema pia kiwanda kinachohusika na uchakataji wa bidhaa za misitu,magogoro na mbao na kutengeneza bidhaa mbalimbali na mashine zipo njiani lakini wameona mashine mpya contena tatu  zipo ambao wanaanza kuzifunga kuanzia wiki tatu zijazo na wataanza majaribio kuanza desemba na Januari wataanza uzalishaji.

Hata hivyo alisema kwamba ni faraja kubwa kwamba Serikali ya Mkoa wa Tanga na Idara ya Misitu wamewapatia malighafi ambazo zinaweza kuwapatia malighafi kwa muda wa miaka 10 hivyo kwa miaka hiyo mfululizo wana malighafi ya uhakikika.

Awali akizungumza Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Rashid Mchatta alisema wanashukuru kupokea ugeni huo wa katibu mkuu ambaye yupo katika ziara ya ufuatiliaji ufufuaji viwanda mkoa wa Tanga kama unavyofahamu miaka ya nyuma Tanga kulikuwa na viwanda vingi vilikuwa vinafanya kazi.

Alisema lakini hapo katika viwanda vingi vilikuwa havifanyi kazi hivyo ziara hiyo italeta mageuzi makubwa katika kufufua viwanda hivyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa watafanya kazi kwa karibu na Wizara kuhakikisha malengo ya kufufua viwanda yanafanyika na kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji wanaowekeza mkoa wa Tanga ambao una mazingira bora ya uwekezaji kama unavyofahama Bandari inafanya kazi kwa kiwanda kizuri sana.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Kiwanda Ply&Panel Limited Wazalishi wa PlyWood Hussein Moor alisema wanashukuru ziara hiyo ya Katibu Mkuu katika kiwanda hicho ambacho kilikuwa kimesimama muda mrefu lakini kwa sasa tayari wameagiza mashine mpya na nyengine zipo njiani na wanategemea wataalamu watakuja kufunga mashine baada ya kufika zote.

Alisema kwamba ahaidi wanayoitoa kwa Serikali na Wakazi wa Tanga  kwamba kiwanda hicho kitaanza uzalishaji mwakani 2026 huku akiwahaidi wananchi wa mkoa huo ajira zitakuwepo nyingi za moja kwa moja,za mkataba na baadae pia wataleta mashine nyengine mpya na kuwa na ziara ya ajira  

Mwisho.