Na Oscar Assenga, TANGA
WIZARA ya Viwanda na Biashara imemshukuru Rais Dkt
Samia Suluhu kwa kuwawezesha Kisera na miongozo ambayo inapelekea ufufuaji wa
viwanda nchini hususani katika Mkoa wa Tanga.
Kauli hiyo ilitolewa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Viwanda na Biashara Dkt Hashil Abdallah wakati wa ziara yake ya kutembelea viwanda
mbalimbali mkoani Tanga inayolenga ufuatiliaji ufufuaji viwanda mkoa wa Tanga
ambapo alitembelea kiwanda cha Chuma, Sabuni na Mbao.
Hatua ya ziara ya kiongozi huyo inatajwa kwamba italeta mageuzi makubwa katika ufufuaji viwanda katika mkoa huo ambao miaka ya nyuma kulikuwa na viwanda vingi vilikuwa vinafanya kazi lakini hapo katika viwanda vingi havifanyi kazi.
Alisema ziara hiyo pia ni kuhakikisha Tanga inakuwa
ya viwanda ili kujibu mambo mbalimbali ikiwemo changamoto za ajira kwa mkoa wa
Tanga kama unavyojua zaidi ya mara mbili Mhe Rais Dkt Samia Suluhu amesisitiza
waangalie changamoto za wenye viwanda na wazalishaji ndani ya nchi nzima.
Aidha alisema lakini pia wapeleke jicho lao kwenye
mkoa wa Tanga kwa hiyo ni ziara maalumu ya Kiserikali wakiwa wameambana na
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Rashid Mchata na maofisa wa Serikali wakiangalia
utekelezaji wa yale ambayo walikaa na wenye viwanda na kuona walichokuwa wamewahaidi.
“Tunafurahi kiwanda cha kwanza ambacho tumetembelea
leo wapo kenye majaribio ya uzalishaji na wamehaidi ndani hya mwezi mmoja
uzalishaji wa majaribio utakuwa umekamilika na hivyo kuanza uzalishaji rasmi”Alisema
“Lakini tumetembelea viwanda viwili kimoja cha kuchakata chuma wameshaagiza mashine zipo njiani mwezi ujao watafunga mashine na mwezi wa Desemba watakuwa kwenye majaribio na Januari wataanza uzalishaji”Alisema
Katibu mkuu huyo alisema pia kiwanda kinachohusika na uchakataji wa bidhaa za misitu,magogoro na mbao na kutengeneza bidhaa mbalimbali na mashine zipo njiani lakini wameona mashine mpya contena tatu zipo ambao wanaanza kuzifunga kuanzia wiki tatu zijazo na wataanza majaribio kuanza desemba na Januari wataanza uzalishaji.
Hata hivyo alisema kwamba ni faraja kubwa kwamba
Serikali ya Mkoa wa Tanga na Idara ya Misitu wamewapatia malighafi ambazo
zinaweza kuwapatia malighafi kwa muda wa miaka 10 hivyo kwa miaka hiyo mfululizo
wana malighafi ya uhakikika.
Awali akizungumza Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga
Rashid Mchatta alisema wanashukuru kupokea ugeni huo wa katibu mkuu ambaye yupo
katika ziara ya ufuatiliaji ufufuaji viwanda mkoa wa Tanga kama unavyofahamu
miaka ya nyuma Tanga kulikuwa na viwanda vingi vilikuwa vinafanya kazi.
Alisema lakini hapo katika viwanda vingi vilikuwa
havifanyi kazi hivyo ziara hiyo italeta mageuzi makubwa katika kufufua viwanda
hivyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa watafanya kazi kwa karibu na Wizara kuhakikisha
malengo ya kufufua viwanda yanafanyika na kuweka mazingira wezeshi kwa
wawekezaji wanaowekeza mkoa wa Tanga ambao una mazingira bora ya uwekezaji kama
unavyofahama Bandari inafanya kazi kwa kiwanda kizuri sana.
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Kiwanda Ply&Panel
Limited Wazalishi wa PlyWood Hussein Moor alisema wanashukuru ziara hiyo ya Katibu
Mkuu katika kiwanda hicho ambacho kilikuwa kimesimama muda mrefu lakini kwa
sasa tayari wameagiza mashine mpya na nyengine zipo njiani na wanategemea
wataalamu watakuja kufunga mashine baada ya kufika zote.
Alisema kwamba ahaidi wanayoitoa kwa Serikali na
Wakazi wa Tanga kwamba kiwanda hicho
kitaanza uzalishaji mwakani 2026 huku akiwahaidi wananchi wa mkoa huo ajira
zitakuwepo nyingi za moja kwa moja,za mkataba na baadae pia wataleta mashine
nyengine mpya na kuwa na ziara ya ajira
Mwisho.
EmoticonEmoticon