Showing posts with label siasa. Show all posts
Showing posts with label siasa. Show all posts

MLAPONI AUTAKA UDIWANI KATA YA KIMANG'A

June 30, 2025 Add Comment

Joto la uchukuaji fomu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) linazidi kupamba moto ambapo sasa Ndugu Hamisi Mlaponi amechukua rasmi fomu kwa ajili ya nafasi ya Udiwani katika kata ya Kimang’a, wilayani Pangani, mkoani Tanga.


Mlaponi ni Mwanasayansi katika eneo la Jamii anayejihusisha na masuala ya misaada ya kibinaadamu na kuhamasisha mifumo ya hifadhi ya jamii hususani katika vijiji vilivyopo mkoa wa Tanga.

Pia, kuelekea malengo ya Kidunia ya Maendeleo Endelevu 2030, Mlaponi amadhamiria kutumia ushawishi wa kisiasa katika kuleta mabadiliko chanya kwenye masuala ya Afya, Elimu na Uchumi kwa wakazi wa kata ya Kimang’a 



Mbali na hayo Mlaponi pia ameapa kusimamia kikamilifu utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) 2025-2030 endapo atapata ridhaa ya kuwatumikia wananchi wa Kimang’a na kuwa chachu ya Maendeleo wilayani Pangani.

UMMY NDERIANANGA ACHUKUA FOMU UBUNGE VITI MAALUMU WANAWAKE WENYE ULEMAVU

June 30, 2025 Add Comment


Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Kundi la Wenye Ulemavu  Ummy Nderiananga  Juni 30,2025 amechukua fomu ya kugombea Ubunge Viti Maalum kundi la Wanawake Wenye Ulemavu.


Nderiananga amekabidhiwa fomu hiyo katika Ofisi ya  Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na Katibu UWT  Mkoa wa Kilimanjaro  Ndug. Jane Chatanda.


KADA WA CCM MACRINA AJITOSA UBUNGE VITI MAALUMU MKOA WA TANGA

June 29, 2025 Add Comment

 

KADA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga Macrina Clemens (kulia ) akikabidhiwa fomu na Katibu wa UWT Mkoa wa Tanga Anastazia Aman

Na Mwandishi Wetu,TANGA.

KADA wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Tanga Macrina Clemens amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea Ubunge wa viti Maalumu Mkoa huku akihaidi kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo.

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu alisema ameamua kuchukua fomu ili kuweza kutoa mchango wake kwa wananchi hususani Jumuiya wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi  (UWT) Mkoa wa Tanga.

Zoezi la kuchukua fomu limeanza katika ofisi za Chama cha Mapinduzi linaendelea nchi nzima ambapo watia nia tofauti wameendelea kujitokeza kwa ajili ya kuchukua fomu za Ubunge na Udiwani.




DKT.BITEKO AWAASA CCM BUKOMBE KUDUMISHA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

June 14, 2025 Add Comment


📌 Azindua maduka ya kisasa 31 Ushirombo


Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa,  Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amewaasa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Bukombe wasikubali kuvutana na kugombana bali wadumishe amani, kuendelea kuheshimiana na kulinda utu wao hususan katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani.

Dkt. Biteko amesema hayo Juni 14, 2025 wilayani Bukombe, mkoani Geita mara baada ya kuzindua maduka 31 ya kisasa yaliyopo katika eneo la Ofisi za CCM wilayani humo.

“Naomba niwakumbushe tena kwa sasa tunaukaribia mwezi wa Oktoba, 2025. Tunakaribia kuingia katika zoezi la Uchanguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, niwaombe tu kwamba, zoezi la uchaguzi ni zoezi la mara moja, lakini maisha yetu sisi yanadumu na yataendelea kudumu na kuna maisha baada ya kampeni na baada ya Uchanguzi. Hivyo, kwa heshima, nawaomba tuendelee kudumisha umoja, upendo na undugu uliopo baina yetu,” amesema Dkt. Biteko.


Katika hatua nyingine, amezungumzia ujenzi wa maduka hayo ya kisasa kuwa ni hatua kubwa kwa maendeleo ya wananchi wa eneo hilo la Ushirombo na maeneo mengine ya jirani kwa kuwa ni chanzo cha maendeleo na mzunguko wa fedha katika eneo hilo.

Amesisitiza “ Maduka haya yataongeza mvuto na hivyo kuongeza thamani ya eneo hili la ardhi pamoja na thamani ya jengo. Ukuaji wa eneo letu hili huchangiwa zaidi na shughuli za madini na shughuli nyingine za kiuchumi. Taarifa zinaonesha kuwa, Mkoa wa Geita umeonesha kasi kubwa zaidi ya ukuaji kutokana na shughuli za madini, na watu wanaochimba watapata huduma kwenye hili,”

Aidha, amewapongeza na kuwashukuru Mwenyekiti na Katibu wa CCM Wilaya ya Bukombe na Madiwani 23 kwa ushirikiano wao na kusema kuwa wamefanya kazi kubwa ya kuchangia ujenzi wa maduka hayo na kusema kuwa anafurahishwa kufanya kazi nao akiongeza kuwa wajumbe wa kata wanazotoka wanaweza kuwapima kwa kazi walizofanya. 

Dkt. Biteko amesema kuwa CCM katika wilaya hiyo itaendelea kuunga mkono mawazo mapya yatakayotolewa kwa ajili ya kusaidia maendeleo ambapo ametaja baadhi ya miradi ya ujenzi wa soko, stendi na barabara inayoendelea kujengwa wilayani humo inalenga kukuza uchumi wa wilaya na mkoa kwa ujumla.

Vilevile, Dkt. Biteko awaomba wanachama wa CCM kumuunga mkono kwa kumchagua Rais Samia na mgombea mwenza Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Geita, Nicholous Kasendamila  amewapongeza CCM Wilaya ya Bukombe kwa ujenzi wa maduka hayo na kusema kuwa hilo ni darasa na siasa ni uchumi na ni wajibu wa CCM kukiimarisha chama chao. 


Naye, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Mkoa wa Geita, Evarist Gervas amepongeza Dkt. Biteko kwa kuimarisha Chama katika wilaya  hiyo na kushirikiana vizuri na viongozi wa Chama kwa kuimarisha wilaya hiyo kiuchumi.


Awali akitoa taarifa ya ujenzi wa maduka hayo ya kisasa, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Bukombe, Leonard Mwakalukwa amesema kuwa Wilaya hiyo  inatimiza sera ya CCM ya miradi ya uwekezaji na kwa kutambua kauli mbiu ya siasa na uchumi, ilitekeleza wazo la ujenzi wa maboresho ya vibanda hivyo 21 vilivyokuwepo awali liliasisiwa na Mbunge wa jimbo la Bukombe Dkt. Biteko.


Amesema Dkt. Biteko alitoa wito wa kuwa na vitega uchumi zaidi vya Chama cha Mapinduzi na kutunza na kuboresha mandhari ya eneo la CCM la Wilaya ya Bukombe. Ndipo Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Bukombe ikapitisha pendekezo hilo.


Ametaja faida za mradi kuwa ni pamoja na CCM wilayani humo kukusanya mapato kwa wingi.


MWISHO

MBOGGO ACHUKUA FOMU YA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA TANGA KUPITIA ACT- WAZALENDO HUKU AKIHAIDI KUIREJESHA TANGA YA VIWANDA

May 27, 2025 Add Comment
Katibu wa Chama cha ACT -Wazalendo  Wa Jimbo la Tanga Mohamed Salim Ponda (kushoto)  akimkabidhi fomu ya kuomba kuteuliwa kuwa mgombea Ubunge Jimbo la Tanga mwanachama wao John Charles Mboggo  (katikati)  kulia ni Mwenyekiti wa Wazee Jimbo la Tanga (ACT Wazalendo) Zaharan Mohamed


Na Oscar Assenga, Tanga.

KADA wa Chama Cha ACT –Wazalendo Mkoani Tanga John Charles Mboggo amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa kuwania Ubunge katika Jimbo la Tanga kupitia chama hicho huku akihaidi kuirejesha Tanga ya Viwanda ambayo ni ndoto kubwa ya wananchi wa mkoa huo.

Akizungumza leo na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu hiyo alisema lenbgo la kuchukua fomu ya kuwania Ubunge ni kutaka kuhakikisha anatoa mchango wake katika kurejesha viwanda vya Tanga ambavyo wananchi wamekuwa na kiu navyo.

Alisema kwamba kwa sababu viwanda ni ajira  na nguvu kazi ya Tanga wanaongelea kuna vijana asilimia 68 ya vijana wakitumika kwenye viwanda watakuwa na uchumi kwenye Jimbo hilo na Mkoa kwa Ujumla.

“Tanga tunaamini sisi ni watu tunaamini watu wa kuleta maendeleo na ndio maana tunawahamasisha wananchi wenye sifa za kupiga kura kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye zoezi la kura  kwa lengo la kuwachaguoa viongozi watakaowaongoza”Alisema



Aidha alisema kwamba wasione aibu kutokana na uwepo wa hila mbalimbali wanajua namna ya kubaliana nayo ili kuhakikisha hazijitokezi kwenye mchakato huo.

Awali akizungumza Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Jimbo la Tanga  Anasi Mohamed Rweymamu alisema kwamba wanaendelea kuwakaribisha wagombe na kura zao wa maoni ndani ya chama ndizo zitakazoamua nani anaweza kupeperusha tiketi ya chama hicho kwenye nafasi ya Ubunge.

Alisema kwamba ACT Wazalendo ndio chama pekee ambacho kinaweza kupeperusha vyema Bendera yake katika kuibuka na ushindi kwenye nafasi ya Ubunge Jimbo la Tanga na Tanzania kwa upekee.

Naye kwa upande Katibu wa ACT  WaaJimbo la Tanga Mohamed Salim Ponda alisema kwamba wapo kwenye maandalizi ya uchaguzi kama chama hicho Taifa kilipotangaza kwamba zoezi la kuchukua fomu kutoka Aprili 18 mwaka huu mpaka 31 mwezi Mei katika nafasi za Ubunge na Udiwani.

Alisema kwamba katika uchaguzi huo wamejipanga kwamba wagombea watakao wapitisha katika kinyang’anyiro cha Ubunge katika Jimbo hilo watakuwa imara kuhakikisha wanapeperusha vyema bendera hiyo.

Mwisho.