“TPDC ni Shirika letu la mafuta ambalo limepewa jukumu la utafutaji, uendelezaji na uzalishaji wa gesi asi asilia hapa nchini. Nimepata maelezo hapa kupitia Wataalamu wetu kwamba kwa sasa Taifa letu limefanikiwa kugundua gesi asilia futi za ujazo trilioni 57, nab ado Serikali yetu kupitia TPDC inaendelea na utafiti katika maeneo mbalimbali nchini.”
“Kupitia miradi ya kimkakati ya utafutaji wa mafuta na gesi asiliainayotekelezwa na TPDC ni dhahiri kwamba, bado Taifa letu lina kiu ya kutafuta zaidi rasilimali za mafuta na gesi ambazo ni muhimu katika kukuza uchumi wa Taifa letu. Nitumie fursa hii kuwapongeza TPDC kwa kazi nzuri wanayoifanya na hasa katika Mikoa ya Lindi na Mtwara.” Aliongeza Kanali Sawala.
Kwa upande wake Mtaalamu wa Miamba kutoka TPDC Bw. Innocent Mvamba alieleza kuwa, “TPDC inaendelea na utafutaji wa mafuta na gesi asilia katika vitalu vya Lindi-Mtwara, Mnazi bay Kaskazini, Eyasi Wembere, SongoSongo Magharibi, 41B/41C pamoja na utekelezaji wa mradi wa bomba la EACOP ambao mpaka sasa umefikia asilimia 65.
Ushiriki wa TPDC katika maonesho ya Nanenane Kanda ya kusini, yenye kauli mbiu isemayo “Chagua viongozi bora kwa maendeleo endelevu ya kilimo mifugo na uvuvi 2025” umetoa fursa kwa wadau mbalimbali wa mikoa ya Lindi na Mtwara kupata elimu ya tasnia ya mafuta na gesi asilia pamoja na miradi inayotekelezwa na TPDC kwa niaba ya Serikali.





EmoticonEmoticon