Showing posts with label siasa. Show all posts
Showing posts with label siasa. Show all posts

MBUNGE MAKBEL AWATAKA MADIWANI KUSIMAMIA KWA WALEDI FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO

December 03, 2025 Add Comment





Na Oscar Assenga, TANGA

Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Kassim Amary Mbaraka Makbel amewataka madiwani kuhakikisha wanasimamia kwa waledi halmashauri ikiwemo fedha zote za miradi ya maendeleo zinazotolewa na Serikali ziende kwenye miradi husika.

Makbel aliyasema wakati akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari wakati wa mchakato wa kumpitisha Mgombea nafasi ya Umeya na Naibu Meya wa Jiji hilo ambapo alisema kwamba wanawashukuru vongozi wa CCM na kamati kuu kwa kumteua na kumpendekeza kuwa miongoni mwa wagombea.

Alisema kwamba lazima madiwani wahakikishe wanasimamia vema halmashauri kuhakikisha fedha zote za miradi ya maendeleo ya Serikali ziende kwenye miradi husika ikiwemo kutokuwa na ubadhirifu wa aina yote kuhakikisha miradi inakamilika na hilo jambo ambalo watalisimamia kwa ukaribu.

Alisema kwamba hatataka kuona matumizi mabaya ya Fedha za Umma bali ni kuhakikisha kila fedha zinatumika kulingana na taratibu zake ili ziweze kuleta matokeo yaliyokusudiwa

“Katika hili niwaambie Madiwani kwamba sitataka kuona matumizi mabaya ya fedha zaa umma ambazo zinaletwa katika Halmashauri hivyo lazima tuwe makini “Alisema

Awali akizungumza Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mhandisi Mwanaisha Ulenge alisema kwamba watakwenda bungeni kusukuma kwa nguvu kuhakikisha fedha zinakuja pamoja na kuhakikisha matumizi mazuri ya fedha zinazoletwa kwa ajili ya maendeleo ya watu kama ilivyo dhamira ya Rais Dkt Samia Suluhu ili kupeleka tabasamu kwa wananchi.

Naye kwa upande wake Mstahiki Meya Mteule wa Jiji la Tanga Selebosi Mhina Mustafa amehaidi kusimamia kikamilifu suala la mapato katika Jiji hilo ikiwemo kuzuia mianya ya upotevu wake kwa njia moja ama nyengine ili kuhakikisha halmashauri inakuwa na mafanikio makubwa.

Selebosi aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari ambapo alisema kwamba wanawashukuru vongozi wa CCM na kamati kuu kwa kumteua na kumpendekeza kuwa miongoni mwa wagombea.

Alisema kwamba hiyo ni imani kubwa ambayo walikuwa nayo juu yake huku madiwani wenzake wa Jiji hilo wakimthibitishia kwa kumpitisha kuwa mgombea wa nafasi hiyo na ndio mteule hivyo atakwenda Halmashauri kushirikiana na madiwaniwenzake kuwa chachu ya maendeleo.

“Kwa kweli nawashukuru sana kwa kuniteua kuwa mgombea na nafasi hii lakini niwaambie kwamba kubwa nitakwend kuzuia mianya yote ya upotevu wa mapato kwa njia moja ama nyengine wanaijua ili kuhakikisha halmashauri isimame kama Halamshauri”Alisema

Alisema kwamba katika kufanikisha jambo hilo watahakikisha wanakuwa makini katika suala la ukusanyaji wa mapato huku akiwaomba ushirikiano ili kuweza kutekeleza majukumu yao kwa tija na kufikia malengo waliojiwekea.

Aidha alisema pia atakwenda kusimamia kutekeleza ilani ya CCM na ndio muongozo wao na dira yao ya kwenda kuifanyia pamoja na kuwa wasimamizi wakuu wa fedha za miradi mbalimbali ambazo Mhe Rais Dkt Samia Suluhu amekuwa akizielekeza Tanga kuhakikisha zinatumika kwenye malengo yaliyokusudiwa na sio vyenginevyo.

“Lakini niwaombe wana Tanga ushirikiano,umoja pamoja na ubunifu katika kutekeleza miradi ya maendeleo na kuwa na vyanzo vipya vya mapato ili kuifanya Halmashauri yao iweze kupiga hatua kubwa za kimaendeleo.

“Tanga ni Jiji hivyo kuhakikisha kusimamia Bilioni 22 kwa Jiji la Tanga lenye viwanda karibuni 7 hadi 5 bado kwake ni ni fedha ndogo ipo haja ya kwenda kuzuia mianya yote ambayo kwa njia moja ama nyengine ”Alisema

Katika hatua nyengine Selebosi alizungumzia kuhusu uwepo wa tishio la maandamano Desemba 9 mwaka huu ambako aliwaambia madiwani kwamba wao ndio wanakaa na wananchi lazima viongozi wachukua hatua ikiwemo viongozi wa mitaa na watendaji wa kata ambao ndio walinzi wa amani katika maeneo yao.

“Katika hili lazima kwenye maeneo yenu tuisaidie serikali na kumsaidia Rais kuhakikisha hakutakuwa na maandamano yasiyokuwa rasmi kutokana na kwamba hayana tija kwa maendeleo “Alisema

Alisema kwambaa wanaofanya maandamano hawazuki tu bali wapo kwenye maeneo wanakutana na wana maeneo wanatokea hivyo lazima ifike mahali waisaidie Serikali kuhakikisha viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani hawavipi nafasi.

Awali akizungumza na waandishi wa habari Katibu Itikadi,Mafunzo na Uenezi Mkoa wa Tanga (CCM) Mngazija alisema kwamba alisema kwamba katika mchakato wa nafasi ya Meya na Naibu Meya wamewapitisha Selebosi Mhina Mustapha kuwa mgombea wa CCM baada ya kupata kura 24 kwa 14 dhidi ya mpinzani wake Hamza Bwanga.

Alisema kwamba katika nafasi ya Naibu Meya walimpitisha Khalid Rashid Hamnza kuwania nafasi hiyo baada ya kumgaragaza mpinzani wake Mwanaidi Chombo kwa kura 21 dhidi ya 16 .


Mwisho.

CCM TANGA KUUNDA KAMATI ITAKAYOCHUNGUZA CHANZO CHA KUFUNGIWA UWANJA WA CCM MKWAKWANI NA TFF

November 28, 2025 Add Comment



Na Paskal Mbunga, Tanga

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga Rajabu Abdurhaman ametangaza kuunda kamati maalumu itakayochunguza sababu zilizosababisha uwanja wa CCM Mkwakwani kufungiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutokuchezewa mechi.

Akizungumza na waandishi wa habari siku baada ya uwepo wa Taarifa za kufungiwa uwanja huo na TFF,Rajabu alisema kwamba tume hiyo itajumuisha kamati ndogo kutoka CCM,Maafisa wa TFF na baadhi ya wadau soka mkoa wa Tanga.

Alisema kwamba wameamua kufanya hivyo kutokana na kwamba waanaamini kuna uzembe ulijitokeza kwa wale ambao walipewa jukumu la kusimamia uwanja huo na kupelekea kukumbana na rungu hilo la TFF.

Aidha alisema kwamba ameshangazwa na hatua ya TFF kufungia uwanja huo kutokana na hivi karibuni waliufanyia marekebisho makubwa na kujiridhisha kwamba unaweza kutumika kwa ajili ya mashindano mablimbali ya ndani na nje ya hicho hivyo walishangazwa kuona taarifa hiyo.

“Nilikuwa nimesafiri nje ya mkoa wa Tanga kikazi lakini nimelazimika kuhairisha safari yangu ili niweze kushughulika tatizo hilo na ndio maana leo hiii nimefika hapa uwanja kujionea na kuzungumza nanyi wanahabari na kukubaliana na uamuzi wa TFF kwamba zipo dosari ambazo zinapaswa kurekebishwa na hili tutalifanyia kazi”Alisema

Katika hatoba yake fupi iliyojaa hekima alionyesha kutokuwa na imani na viongozi ambao wamepewa dhamana ya kusimamia uwanja hatua iliyopelekea kuwaita mbele ya wanahabari na wadau wengine watoe maelezo.

Awali akizungumza kabla ya mkaribisha Mwenyekiti huyo,Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga Mfaume Kizito alisema kwamba uwanja huo ulikuwa kwenye hali nzuri lakini alishtushwa na uamuzi ambao ulichukuliwa na TFF kuufungia uwanja huo.

Pamoja na kauli hiyo Mwenyekiti wa CCM Mkoa alimtaka Meneja wa Uwanja wa CCM Mkwakwani Akida Machai aeleze nini ambacho kimepelekea uwanja huo kufungiwa licha ya kufanyiwa maboresho makubwa katika siku zilizopita.

Ambapo Meneja huyo alidai kuwa moja ya changamoto iliysababisha hali hiyo ni kutokuwepo na maji ya kutosha kutokana na chanzo cha maji kwenye uwanja huo kukauka na kupelekea nyasi za uwanja kukauka.

Alisema kwamba changamoto nyengine ni uwepo wa mchwa katika eneo lenye majani na hivyo kuwalazimu kutumia dawa ya kumwagilia na kufanikiwa kuwaondosha


Mwisho.




MCC RAJAB APIGA KURA PANGANI,AIPONGEZA INEC KWA KUWEKA UTARATIBU MZURI WA UPIGAJI KURA VITUONI

October 29, 2025 Add Comment



Na Oscar Assenga,PANGANI.

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa (MCC) Rajabu Abdurhamani ameipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi(INEC) kwa kuweka utaratibu mzuri wa watanzania kupigia kura kwenye vituo mbalimbali hapa nchini.

Pongezi hizo alizitoa leo mara baada ya kupiga kura katika kituo cha Pangani Mashariki ambapo aliungana na wananchi wa eneo hilo kupiga kura kwa ajili ya kuwachagua viongozi mbalimbali akiwemo Rais,Wabunge na Madiwani.

Alisema kwamba ameanzia Pangani lakini anategemea baadae kwenye maeneo mengine na amejionea namna hali ilivyo katika vituo vya kupigia kura kutokana na mpango mzuri uliowekwa na tume na hivyo kuwawezesha wananchi kutimiza haki yao na msingi bila kuwepo kwa changamoto yoyote ile.

“Kwa kweli katika hili niwapongeze sana Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kwa kuweka utaratibu mzuri nimeuliza hapa nimeambiwa watu wanapiga kura na utaratibu uliowekwa ni mzuuri na hivyo kuwawezesha wananchi kutimiza haki yay a msingi bila vikwazo vyoyote”Alisema

“Lakini kabla ya uchaguzi huu tulipita kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kwa kipindi cha miezi miwili hivyo leo nimeona nitimize wajibu wangu wa kupiga kura na hivyo kuhamasisha wananchi kama viongozi tunapiga kuwa na wao kutoka kwa wingi kupiga kura”Alisema

Hata hivyo alisema kwamba wananchi ni vema kuendelea kujitokeza kwa wingi kutokana na hali ya amani,mshikamano umetawala na kila mmmoja anapata haki yay a kupiga kura katika maeneo waliopo.






CCM YASIMAMISHA JIJI LA TANGA WAKIFUNGA KAMPENI

October 28, 2025 Add Comment

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimefanya mkutano mkibwa wa kufunga kampeni za uchaguzi mkuu kimkoa.

Mkutano huo umefanyika jana Oktoba 27 katika eneo la Comercial na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi wa jiji hilo na kutoka maeneo mengine ya mkoa wa Tanga.

Mgeni rasmi alikuwa ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Rajab Abdurhaman.


Mkutano huo pia umehudhuriwa na wagombea wote wa ubunge wa CCM kutoka majimbo 12 ya mkoa wa Tanga, wakiongozwa na mwenyeji wao mgombea wa Jimbo la Tanga Mjini, Kassimu Amari Ambaraka (Anko Makbel).


Wengine walioshiriki ni wagombea udiwani kutoka kata mbalimbali za mkoa wa Tanga, viongozi wa ngazi mbalimbali wa CCM mkoa wa Tanga, wanachama, wananchi na wakereketwa wa chama hicho.


Umati wa wananchi ulianza kujitokeza katika eneo la mkutano kuanzia majira ya saa 8:00 mchana kwa ajili ya kushiriki shamramshamra za  ufungaji wa kampeni hizo, pamoja na kusikiliza hotuba za viongozi hadi shughuli hiyo ilipohitimishwa saa 12:00 jioni.

Mavazi ya njano na kijani yalitawala katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo, huku mabango na bendera za chama hicho zikipepea katika maeneo maeneo mbalimbali.

Wasanii mbalimbali, ngoma za asili, vikundi vya hamasa na nyimbo mbalimbali za hamasa za CCM zilipamba ufungaji huo na kuleta ladha ya aina yake.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Rajabu amewaomba wananchi wa mkoa wa Tanga kuipigia kura nyingi za ushindi wa kishindo CCM, kwani imetekekeza kwa vitendo ahadi zote ilizotoa katika ilani yake ya uchaguzi iliyopita ya 2020/2025.

Ametaja baadhi ya ahadi zilizotekelezwa na kuleta manufaa makubwa kwa wananchi ni,  uboreshaji wa huduma za kijamii kama ujenzi wa miundombini ya barabara, bandari,  hospitali na vituo vya afya, ujenzi wa shule mpya na madarasa kwa shule za msingi na sekondari, usambazaji wa maji na umeme hadi vijijini, kudumisha amani na utulivu na mengineyo mengi.

Aidha, amesema ilani mpya ya uchaguzi ya 2025/2030 imeahidi mambo mengi makubwa zaidi ya maendeleo, ikiwamo kuendeleza  ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli ya kisasa (SGR), upanuzi wa uwanja wa ndege wa Tanga, uboreshaji wa huduma za maji, umeme, afya na elimu na uboreshaji zaidi wa Bandari ya Tanga.

Nae mgombea ubunge Jimbo la Tanga Mjini, Kassimu amewaomba wanachi wa jimbo hilo kumpigia kura nyingi za ndio mgombea urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, yeye katika nafasi ya ubunge na wagombea wote wa udiwani wa chama hicho, ili waweze kushirikiana nao kuleta maendeleo makubwa zaidi.

Akitoa taarifa ya CCM mkoa, Katibu wa chama hicho mkoa wa Tanga, Jamal Abasi Kimji amesema chama hicho  kimefanya kampeni zake kwa amani na kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa na Tume Huru ya Uchaguzi.

Amesema katika kipindi hicho cha kampeni, wagombea wa chama hicho wamewafikia wananchi wengi na kuinadi vyema Ilani ya uchaguzi.

Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani unafanyika kesho.

#kazinaututunasongambele

#OktobaTunatiki

#Anko Makbel



DOYO ATANGAZA NEEMA KWA WAFANYABIASHARA KATIKA MASOKO,AHAIDI KUTOA MIKOPO ISIYOKUWA NA RIBA

October 26, 2025 Add Comment



Na Oscar Assenga,Tanga.

MGOMBEA Urais kupitia NLD Doyo Hassan Doyo amewahaidi wafanyabiashara katika masoko mbalimbali hapa nchini kwamba wakimchagua Octoba 29 serikali yake itatoa mikopo isiyokuwa na riba kwa wafanyabiashara hao.

Doyo aliyasema hay oleo Jijini Tanga wakati alipofanya ziara ya kutembelea masoko mbalimbali Jijini humo ikiwa ni kampeni zake za lala salama kuelekea Octoba 29 mwaka huu ambapo alisema watafanya hivyo ili wawe na mitaji isiyokuwa na matatizo.

Alisema leo kuna mikopo ya kausha damu inayozalilisha watu hivyo watahakikisha wanakuwa na ambayo haina riba na yenye heshima ambayo itatolewa na Halmashauri jambo ambalo linawaondolea mzigo ikiwemo msongo wa mawazo kutokana na madeni ya mikopo ya aina hiyo.

Akizungumza akiwa katika soko la Mlango wa Chuma Jijini humo alisema kwamba anataarifa zinazoeleza kwamba soko hilo liliingiziwa zaidi ya Milioni 200 lakini zimeliwa na soko halijajengwa hivyo wakimchagua akiwa Rais kwanza atawakamata viongozi wanaodaiwa kula pesa za soko hilo ili wamueleza fedha hizo zimepekekwa wapi.

Aidha alisema pia watakapopata Serikali watajenga soko la Ghorofa tatu ili kulipa hadhi soko hilo Kongwe ambalo linahitaji kuwa la Kisasa ili waweze kufanya biashara za bila kuwepo kwa changamoto zilizopo kwa sasa.

Alisema kwamba katika ujenzi wa soko hilo eneo la chini litakuwa la mbogamboga na katikati watu wa mchele na nafaka huko juu na watu wa nyanya na mambo mengine mtu akija sokoni anamaliza kila kitu.

“Sokoni sio sehemu ya kuuza tu mbogamboga na nyanya bali ni sehemu ya biashara zote mkinichagua kuwa tutakwenda kujenga soko la biashara na nyie muwe watu kwa watu kwa kuwa kwenye soko lenye hadhi na meza za kisasa”Alisema

Hata hivyo pia alimuombea kura Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga Ramadhani Mwaligo awe mbunge wa Jimbo hilo ili waweze kushirikiana kwa ukaribu kuweza kuwaletea mandeleo kwa wananchi.

Mwisho.

KIKWETE AHITIMISHA KAMPENI ZA CCM MAJIMBO MATANO YA UNGUJA, ASEMA CCM NI CHAMA CHA KUTENDA NA SIO CHA MANENO

October 26, 2025 Add Comment

 


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Makunduchi Bi. Wanu Hafidh Ameir wakati wa kufunga rasmi kampeni katika  uwanja wa Jambiani Jimbo la Paje, Mkoa wa Kusini Unguja. 

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akimnadi mgombea ubunge Mhe Issa Haji Ussi (Gavu) wa Jimbo la Chwaka, wakati wa kufunga rasmi kampeni katika  uwanja wa Jambiani Jimbo la Paje, Mkoa wa Kusini Unguja. 

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akimnadi  mgombea uwakilishi jimbo la Makunduchi  Dkt. Mwalimu Haroun Ali Suleiman wakati wa kufunga rasmi kampeni katika  uwanja wa Jambiani Jimbo la Paje, Mkoa wa Kusini Unguja. 
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akimnadi  mgombea uwakilishi jimbo la Paje Mhe Jaku Hashim Ayoub wakati wa kufunga rasmi kampeni katika  uwanja wa Jambiani Jimbo la Paje, Mkoa wa Kusini Unguja. 

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, aongea na mgombea  ubunge jimbo la Makunduchi Bi. Wanu Hafidh Ameir na mgombea Uwakilishi jimbo la Chwaka Mhe. Simai Mohamed Saidi Mpakabasi wakati wa kufunga rasmi kampeni katika  uwanja wa Jambiani Jimbo la Paje, Mkoa wa Kusini Unguja.



Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amesema CCM si chama cha maneno maneno bali ni chama cha vitendo, akisisitiza kuwa chama hicho kitaendelea kutekeleza ahadi zake kwa wananchi kwa vitendo.

 

Dkt. Kikwete alitoa kauli hiyo jana jioni katika Uwanja wa Jambiani, Mkoa wa Kusini Unguja, alipohitimisha rasmi kampeni za CCM katika majimbo matano ya mkoa huo ya Tunguu, Chwaka, Uzini, Paje na Makunduchi kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29 mwaka huu.

 

Akihutubia mamia ya wananchi waliofurika uwanjani hapo, Dkt. Kikwete alisema CCM imeendelea kuwa chama cha kuaminika kwa Watanzania kutokana na utekelezaji wa Ilani yake kwa vitendo na kwa ufanisi mkubwa.

 

Alisema kuwa Ilani ya CCM imefikiwa kwa zaidi ya asilimia 85 na miradi iliyosalia inaendelea kutekelezwa kwa kasi. “CCM si chama cha maneno, ni chama cha kutenda. Tumetekeleza Ilani yetu kwa zaidi ya asilimia 85, na miradi inayobaki inaendelea. Huu ndio uthibitisho kwamba ahadi za CCM ni deni, na tunalilipa kwa vitendo,” alisema Kikwete huku akishangiliwa na wananchi.

 

Aidha, Dkt. Kikwete aliwapongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kwa uongozi wao bora na utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo katika pande zote za Muungano.

 

Alisema viongozi hao wameonyesha uongozi wa wazi, wa kisasa na wenye matokeo chanya kwa wananchi. “Wananchi wanampenda kiongozi anayesema ukweli na anayetekeleza. Dkt. Samia na Dkt. Mwinyi wameonyesha uongozi wa vitendo,” alisema.

 

Dkt. Kikwete aliongeza kuwa chini ya uongozi wa viongozi hao, huduma za jamii zimeimarika kwa kasi kubwa, zikiwemo afya, elimu, maji na barabara. Alisema Zanzibar ya sasa imepiga hatua kubwa kimaendeleo ikilinganishwa na miaka kumi iliyopita, huku akitaja mafanikio kama kuongezeka kwa upatikanaji wa maji safi kutoka shehia 54 hadi 62, na ongezeko la uzalishaji wa samaki kutoka tani 5,606 hadi tani 12,155.

 

Pia alitaja mafanikio katika elimu ambapo kiwango cha ufaulu wa kidato cha nne kimepanda hadi asilimia 98.5, huku shule, maabara na hospitali mpya zikijengwa maeneo mbalimbali ya Unguja na Pemba. “Hospitali za Kitogani, Mwera Pongwe na Makunduchi ni ushahidi wa kazi nzuri ya serikali ya CCM,” alisema Kikwete.

 

Akiwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba 29, Dkt. Kikwete alisema ni muhimu kila Mtanzania kutumia haki yake ya kikatiba kwa amani na utulivu. “Usikubali mtu akuambie usipige kura, hiyo ni haki yako ya kikatiba. Ukiikosa, utamwachia asiye na nia njema ashinde,” alisisitiza.

 

Kikwete alisema serikali ya CCM itaendelea kuimarisha uchumi, kuongeza ajira zaidi ya 350,000, kukuza sekta ya utalii na kuanzisha hifadhi ya mafuta Zanzibar kupitia Ilani ya 2025–2030 yenye kaulimbiu ‘Kazi na Utu, Tunasonga Mbele’.

 

Aliwataka wananchi wa Zanzibar na Tanzania Bara kulinda amani na umoja uliopo, akisema CCM itaendelea kuendeleza misingi ya ASP na TANU ya usawa, umoja na maendeleo kwa wote.

 

“Wachochezi walijaribu huko nyuma hawakufaulu, na hawatafaulu kamwe. CCM imesimama kwa misingi ya Mapinduzi ya 1964 na itaendelea kulinda umoja wa Wazanzibari na Watanzania,” alisema.

 

Akihitimisha hotuba yake, Dkt. Kikwete aliwataka wananchi wote kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura na kuhakikisha ushindi wa CCM unapatikana kwa kishindo.

 

"Tarehe 29 Oktoba tujitengeze historia. Tuchague Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Hussein Ali Mwinyi kuwa Rais wa Zanzibar na wagombea wote wa CCM,” alisema huku akishangiliwa.

 

Katika mkutano huo wa kufunga kampeni, Dkt. Kikwete aliwanadi kwa nguvu wagombea wote wa chama hicho ikiwa ni pamoja na Bi. Wanu Hafidh Ameir, mgombea ubunge wa Jimbo la Makunduchi, pamoja na wagombea wa uwakilishi wakiwemo Issa Haji Ussi (Gavu) wa Jimbo la Chwaka, Simai Mohamed Said Mpakabasi wa Jimbo la Tunguu, na Saidi Azani Hassani (Msingiri) wa Jimbo la Uzini.

 

Kutoka Wilaya ya Kusini walihusishwa pia Dkt. Mwalimu Haroun Ali Suleiman (Makunduchi) na Jaku Hashim Ayoub (Paje), ambao wote walipata fursa ya kusalimiana na wananchi na kutoa salamu za kuhitimisha kampeni kwa matumaini makubwa ya ushindi.