‎WATU ZAIDI YA 5,000 WAPATIWA MSAADA WA KISHERIA NANENANE

August 11, 2025
‎Na Edward Winchislaus.
‎Watu  zaidi  Elfu tano  wamepatiwa msaada wa kisheria katika banda la wizara ya Katiba na sheria katika maonesho ya nanenane yaliyofanyika Nzuguni Jijini Dodoma tangu Agosti 1 hadi Agosti 10.2025.
‎Hayo yameelezwa  Agosti 10.2025 na Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya katiba katika wizara hiyo Bw.Prosper Kisinini wakati akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya nanenane jijini  Dodoma.
‎Amesema  Kati yao wanawake walikuwa zaidi ya 3,000 huku wanaume walikuwa  zaidi ya 2,000  na migogoro zaidi ya 100 imetatuliwa.
‎"Wizara ya katiba na sheria imetoa msaada wa kisheria kwa watu zaidi 5,526 ambapo wanawake walikuwa zaidi ya 3,408 na wanaume zaidi ya 2,473  na kushughulikia migogoro 103,"amesema.
‎Katika hatua nyingine Katibu mkuu wa wizara ya katiba na sheria Bw.Eliakim Chacha Maswi mewapongeza watendaji wa wizara hiyo kwa kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi hao.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »