Joto la uchukuaji fomu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) linazidi kupamba moto ambapo sasa Ndugu Hamisi Mlaponi amechukua rasmi fomu kwa ajili ya nafasi ya Udiwani katika kata ya Kimang’a, wilayani Pangani, mkoani Tanga.
Mlaponi ni Mwanasayansi katika eneo la Jamii anayejihusisha na masuala ya misaada ya kibinaadamu na kuhamasisha mifumo ya hifadhi ya jamii hususani katika vijiji vilivyopo mkoa wa Tanga.
Pia, kuelekea malengo ya Kidunia ya Maendeleo Endelevu 2030, Mlaponi amadhamiria kutumia ushawishi wa kisiasa katika kuleta mabadiliko chanya kwenye masuala ya Afya, Elimu na Uchumi kwa wakazi wa kata ya Kimang’a
Mbali na hayo Mlaponi pia ameapa kusimamia kikamilifu utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) 2025-2030 endapo atapata ridhaa ya kuwatumikia wananchi wa Kimang’a na kuwa chachu ya Maendeleo wilayani Pangani.
EmoticonEmoticon