
Na Linda Akyoo - Tanga.
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (TANGA UWASA) imepokea gari kwa lengo la utekelezaji wa mradi wa usimamizi wa kupunguza upotevu wa maji katika maeneo ya huduma kwa kushirikiana na Mamlaka za Maji nchini Uholanzi (VEI).
Akizungumza mara baada ya kupokea gari hilo Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (TANGA UWASA) Mhandisi Geofrey Hilly ameipongeza VEi Mkoa wa Tanga,kutokana na juhudi zao za kuhakikisha TANGA UWASA inakabiliana na upotevu wa maji kwa wakati.
Aidha Mhandisi Hilly amesema kuwa TANGA UWASA na VEi ujio wa gari hili unaenda sambamba na makabidhiano ya pikipiki na Maguta kama sehemu ya mradi huo.
Mhandisi Hilly amewashukuru VEi kwa jitihada zao ambazo zitakuwa chachu ya kuweza kukabiliana na upotevu wa maji kwa mafanikio ambapo mradi huo ni wa ushrikiano unaotekelezwa na Mamlaka nyengine Nchini Tanzania kiwemo Dodoma,Arusha Mwanza.
“Kwa sasa VEi wanafanya kazi kwenye Mamlaka nne na wanatoa ufadhili tofauti toafuti ambapo TANGA UWASA tunafadhiliwa na GIZ kupitia mradi wa "Green Smart City sasa" unaogharimu kiasi Cha shilingi Bilioni 3 ambao kwa sasa unaendelea lengo kuu ni kupambana na upotevu wa maji”Alisema Mhandisi Hilly
Kwa upande wake Mratibu wa VEi TANGA UWASA Mhandisi Violet Kazumba amesema kuwa VEi Mkoa wa Tanga wana furaha ya kufanikisha zoezi hilo la kukabidhi gari ambalo litakwenda kusaidia katika kazi ya kupambana na maji yanayopotea .
Alisema kwamba wanawapongeza Tanga Uwasa na wanamshukuru Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly kwa ushirkiano mkubwa na watumishi wote.
EmoticonEmoticon