*Asisitiza mabalozi kupandisha bendera za chama kwenye maeneo yao.
* Asema chama kinawajali na kuwathamini mabalozi.
Mahusiano kati ya maendeleo ya jamii na maendeleo ya kisiasa hayawezi kutenganishwa, kwani maendeleo ya kweli huanzia katika misingi imara ya uongozi wa wananchi wenyewe.
Kauli hiyo imesisitizwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, alipobainisha kuwa injini ya maendeleo ya chama na Taifa kwa ujumla ipo katika mashina ya CCM.
Dkt. Migiro amesema maendeleo ya kweli kwa wananchi huanzia katika mashina ya Chama hicho, akisisitiza kuwa jitihada zote za maendeleo ya kijamii na kiuchumi hupata nguvu kupitia uongozi wa ngazi za chini.
Katibu Mkuu huyo, ambaye ni mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo tangu chama kianzishwe, ameyasema hayo katika mkutano wake na Mabalozi wa Mashina wa CCM Wilaya ya Ilala, ikiwa ni hitimisho la ziara yake katika Mkoa wa Dar es Salaam yenye lengo la kuimarisha uhai wa CCM kuanzia mashinani, kwa kauli mbiu ya “Shina lako linakuita.”
Akizungumza na mabalozi hao, amesema mashina ndiyo ngazi ya kwanza inayowawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika mchakato wa maendeleo, kwa kuwa ndiko wanakotoka wananchi wenyewe na ndiko changamoto zao halisi zinapojadiliwa na kutafutiwa ufumbuzi.
Ameeleza kuwa mashina imara huwezesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa uwazi, ushirikishwaji na uwajibikaji, jambo linaloongeza imani ya wananchi kwa Chama Cha Mapinduzi na kuimarisha mshikamano wa kisiasa na kijamii.
Ameongeza kuwa viongozi wa mashina wana wajibu mkubwa wa kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao, akisisitiza kuwa uangalizi wa karibu wa miradi hiyo ndio msingi wa maendeleo yenye tija na yanayogusa maisha ya wananchi moja kwa moja.
Aidha, Mwanadiplomasia huyo amesema Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amepongeza kazi kubwa inayofanywa na Mabalozi wa Mashina, huku akibainisha kuwa chama kitaendelea kuwajali, kuwathamini na kuwatambua kama mhimili muhimu wa uhai na ushindi wa CCM kuanzia ngazi ya chini.

EmoticonEmoticon