Na Oscar Assenga,TANGA
JOPO la Mawakili wa Serikali 40
wanatarajiwa kutua mkoani Tanga mahususi kwa ajili ya kusikiliza kero sugu za
kisheria ambazo zitatolewa ufafanuzi wa kisheria na hatimaye kufungwa na kuweza kuzimaliza.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi,Batilda
Burian wakati akieleza kuhusu uzinduzi wa Kamati ya Ushauri wa Masuala ya
Kisheria ngazi wa Mkoa Bila Malipo itakayofanyika kwenye viwanja vya Tangamano
Jijini Tanga ikianza Machi 9 hadi 15 mwaka huu huku akiwataka wananchi wote .
Alisema kamati hizo zinalenga kutoka huduma kwa wananchi na
watuumishi wa umma ,viongozi wa umma na wengine bila kubagua ili kutatua
changamoto za kisheria zinazojitokeza huku akieleza itasadia kupunguza mashauri
au migogoro dhidi ya Serikali katika ngazi ya mikoa na wilaya.
“Lakini kama mtakumbuka Rais Dkt Samia Suluhu alituma jopo
la wanasheria kutoa Wizara ya sheria wakiongozwa na Waziri kwa ajili ya
kuzindua kliniki za sheria mkoa lakini ofisi ya Mwanasheria mkuu wa Serikali
alituma jopo la wanasheria kutoka ofisi yake na waliopo kwenye mikoa kushirikiana
na wanasheria wengine wa kujitolea hapa Tanga”Alisema .
“Kama mtakumbuka hivi karibuni Waziri Mkuu alianza ziara
ameenda Arusha na Manyara migiogoro ni mingi wenzetu hawa wamekuja kusaidia
kutoa suluhu za kisheria na kuwasaidia
wananchi na zitakutanaisha mawakili wa serikali na taasisi mbalimbali
kuwasaidia wananchi wenye changamoto mbalimbali”Alisema
Hata hivyo alisema kwamba huduma hiyo itawezesha kupunguza malalamiko kwa wananchi na hata jopo hilo likiondoka utaratibu huo utaendelea na zoezi hilo litafanyika bila malipo kwa hiyo wananchi wajitokeze kwa wingi wenye malalamiko ikiwemo mabando yenye malalamiko yawabebe na yawe na vielelezo vya kutosha.
Alieleza kwamba hiyo yote ni ni muendelezo wa kazi nzuri
anayoifanya Rais Dkt Samia Suluhu na wanaendelea
kumpongeza kuweza kulinda,kukuza na kutetea haki za wananchi wanyonge na
kupinga vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora na
kuhakikisha ukatili wa kijinsia unatokomezwa.
Mkuu huyo wa mkoa alisema pia lakini kuheshimu utawala wa sharia ambao ndio
msingi wa maendeleo kwenye mkoa huo wanaendeela kupongeza Ofisi ya Mwanasheria
Mkuu wa Serikali kwa kuhakikisha kamati ya ushauiri wa kisheria kwenye mkoa wa
Tanga inazinduliwa na kuanza kutioa huduma kwa wananchi wote bila kujali uwezo
wao wa kifedha .
Mwisho.



EmoticonEmoticon