MBUNGE MAKBEL AWATAKA MADIWANI KUSIMAMIA KWA WALEDI FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO

December 03, 2025





Na Oscar Assenga, TANGA

Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Kassim Amary Mbaraka Makbel amewataka madiwani kuhakikisha wanasimamia kwa waledi halmashauri ikiwemo fedha zote za miradi ya maendeleo zinazotolewa na Serikali ziende kwenye miradi husika.

Makbel aliyasema wakati akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari wakati wa mchakato wa kumpitisha Mgombea nafasi ya Umeya na Naibu Meya wa Jiji hilo ambapo alisema kwamba wanawashukuru vongozi wa CCM na kamati kuu kwa kumteua na kumpendekeza kuwa miongoni mwa wagombea.

Alisema kwamba lazima madiwani wahakikishe wanasimamia vema halmashauri kuhakikisha fedha zote za miradi ya maendeleo ya Serikali ziende kwenye miradi husika ikiwemo kutokuwa na ubadhirifu wa aina yote kuhakikisha miradi inakamilika na hilo jambo ambalo watalisimamia kwa ukaribu.

Alisema kwamba hatataka kuona matumizi mabaya ya Fedha za Umma bali ni kuhakikisha kila fedha zinatumika kulingana na taratibu zake ili ziweze kuleta matokeo yaliyokusudiwa

“Katika hili niwaambie Madiwani kwamba sitataka kuona matumizi mabaya ya fedha zaa umma ambazo zinaletwa katika Halmashauri hivyo lazima tuwe makini “Alisema

Awali akizungumza Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mhandisi Mwanaisha Ulenge alisema kwamba watakwenda bungeni kusukuma kwa nguvu kuhakikisha fedha zinakuja pamoja na kuhakikisha matumizi mazuri ya fedha zinazoletwa kwa ajili ya maendeleo ya watu kama ilivyo dhamira ya Rais Dkt Samia Suluhu ili kupeleka tabasamu kwa wananchi.

Naye kwa upande wake Mstahiki Meya Mteule wa Jiji la Tanga Selebosi Mhina Mustafa amehaidi kusimamia kikamilifu suala la mapato katika Jiji hilo ikiwemo kuzuia mianya ya upotevu wake kwa njia moja ama nyengine ili kuhakikisha halmashauri inakuwa na mafanikio makubwa.

Selebosi aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari ambapo alisema kwamba wanawashukuru vongozi wa CCM na kamati kuu kwa kumteua na kumpendekeza kuwa miongoni mwa wagombea.

Alisema kwamba hiyo ni imani kubwa ambayo walikuwa nayo juu yake huku madiwani wenzake wa Jiji hilo wakimthibitishia kwa kumpitisha kuwa mgombea wa nafasi hiyo na ndio mteule hivyo atakwenda Halmashauri kushirikiana na madiwaniwenzake kuwa chachu ya maendeleo.

“Kwa kweli nawashukuru sana kwa kuniteua kuwa mgombea na nafasi hii lakini niwaambie kwamba kubwa nitakwend kuzuia mianya yote ya upotevu wa mapato kwa njia moja ama nyengine wanaijua ili kuhakikisha halmashauri isimame kama Halamshauri”Alisema

Alisema kwamba katika kufanikisha jambo hilo watahakikisha wanakuwa makini katika suala la ukusanyaji wa mapato huku akiwaomba ushirikiano ili kuweza kutekeleza majukumu yao kwa tija na kufikia malengo waliojiwekea.

Aidha alisema pia atakwenda kusimamia kutekeleza ilani ya CCM na ndio muongozo wao na dira yao ya kwenda kuifanyia pamoja na kuwa wasimamizi wakuu wa fedha za miradi mbalimbali ambazo Mhe Rais Dkt Samia Suluhu amekuwa akizielekeza Tanga kuhakikisha zinatumika kwenye malengo yaliyokusudiwa na sio vyenginevyo.

“Lakini niwaombe wana Tanga ushirikiano,umoja pamoja na ubunifu katika kutekeleza miradi ya maendeleo na kuwa na vyanzo vipya vya mapato ili kuifanya Halmashauri yao iweze kupiga hatua kubwa za kimaendeleo.

“Tanga ni Jiji hivyo kuhakikisha kusimamia Bilioni 22 kwa Jiji la Tanga lenye viwanda karibuni 7 hadi 5 bado kwake ni ni fedha ndogo ipo haja ya kwenda kuzuia mianya yote ambayo kwa njia moja ama nyengine ”Alisema

Katika hatua nyengine Selebosi alizungumzia kuhusu uwepo wa tishio la maandamano Desemba 9 mwaka huu ambako aliwaambia madiwani kwamba wao ndio wanakaa na wananchi lazima viongozi wachukua hatua ikiwemo viongozi wa mitaa na watendaji wa kata ambao ndio walinzi wa amani katika maeneo yao.

“Katika hili lazima kwenye maeneo yenu tuisaidie serikali na kumsaidia Rais kuhakikisha hakutakuwa na maandamano yasiyokuwa rasmi kutokana na kwamba hayana tija kwa maendeleo “Alisema

Alisema kwambaa wanaofanya maandamano hawazuki tu bali wapo kwenye maeneo wanakutana na wana maeneo wanatokea hivyo lazima ifike mahali waisaidie Serikali kuhakikisha viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani hawavipi nafasi.

Awali akizungumza na waandishi wa habari Katibu Itikadi,Mafunzo na Uenezi Mkoa wa Tanga (CCM) Mngazija alisema kwamba alisema kwamba katika mchakato wa nafasi ya Meya na Naibu Meya wamewapitisha Selebosi Mhina Mustapha kuwa mgombea wa CCM baada ya kupata kura 24 kwa 14 dhidi ya mpinzani wake Hamza Bwanga.

Alisema kwamba katika nafasi ya Naibu Meya walimpitisha Khalid Rashid Hamnza kuwania nafasi hiyo baada ya kumgaragaza mpinzani wake Mwanaidi Chombo kwa kura 21 dhidi ya 16 .


Mwisho.

Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »