Na Mwandishi Wetu - Dar es Salaam
"Nyakati zinabadilika, sekta zetu za biashara zinabadilika, na miradi inabadilika – lakini dhamira yetu ya asili ya kuendelea pamoja na Tanzania haijawahi kubadilika."
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa CRJE (E.A) LTD na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Makampuni ya Kichina Nchini Tanzania (CEAT), Bw. Jiang Yuntao, wakati akizungumza katika Jukwaa la Maendeleo ya Kimataifa la Makampuni – Tanzania (Phoenix Global Development Forum for Enterprises–Tanzania) lililofanyika Oktoba 3, 2026 katika Hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam.
Jukwaa hilo liliandaliwa kwa pamoja na Phoenix TV na CEAT kwa kaulimbiu ya "Kugundua Afrika Mpya, Kuchunguza Fursa Mpya," na kuhudhuriwa na wageni takriban 100 kutoka serikalini, sekta binafsi na vyuo vikuu.
Miongoni mwa wageni wa heshima waliohudhuria na kutoa hotuba za ufunguzi walikuwa Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji; Bw. Shigeki Komatsubara, Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini Tanzania; na Mhe. Chen Mingjian, Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania.
Bw. Jiang alieleza kuwa historia ya CRJE nchini Tanzania inaanzia kwenye Reli ya Tanzania-Zambia (TAZARA), ambapo tangu mwaka 1969 kampuni mama ya CRJE, China Railway Construction Engineering Group (CRCEG), ilituma wafanyakazi 1,114 kushiriki ujenzi wa reli hiyo, ikijenga takriban mita za mraba 506,400 za majengo mbalimbali ikiwemo vituo 93.
Baada ya TAZARA kuanza kufanya kazi, CRCEG ilibakiza timu ndogo ya matengenezo, na mwaka 2000 ilisajiliwa rasmi kama tawi la Tanzania – mwaka ule ule Tanzania ilipozindua Dira ya Maendeleo 2025 – na mwaka 2013 ikabadilishwa jina na kuwa CRJE (E.A) LTD.
Alisema Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 iliyozinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan Julai 2025 inalenga kujenga Tanzania iliyo na ustawi, haki, ushirikishwaji na kujitegemea ifikapo 2050, ikiungwa mkono na mradi wa uhuishaji wa TAZARA Septemba 2025 na tamko la pamoja la China, Tanzania na Zambia Novemba 2025 la kujenga Ukanda wa Ustawi wa TAZARA.
Alisema CRJE itaendelea kuimarisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi kupitia miundombinu ya hoteli za nyota tano kama Kilimanjaro, Gran Melia na Park Hyatt, Daraja la Nyerere, Bandari ya Mtwara, umwagiliaji Iringa, umeme Geita, jengo la VIP Terminal 1 siku 75, Johari Rotana, na Uwanja wa Arusha wa AFCON mwakani, huku Watanzania wakichukua zaidi ya asilimia 90 ya ajira na kupitia Programu ya Kukuza Vipaji ya Ufundi wa Kichina.







EmoticonEmoticon