DED CHONDO AKABIDHIWA OFISI

October 08, 2026


Mapema leo tarehe 08/10/2026 Dkt. Jumaa Mhina amekabidhi rasmi ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Muheza kwa Bi. Naima B. Chondo ambaye aliteuliwa tarehe 29/09/2026.

Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji na kuhudhuriwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Muheza Bw. Mohamed Mfaki, Wakuu wa Idara na Vitengo.

Aidha makabidhiano hayo yaliambatana na hafla fupi iliyoandaliwa na ofisi ya Utawala kwa watumishi wote waliopo ofisi kuu kupata nafasi yakumkaribisha Mkurugenzi mpya na kumuaga Mkurugenzi anayeondoka.

Akizungumza katika matukio yote Bi. Naima amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kumuamini na kumpa nafasi yakuwatumikia wananchi wa Muheza.

Zaidi aliwataka watumishi wote kumpa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake ili kuhakikisha Muheza na wananchi wake wanapata maendeleo.

Katika hafla hio pia, Dkt. Mhina aliwashukuru watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza kwa ushirikiano waliompatia wakati wote katika utekelezaji wa majukumu yake, zaidi alimshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini kwa kipindi chote alichohudu kwa nafasi ya Ukurugenzi.



Share this

Related Posts

Previous
Next Post »