KAMPUNI ya Oryx Energies Tanzania imezindua kituo kipya cha mafuta eneo la Wazo jijini Dar es Salaam huku mkakati wa kampuni hiyo ukiwa ni kuendelea kusogeza huduma za nishati za mafuta na gesi karibu na wananchi.
Akizungumza leo Juni 15,2026 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kituo hicho,Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Energies Tanzania Iman Mtafya amesema mazingira bora ya uwekezaji yanayofanywa na Serikali katika sekta ya nishati ya mafuta na gesi imewezesha Oryx kuendelea kusogeza upatikanaji wa nishati hizo.
“Oryx ndio tunaongoza kwenye mtandao wa vituo vya mafuta na usambazaji wa gesi na tutaendelea kuiunga mkono serikali katika kuhamasisha matumizi ya nishati na uzinduzi wa kituo hiki ni mkakati wetu wa kuendelea kusogeza huduma zetu.
“Kwahiyo tunaendelea kuwekeza maeneo mbalimbali na tumeanza hapa Wazo na hivi karibuni tutafungua kituo kingine Dodoma ambacho kitakuwa umbali wa kilometa 40 kutoka Dodoma Mjini.Lengo ni kuonesha kama kampuni tunaendelea kuwafikia wateja kokote walipo, hata vijijini.”
Akieleza zaidi kampuni ya Oryx inajali usalama na katika kituo hicho wametumia teknolojia ya juu huku akisisitiza pia wanazingatia ubora wa bidhaa zao na Oryx ndio kampuni pekee yenye maabara ya kupima ubora wa bidhaa zao ili kuhakikishia wateja wanapoweka mafuta katika vyombo vya moto yanakuwa yamezingatia ubora.
Mtafya amesema pia kama Serikali inavyoendelea kuweka mazingira bora ya uwekezaji ndio maana unaona na wao wanaendelea kukua kwa panua huduma na sio Dar es Salaam tu bali na mikoani.
“Mazingira yaliyowekwa na Serikali kupitia Wizara ya Nishati wawekezaji tunapata msaada mkubwa wa kupanua wigo wa kusogeza huduma karibu na wananchi, katika sekta ya nishati tunaona Waziri wa Nishati anavyoendelea kuhamasisha uwekezaji katika sekta ya nishati .
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa CDT Oil na CDT Energies Boniphace Nasibu ambaye ndio msimamizi wa kituo hicho katika biashara ya mafuta,vilainishi pamoja na gesi amesema wameangalia jami inayozunguka eneo hilo na kuona kuna kila sababu ya kusogeza huduma.
“Kituo chetu kipo karibu Madale ambako kuna mashamba ya jeshi,kiwanda cha saruji cha Wazo pamoja na watu wa eneo la Wazo na kwa ujumla tumejiridhisha hapa ni sehemu sahihi ya kuwahakikishia wananchi kupata mafuta na gesi ya kupikia.”
Amewahakikishia wateja wao watapata huduma zote zinazostahili ili wafurahie huduma za Oryx zinazopatikana huku akiishukuru oryx kwa kufanikisha uwepo wa kituo hicho.
Wakati huo huo akizungumza kwa niaba ya wananchi wa eneo la Wazo Sheikh Amani Hamis amesema kufunguliwa kwa kituo hicho mbali ya kusogeza huduma za nishati ya mafuta pamoja na gesi pia imewezesha vijana wa eneo hilo kupata ajira kupitia kituo hicho.
Amesema pia anaishukuru Serikali kwa kutoa fursa kwa wawekezaji kuja kuwekeza nchini na hivyo wawekezaji hao kuwezesha wananchi wa Watanzania kunufaika na uwekezaji huo.
EmoticonEmoticon