MBUNGE MAKBEL AWATAKA WAKAZI WA JIJI LA TANGA KUTUNZA FUKWE ZA BAHARI

December 04, 2025


 Wakazi wa Jiji la Tanga wahimizwa kuzitunza fukwe za bahari hususan kukabiliana na changamoto ya uchafuzi wa taka za plastiki zenye kuathiri ikolojia ya bahari. 

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Tanga Mjini Kassimu Amari Mbaraka Makbel alipotembelewa na ugeni wa ofisi ya Makamu wa Raisi divisheni ya mazingira.

Makbel alihimiza juu ya utunzaji wa fukwe za bahari kutokana na umuhimu wake mkubwa kwenye sekta ya uchumi wa buluu na utalii wa fukwe.

Fukwe huhamasisha utaliii wa bahari haswa zinapokuwa safi huleta ajira na kuongeza pato la nchi katika sekta ya utalii.


Mbunge wa Tanga Mjini pia ameipongeza ofisi ya Makamu wa Raisi kitengo cha mazingira kwa kuichagua Tanga kuwa ni miongoni mwa fukwe za kimkakati kwenye uhifadhi wa ikolojia ya bahari na utunzaji wa Mazingira.

Amewahimiza wadau wa mazingira wote kuunga mkono juhudi hizo na kuendelea kudumisha zoezi la kusafisha na kuzitunza fukwe za bahari halikadhalika kuendelea kutoa elimu ya mazingira kwa jamii inayoendesha shughuli zake za kiuchumi kwenye fukwe za bahari


Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »