
📌 *Wapanda kutoka asilimia 95 hadi 96.16 katika kipindi cha robo mwaka*
📌 *Mhandisi Mramba asema ongezeko hilo linaakisi utoaji wa huduma kwa wananchi*
📌 *Apongeza Taasisi kuendelea kuboresha utoaji huduma kwa Wananchi.*
📌 *Asisitiza mitandao ya kijamii kutumika ipasavyo utoaji elimu Nishati Safi ya kupikia.*
Imeelezwa kuwa, utendaji kazi wa Wizara ya Nishati kupitia Taasisi inazosisimamia umezidi kuimarika na kufikia asilimia 96.16 katika kipindi cha robo nne ya mwaka 2024/2025.
Hayo yamefahamika wakati wa kikao cha Tano cha Tathmini ya utendaji kazi wa Wizara ya Nishati na Taasisi zake kwa robo nne ya mwaka 2024/2025 kilichofanyika jijini Dodoma na kuongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba.

Kufuatia tathmini hiyo, Mha. Mramba amewapongeza Watendaji wa Wizara ya Nishati na Taasisi zake kwa kuendelea kuboresha utendaji kazi kupitia utekelezaji wa miradi na utoaji huduma kwa wananchi hali inayoleta matokeo chanya katika Sekta ya Nishati.

Katika kikao hicho, Mha. Mramba amelipongeza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kuendelea kutoa taarifa kwa wananchi kwa wakati jambo ambalo limeleta ongezeko la kuimarika kwa utoaji huduma.

Vilevile,amekipongeza Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini cha Wizara ya Nishati kwa kutekeleza jukumu lao kwa ufanisi huku akisisitiza kuwa Kitengo hicho kipewe ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake ikiwa ni pamoja na kuhakikisha Idara, Vitengo na Taasisi zinawasilisha taarifa za utendaji kazi kwa wakati ili kitengo hicho kiongeza ufanisi zaidi katika kazi ya tathmini na hivyo kuboresha utendaji kazi.

Awali, Akiwasilisha taarifa ya tathmini ya utendaji kazi kwa Wizara na Taasisi zake, Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini, Wizara ya Nishati, Bi. Anita Ishengoma alisema kuwa kutoka zoezi la tathmini lianze kufanyika, limeleta ufanisi hasa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali pamoja na mipango ya Wizara kwani utendaji kazi wa Taasisi umeongezeka.

Aidha, Taasisi zilizofanya vizuri zaidi katika utendaji kazi kwa tathmini iliyofanyika katika kipindi cha robo nne ya mwaka 2024/2025 ni Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) - nafasi ya kwanza), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) -nafasi ya Pili) na Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA)- nafasi ya Tatu).
Mikoa ya Kitanesco iliyofanya vizuri katika utendaji kazi kwa tathmini iliyofanyika katika kipindi cha robo nne ya mwaka 2024/2025 ni Manyara (nafasi ya kwanza), Kinondoni Kusini ( nafasi ya Pili) na Simiyu ( nafasi ya Tatu).
Ilielezwa kuwa utendaji kazi wa mikoa ya kitanesco kwa ujumla umeimarika kwani hamna mkoa ambao utendaji wake umekuwa chini ya asilimia 91.83.
Katika Kikao hicho pia Taasisi ziliweza kuwasilisha taarifa za utendaji kazi wake.
![]() |
![]() |
![]() |
kikao hicho kilihudhuriwa na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara, Wakurugenzi wa Vitengo Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Wizara mbalimbali, Menejimenti ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake pamoja na Mameneja wa Kanda wa TANESC





EmoticonEmoticon