Na Oscar Assenga, TANGA
MRADI wa Kijana Togora tunakusikiliza unaotekeleza na Taasisi ya Afya Cheki chini ya Programu ya Tanga Yetu unaofadhiliwa na Botnar Foundation na kusimamiwa na Innovex umezinduliwa rasmi Jijini Tanga huku vijana zaidi ya 1000 wenye umri wa miaka 11 hadi 35 kutoka Kata 27 wanatarajiwa kunufaika.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo uliofanyika kwenye kituo cha Sayansi cha Stem Park Jijini humo, Mkurugenzi wa AfyaCheck na Msimamizi wa Mradi huo Dkt.Isaac Maro alisema kuwa mradi huo unalenga kusikiliza changamoto za maisha ya vijana Jijini Tanga kufuatia utafiti wa kina.
Mradi huo pia unalenga kusikiliza na kuwawezesha vijana kujadili kwa uwazi masuala yanayowagusa kwenye maeneo ya afya ya akili, afya ya uzazi na matumizi ya dawa za kulevya pamoja na vilevi.

Alisema ujio wa mradi huo ni baada ya utafiti walioufanya uliyobainisha changamoto nyingi hivyo kuona ni vyema kuweka utaratibu maalum wa kuwasikiliza vijana ili kujua shida zao pamoja na kuona namna ya kuzitatua.
Mradi wa Kijana Togora, Tunakusikiliza unalenga kusikiliza na kuwawezesha vijana kujadili wazi masuala muhimu ya ya Afya ya akili afya ya uzazi na matumizi ya dawa za kulevya na vilevi.

Akizungumza kuhusu mradi huo Dkt Maro alielekeza pongezi nyingi kwa vijana wa Tanga jiji kwa kupewa jukwaa lakusikilizwa sauti zao na hatimae kuzitatua.
Awali akizungumza Mwakilishi wa Botner Foundation Dkt Hasan Mshinda ambao ndio wafadhili wa miradi ya Tanga yetu ikiwemo Kijana Togora alisema kuwa katika utafiti walioufanya waligundua matatizo mbalimbali ilikwemo mimba za utotoni, matumizi ya Madawa ya kulevya ambayo ndio hatarisha maisha ya vijana ambao ndio nguvu kazi Taifa.

Aidha alisema kuwa Mkoa wa Tanga upo kwenye ngazi ya juu kwa matumizi ya dawa za kulevya hivyo kupitia mpango huo wa kijana Togora tunakusikiliza watajua kwanini wanajihusisha matumizi hayo na kwamba watapa elimu ya jinsi ya kuachana uraibu huo ikiwemo ushirikiano katika ngazi ya familia .
Kwa Naye kwa upande wake, Mrakibu wa Polisi wilaya ya Tanga Keneth Muhangwa alisema Jeshi la polisi wameanzisha pia mradi wa ngorika kwa kuunga mkono juhudi hizo ili kutokomeza matumizi ya dawa ya kulevya hivyo kwani mara nyingi wao wamekuwa wakidili na matokeo ya mambo yanayotoke katika jamii.

Alisema kwamba wameona ni vyema wao Jeshi la Polisi kuwa mradi mahususi kwa kujadili utoaji wa elimu juu ya matumizi ya dawa za kulevya ambapo ni vyema kila kijana atoe ushirikiano ili kutimiza wajibu wake katika kutoa taarifa ya uhalifu na wahalifu badala ya kuhusika kuafanya uhalifu unaotokana matumizivya dawa ya kulevya.
Hata hivyo akizungumzia mradi huo Afisa Maendeleo Jiji la Tanga Fatma Kinyumbi ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi huo aliwashukuru na kuwapongeza Botner faundation kwa miradi mbalimbali inayohusu vijana chini ya Tanga yetu.
"Mradi wa kijana Togora ni mradi Muhimu sana kwa vijana hivyo manapaswa kuchangamkia fursa za elimu ili wafikie malengo yenu hususani kupitia mradi wa kijana Togora ni vyema kujitokeza kwa wingi ili kupata fursa inayotokana na mradi huo "alisema Kinyumbi
Mwisho.
EmoticonEmoticon