NGORONGORO INATHAMINI MCHANGO WA WAONGOZA WATALII- NAIBU KAMISHNA MAKWATI

September 30, 2025


Na Mwandishi wa NCAA.

Karatu, Arusha.


Naibu Kamishna wa Uhifadhi Ngorongoro Joas Makwati ameeleza kuwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) inathamini mchango wa waongoza watalii (Tour Guides) kwa kuwa kundi hilo ndio linalopokea wageni, kukaa nao mda mrefu na kuwaongoza maeneo mbalimbali ya hifadhi yenye vivutio vya Utalii hadi siku wanapondoka 

Akizungumza wakati wa Kilele cha tuzo za waongoza Watalii 2025 kilichofanyika tarehe 27 Septemba, 2025 Karatu ambapo Ngorongoro ni sehemu ya wadhamini wakuu, Makwati ameongeza kuwa waongoza watalii ni wadau wakubwa na na wamekuwa mabalozi wazuri wa vivutio vya utalii vilivyopo Ngorongoro vikijumuisha Kreta ya Ngorongoro, Empakai, Olmot, Makumbusho ya Olduvai, mchanga unaohama, tambarare za Ndutu, wanyama wakubwa watano "Big Five" pamoja na vivutio vingine.

Ameongeza kuwa "Ngorongoro pamoja na shughuli za uhifadhi, inatunza utamaduni wa asili ikiwepo uhalisia wa chimbuko la binadamu wa kale, Nyayo za Laetoli, gunduzi mbalimbali za kihistoria, eneo lenye hadhi ya Jiopaki ambavyo vyote kwa pamoja vinafanya Ngorongoro kuwa kivutio bora cha utalii na moja ya Maajabu saba katika bara la Afrika" ameongeza Makwati.

 Kufanyika kwa tuzo za Waongoza Watalii Wilayani Karatu ni heshima ya  kuendela kuitangaza Ngorongoro kama kivutio bora za Utalii Afrika kwa wadau mbalimbali ndani na Nje ya Nchi.

Katika kilele cha tuzo hizo washindi wa mwaka huu ni Daudi Peter kutoka kampuni ya utalii ya “Gosheni Safari” aliyepata tuzo ya “Overall Best Tour Guide of the Year 2025” pamoja na Neema Amosi Ngowi (Singita) aliyepata tuzo ya “Best Female Tour Guide 2025”



Share this

Related Posts

Previous
Next Post »