Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko akiwasili katika ukumbi wa Diamond Jubilee - Dar es Salaam, kuzindua Mpango Kazi wa Taifa wa Haki na Ustawi wa watu wenye Ualbino pamoja na mkakati wa Taifa wa Teknolojia Saidizi unaolenga kuongeza ufahamu wa changamoto za watu wenye ulemavu.
Mikakati hiyo inazinduliwa leo Disemba 03, 2024 ambayo pia ni Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu ambayo Kauli mbiu yake ni 'Kukuza uongozi wa watu wenye ulemavu kwa ajili ya mustakabali jumuishi na endelevu'.
EmoticonEmoticon