MJUMBE WA BODI YA MSD ATEMBELEA WATEJA WA MSD KANDA YA TANGA

December 03, 2024


Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Bohari ya Dawa (MSD) Dkt. Rukia Mwifunyi amepongeza Kanda ya MSD Tanga kwa kuvuka malengo ya mauzo, katika robo mwaka ya kwanza ya mwaka kwa asilimia 12.

Mjumbe huyo wa Bodi, ambaye ni mlezi wa Kanda ya MSD TANGA amefuatana na  Meneja Huduma za Sheria MSD, Elisamehe Macha katika ziara ya kutembelea wateja wanaohudumiwa na Kanda ya Tanga,ziara ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka thelathini (30) ya utendaji wa MSD tangu kuundwa kwake.

Akizungumza na watumishi wa Kanda ya Tanga Dkt. Mwifunyi amemwelekeza Meneja wa MSD Kanda ya Tanga, Sitti Abdurahman kuhakikisha wanafuatilia kwa karibu madeni wanayowadai wateja wao.

Ziara hiyo inaendelea leo kwa kutembelea Hospitali ya Mkoa Bombo, na kituo cha afya Nkumba  kilichopo Wilaya ya Muheza, mkoani hapa.
Meneja wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Tanga, Sitti Abdulrahman. (kushoto) akitoa maelezo kwa Mjumbe wa Bodi ya MSD,  Dkt. Rukia Mwifunyi (katikati) ya jinsi wanavyopokea na kuhifadhi bidhaa wakati wa ziara ya kutembelea wateja wanaohudumiwa na Kanda ya Tanga Desemba 2, 2024. Kulia ni Afisa Maghara MSD Kanda ya Tanga, Alex Nsabila.Meneja wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Tanga Sitti Abdulrahman. (kushoto)  akisisitiza jambo wakati wa ziara hiyo.Meneja wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Tanga Sitti Abdulrahman. (kushoto) akitoa maelezo wakati wa ziara hiyo.  Kutoka kulia ni Kaimu Meneja wa Huduma kwa Wateja na Miradi Misonge (SPM) wa MSD, Dkt. Pamella Sawa na katikati ni Mjumbe wa Bodi ya MSD,  Dkt. Rukia Mwifunyi ambaye pia ni Mlezi wa MSD Kanda ya Tanga
Ziara hiyo ikiendelea
Meneja wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Tanga Sitti Abdulrahman. (kushoto) akitoa ufafanuzi wa jinsi ya maandalizi  na ufungashaji wa  bidhaa za afya na usambaji hadi kufika kwenye vituo. Kutoka kulia ni Dereva wa MSD, Musa Magnus, Afisa Maghara wa MSD Kanda ya Tanga, Alex Nsambila,  Kaimu Meneja wa Huduma kwa Wateja na Miradi Misonge (SPM) wa MSD, Dkt. Pamella Sawa,  Meneja Huduma za Sheria MSD, Elisamehe Macha na Mjumbe wa Bodi ya MSD,  Dkt. Rukia Mwifunyi ambaye pia ni Mlezi wa MSD Kanda ya Tanga 
Muonekano wa uhifadhi wa bidhaa za afya katika Ghara la MSD Kanda ya Tanga
Magari ya MSD yanayotoa huduma ya kusambaza bidhaa za afya Kanda ya Tanga,
Muonekano wa Ofisi ya MSD Kanda ya Tanga

Meneja wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Tanga Sitti Abdulrahman (mbele) akiongoza msafara wakati wa kuelekea kutembelea Ghara za MSD wakati wa ziara hiyo.
Utembeleaji wa Ghara hilo ukiendelea
Watumishi wa MSD Kanda ya Tanga wakiwa katika picha ya pamoja na wa Bodi ya Udhamini ya MSD, wakati wa ziara ya kutembelea wateja wanaohudumiwa na Kanda ya Tanga Desemba 2, 2024.
PICHA ZOTE NA MTANDAO WA SINGIDANI BLOG-TANGA

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »