MAKARANI WAONGOZAJI WAPIGA KURA MUHEZA WATAKIWA KUJIEPUSHA KUWA VYANZO VYA MALALAMIKO KUTOKA VYAMA VYA SIASA

October 25, 2025


Na Oscar Assenga,MUHEZA

MSIMAMIZI wa Uchaguzi Jimbo la Muheza Serapion Bashange amewataka makarani waongoza wapiga kura wajitahidi na kujiepusha kuwa vyanzo vya malalamiko kutoka katika vyama vya siasa wakati wa mchakato wa uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba 29 mwaka huu.

Bashange aliyasema hayo leo mjini Muheza wakati wa mafunzo kwa makarani waongoza wapiga kura ambapo alisema badala yake washirikiane vyema na mawakala wa vyama vya siasa watakaokuwepo vituoni kwa mujibu wa sheria.

Alisema ili wafanye kama timu ili kufanikisha uchaguzi kwenye vituo mbalimbali walivyopangiwa kutekeleza majukumu yao ikiwemo kuhakikisha wanafika mapema kwenye vituo watakavyopangiwa ili kukamilisha upangaji wa vituo kabla ya muda ewea upigaji kuwa

“Leo mpo hapa kwa ajili ya mafunzo ya makarani waongozaji wapiga kura ambao mtakuwa na jukumu la kutekeleza shughuli za uchaguzi ipasavyo katika ngazi za vituo 494 vilivyopo Jimbo la Muheza na Kata 37 kwa wale mnaosimamia zoezi hili kwa mara ya kwanza ni mategemeo yangu mtajifunza niwaase pamoja na uzoefu mlionayo baadhi yetu msiache kusoma katiba,sheria ,kanuni na miongozo na maelekezo mengine yanayotolewa na tume ya uchaguzi”Alisisitiza.

Aliwaleza kwamba nafasi waliopewa ya kuwa makarani katika uchaguzi huo ni nyeti na muhimu kwa mustakabali wa Taifa l hivyo wanategemea watazingatia sheria kanuni na maelekezo watakayopewa mpaka watakapokamilisha jukumu hilo la uchaguzi mkuu.

“Lakini pia niwaase kwamba hakikisheni mnazingatia unadhifu mvae vizuri mpendeze pia tumieni lugh nzuri pamoja na kutoa vipaumbele kwa wapiga kura wenye mahitaji maalumu watakaofika kwenye maeneo yenu ya kupigia kura”Alisema




Aidha pia aliwataka kuhakikisha wanafanya mawasiliano na Afisa Uchaguzi au Msimamizi wa Uchaguzi pale ushauri utakapohitaji kuhusiana na masuala ya uchagizi kwenye vituo vyao

“Lakini pia jazeni fomu za uchgauzi kwa ufasaha na ukamilifu kwa kuhakikisha mnaviweka kwenye bahasha husika kwa mujibu wa maelekezo lakini pokeeni vifaa vya uchagauzi na kuvitunza”Alisema






Share this

Related Posts

Previous
Next Post »