DOYO ATANGAZA NEEMA KWA WAFANYABIASHARA KATIKA MASOKO,AHAIDI KUTOA MIKOPO ISIYOKUWA NA RIBA

October 26, 2025



Na Oscar Assenga,Tanga.

MGOMBEA Urais kupitia NLD Doyo Hassan Doyo amewahaidi wafanyabiashara katika masoko mbalimbali hapa nchini kwamba wakimchagua Octoba 29 serikali yake itatoa mikopo isiyokuwa na riba kwa wafanyabiashara hao.

Doyo aliyasema hay oleo Jijini Tanga wakati alipofanya ziara ya kutembelea masoko mbalimbali Jijini humo ikiwa ni kampeni zake za lala salama kuelekea Octoba 29 mwaka huu ambapo alisema watafanya hivyo ili wawe na mitaji isiyokuwa na matatizo.

Alisema leo kuna mikopo ya kausha damu inayozalilisha watu hivyo watahakikisha wanakuwa na ambayo haina riba na yenye heshima ambayo itatolewa na Halmashauri jambo ambalo linawaondolea mzigo ikiwemo msongo wa mawazo kutokana na madeni ya mikopo ya aina hiyo.

Akizungumza akiwa katika soko la Mlango wa Chuma Jijini humo alisema kwamba anataarifa zinazoeleza kwamba soko hilo liliingiziwa zaidi ya Milioni 200 lakini zimeliwa na soko halijajengwa hivyo wakimchagua akiwa Rais kwanza atawakamata viongozi wanaodaiwa kula pesa za soko hilo ili wamueleza fedha hizo zimepekekwa wapi.

Aidha alisema pia watakapopata Serikali watajenga soko la Ghorofa tatu ili kulipa hadhi soko hilo Kongwe ambalo linahitaji kuwa la Kisasa ili waweze kufanya biashara za bila kuwepo kwa changamoto zilizopo kwa sasa.

Alisema kwamba katika ujenzi wa soko hilo eneo la chini litakuwa la mbogamboga na katikati watu wa mchele na nafaka huko juu na watu wa nyanya na mambo mengine mtu akija sokoni anamaliza kila kitu.

“Sokoni sio sehemu ya kuuza tu mbogamboga na nyanya bali ni sehemu ya biashara zote mkinichagua kuwa tutakwenda kujenga soko la biashara na nyie muwe watu kwa watu kwa kuwa kwenye soko lenye hadhi na meza za kisasa”Alisema

Hata hivyo pia alimuombea kura Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga Ramadhani Mwaligo awe mbunge wa Jimbo hilo ili waweze kushirikiana kwa ukaribu kuweza kuwaletea mandeleo kwa wananchi.

Mwisho.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »